Vurugu za jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.

Nasubiri Katiba mpya! SPIKