Vurugu za Kidini Mbagala: Mtoto akojolea msahafu baada ya kuthubutishwa; makanisa yachomwa

Swali zuri sana Hilo Preta.
Hata waandamanaji walipaswa kutafuta kwanza majibu ya swali hilo. Nasikitika sana haikuwa hivyo. Maana kuchoma makanisa maana yake ni kwamba wameambiwa kuwa Wakristo wamemtuma mtotto huyo kufanya hivyo. Lasivyo, I doubt the nature, reasoning na imani ya waliohusika katika fujo hizo

hapa kuna mkono wa mtu.yule binti alichuchumaa akajolea msahafu.leo tena kijana wa seko nnaye anakojolea msahafu.
Hapa kuna issue bana si bure.
 
Wanasema ukipanda mchicha utavuna mchicha tu.

Naona wahanga wengine ndani ya nchi yetu, nao sio wengine ila ni wachaga.

Chuki inayojengwa dhidi ya watu hawa sioni watakuwa vipi salama. M

ungu ajalie taifa lake na watu wake.

Tusipochukua hatua stahiki mapema, Tanzania hapatakuwa mahali pema tena
 
Wana JF, "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo", samaki mkunje angali mbichi" hizi baadhi tu ya semi ambazo tumezizoea na hutumia kufundishia watoto wanaoonekana kuwa na tabia isiyo kubarika ktk jamii....mengi yanatokea sasa nchin kuanzia wakati wa sensa, uamusho, kidongo chekundu, mambo ya siasa, na sasa la mbagala, bahata mbaya hakuna kaul ya kiongoz wa nch kukemea haya yote...je tunaelekea ilipo Nigeria? Nn kifanyike ndugu zang, maana naona kuna maafa mbelen kama hakuna kauri!...nn maon yako hapa
 
Lowassa aliposema ukosefu wa ajira ni 'bomu' linalongoja kulipuka, sasa ndio watamuelewa alikuwa anamaanisha nini...
 
Kuna watu hawana credibility!

UKOSEFU WA HEKIMA NI JANGA KUBWA ZAIDI

Hii habari ni ishara ya matatizo makubwa zaidi. Hivi majuzi tumesikia kule Pakistan ambapo binti wa Kikritu nusura auwawe kwa sababu ilidaiwa kuwa alikufuru Quran kwa kuchana karatasi zake. Watu walikuja juu sana. Kumbe baadaye ikagundulika ni mzee mmoja wa Kiislamu ndiye aliyemset up yule mtoto ambaye ilidaiwa kuwa ana upungufu wa kiakili wa aina fulani. Baadaye ni yule Sheikh ndiye aliyekamatwa kwani ndiye aliyechana kurasa za Qurani na kuweka kwenye mfuko wa yule binti.

Sasa suala hili lina kila aina ya haja ya hekima. Unaposema kitabu hiki ni "kitakatifu" je mtoto anajua maana ya utakatifu? Je anajua hisia ambazo zinaendana na vitu hivi? Ni sawasawa na Wakatoliki wanaoamini komunyo ni kitu cha kiungu. Je mtoto wa dini nyingine anaweza kuelewa hili? Watoto wamekaa wanabishana kuhusu mambo ya vitabu hivi na mmoja anasema kitu ambapo akili ya kawaida haishawishiki; kwamba ukifanyia hivi basi unageuka panya. Mtoto yule mwingine udadisi umemshinda anasema 'haiwezekani'. Yule mwingine akiamini kabisa kuwa hilo hutokea akaenda kuchukua kitabu na kumletea huyu mwingine (vinginevyo huyo mtoto wa Kikristu alitoa wapi hiyo Quran?). Yule akajaribu na wote wakakaa hapo kuangalia kama atageuka mnyama. Hakugeuka!

Kama angegeuka kuwa panya yule mtoto mwingine angeelezeahilo tukio na badala yake eneo zima watu wangerindima kwa kisa cha mtoto aliyekojolea Quran ageuka panya! Sasa, haya mabishano yalikuwa ni ya kitoto na yasiyo nahekima yoyote. Watu wazima walipoitwa kuoneshwa kilichofanyika (kama ndivyo kilivyofanyika) walitakiwa kuonesha hekima ya kulishughulikia. Walitakiwa wawaeleweshe hawa watoto umakini na sensitivity ya vitu hivi na kwanini ni makosa kumtaka mtu akufuru kitabu cha Mungu ili uone nini kitamtokea na ni kosa pia kukubali jaribio hilo kwani linagusa imani za watu.

Hili jambo wala lisingefika hapa kabisa. Badala yake tunashuhudia mavuno ya mbegu ya udini. Mavuno ambayo watawala wetu wameyapanda na sasa hadi watoto wanavuna. Badala ya watoto wetu kuishi kwa kuaminiana na kupendana urafiki wao umetiwa mashakani na tukio hilo litaacha alama katika maisha yao yote. Na kama walikuwa ni marafiki wa karibu basi siyo tu wamepoteza urafiki kwa sababu ya ujinga wamejenga mpaka mpya kati ya Wakristu na Waislamu.

Yote haya ni kwa sababu ya kukosekana viongozi wenye hekima. Ndio maana binafsi ninalia sana na ukosefu wa hekima kama tunu ya muhimu zaidi kwa viongozi wetu. Leo watajaribu kutaka wananchi watulie kwa sababu sisi sote ni ndugu; lakini wakati mbegu za udini na chuki dhidi ya Wakristu zinapandwa kila siku wako kimya. Wanakuwa kimya pale ambapo Waislamu wanaona wanaonewa na kukandamizwa na mfumo wa kifisadi ambao wanaona umewabeba sana Wakristu! Matokeo yake ndiyo haya. Na tusipoangalia yatazidi kwa sababu endapo vijana wa Kikristu nao wakiamua kuchoma Misikiti au tutakuwa tumefika kule ambako niliwahi kuandika nyuma - Tanzania kufuata njia ya Nigeria.

Lakini cha kukwaza zaidi ni kuwa taarifa kwamba mtoto anayedaiwa kufanya hivyo kumbe ni Muislamu zinatosha kuthibitisha kuwa hekima inahitaji watu kutulia kwanza na kupata ukweli wote badala ya kupaparika na kuwahi kuhukumu watu. Sasa kama ni kweli mtoto aliyefanya hivyo ni Muislamu, hawa waliochoma makanisa wataenda na kuchoma misikiti? Au hawatochoma kwa sababu ni Muislamu "mwenzao"? Au wataamua kwenda kuchoma nyumba yake tu? Lakini watafanya nini kwa makanisa ambayo yamechomwa wwatasaidia na kujitolea kuyajenga tena baada ya kuyaharibu?

Kuna ugumu gani kwa watu kusubiri na kupata taarifa zote kwanza kabla ya kuchukua uamuzi wa kisheria au kisiasa (kuandamana n.k). Itakuwaje kama watu wangeuawa katika hili na baadaye igundulike kuwa ilikuwa ni watoto tu ambao walihitaji kuwekwa sawa tu? Kama kweli mtoto aliyefanya hivi ni Muislamu basi kilichotokea ni ushahidi usiopingika wa udini uliotukuka. Maana kusikia tu "mkristu kafanya hivi" basi Wakristu wote wamekwekwa hatiani!

Tuombe hekima zaidi kuliko kitu kingine kama alivyofanya Mfalme Suleiman (AS)

Mimi Mwanakijiji-Facebook Status.

https://www.facebook.com/mwanakijiji/posts/10151196014096156
 
Hivi jamani hizi vurugu zote na kutaka kuuana tunamjua huyu Mungu? NANI kawahi kumuona Mungu na kwa namna gani?Kweli tutakuja kuumbuka simu moja kwa haya matendo yetu.....
 
ndugu zangu katika jf nimedokezwa sasa hivi kuwa kanisa TAG Mbagala kwa makamu askofu mhiche Waislam wamevamia kanisa kuvunja madhabahu na kuchoma moto magari na askari nimeambiwa wapo eneo hilo. inasemekana sababu ni mtoto mmoja wa muumini alikojolea msahafu. wale wanaoishi maeneo jirani naomba mtujuze au wenye taarifa zaidi mtujuze. Nawakirisha!.
 
Hivi nyie ndugu zetu ktk Adam, allah si amewaambia kwamba mazuri na mabaya yametoka kwake? Mnachoma makanisa mnaacha aliyeleta ubaya! Halafu kawahimiza kwamba muislamu akikasirika akatawadhe ndio kutawadha huko?
 
Quran yetu haitufundishi hivyo eti tumuache mungu ajitete mwenyewe na kwa hali hii vita vipo njiani


Ona Waislamu wenye busara wanavyowaza tofauti:

wote wana makosa -

1 ) aliyekojolea

2)aliyebishana mwinzie akakojolea ...

3)wanaoandamana na kuvunja amani...

Ila sidhani vurugu, na kuchoma iwe kanisa au nyumba yoyote isitoshe kumuuwa huyu kijana ni suluhisho ..

muslims we are supposed to go back and read the Qur'an! how to deal na issues hizi .. kila kitu kipo wazi! jazba hazitatufikisha mahala ...

“Be tolerant, command what’s right, pay no attention to foolish people” [7:199]

“The Servants of the Lord of Mercy are those who walk humbly on Earth, and who, when the foolish address them, reply ‘Peace’” [25:63]

“Call people to the way of your Lord with wisdom and good teaching, and argue with them in the most courteous way” [16:125]

“We have spared you those who ridicule you” [15:95]

“Do not revile those they call on beside God, so they, in their hostility, revile God, without knowledge” [6:108]
NAPITA ...!
 
attachment.php

Baadhi ya waandamanaji wakiwa jirani na Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala jijini Dar leo.
 
da ndugu zetu wanapenda fujo hawa vingap huwa hatufuatilii leo hiii mmmmhhhh kunya anye kuku akinya bata kaaarishaaaa mpo juu ndugu zetu
 
Imani ni kuwa na uhakika na unachokiamini hata kama hakionikani.Dogo aliyekojolea msaafu hakuwa mweu kwa kuwa hana uhusiano na msaafu haina haja waislamu kutumia nguvu wanazotumia wakitaka ushauri zaidi wamuone mzee kingunge.
 
Wanasema ukipanda mchicha utavuna mchicha tu.

Naona wahanga wengine ndani ya nchi yetu, nao sio wengine ila ni wachaga.

Chuki inayojengwa dhidi ya watu hawa sioni watakuwa vipi salama. M

ungu ajalie taifa lake na watu wake.

Tusipochukua hatua stahiki mapema, Tanzania hapatakuwa mahali pema tena


Mkuu mimi sio mchaga kabisa wala si wa kanda ya kaskazini, lakini hawa jamaa wako fit kwa kila anga hapa tanzania.

wachaga wamejaliwa elimu

wachaga wamejaliwa fedha ni wafanyabiashara mashuhuri

Wachaga wamejaliwa kumjuwa mungu.


Lakini hawajamaa kama utajifanya kuwakurupukia na wakathibitisha hivyo kwamba unawatesa, kuwanyanyasa na

kuwaangamiza hakika umekwisha amini nakuambia wanauwezo kufanya malipizi ya maangamizi kiasi kwamba dunia

nzimaikasikitikia, believe me. Ninachowapende wachaga wanaheshima na wanaheshimu utu wa mtu,

hawakurupuki na wanahekima.
 
wakati mwingine Moderators mjifanye hamkaoni kale kakalamka kutupigeni BAN!! manake mmmh.. ban nje nje tu hapa.. mie hata sijui kwakucoment tu hivi yatanikuta ma ban..!! ila Nijualo Tuache Jazba..

Mhe: Rais, nadhani ni wakati wa kufanya Jambo, nahisi Kuna Kundi Haram wanatumia Dini kama kigezo cha kufyatua Upuuzi wao ili kuufanya utawala wakoutetereke. Usipokuwa na akili za kujaa sana na kujua jinsi ya kuwatendea watuhawa Joto la amani litazidi kupanda siku hata siku na hatimae unajua Kitachotokea.

Uislam sidhani kama unaunga mkono Bugudha hizi, na wapo waislam wanaoujua uislam ila wako wachache ambao ni mamluki wa dini, wana lao hawa, nchi isitawalike.. Usikae ukatulia.. nisikilize , soma hapa kwa makini, Fanyajambo.. Kumbuka Utawala wa Mwalimu Nyerere ulianza kwa kuzungukwa na Waislam pande zote, wazee hawa walikuwa wastaarabu kiasi cha kuafiki muungano na Kumweka mkristu yule kama Kinara wa Muungano pasina shaka kwa miaka mingi tu,Kulikoni leo hii, wakati ambapo mseto umekuwa mkubwa nchini, Kweli hakuna akiliza kutosha kunyamanzisha ghasia hizi????

Mweshimiwa sana, Kumbuka jambo hili limegusa moyo wa kitaifa, si la kuwa achiaw engine walishughulikie au litajimaliza lenyewe, si hata kidogo, jambo hililinahusu moyo wa nchi na Raisi ndiye mwenye mamlaka na moyo wa nchi si busarausiinuke kitini pako na Kuchukua hatua kwa akili iliyo makini sana.


Inashangaza sana ha maki wakati WAO kila siku ni kutoa matsuri dhidi ya ukristo na HAKUNA hatua zozote zinazochukuliwa, shame!!! ! Hadi iifikie Hali ya Rwanda NDIpo tutakapochukua hatua????
 
wote wana makosa -

1 ) aliyekojolea

2)aliyebishana mwinzie akakojolea ...

3)wanaoandamana na kuvunja amani...

Ila sidhani vurugu, na kuchoma iwe kanisa au nyumba yoyote isitoshe kumuuwa huyu kijana ni suluhisho ..

muslims we are supposed to go back and read the Qur'an! how to deal na issues hizi .. kila kitu kipo wazi! jazba hazitatufikisha mahala ...

“Be tolerant, command what’s right, pay no attention to foolish people” [7:199]

“The Servants of the Lord of Mercy are those who walk humbly on Earth, and who, when the foolish address them, reply ‘Peace’” [25:63]

“Call people to the way of your Lord with wisdom and good teaching, and argue with them in the most courteous way” [16:125]

“We have spared you those who ridicule you” [15:95]

“Do not revile those they call on beside God, so they, in their hostility, revile God, without knowledge” [6:108]



NAPITA ...!

Well said! Haya ndo mafundisho watu wanapaswa kujifunza
 
Back
Top Bottom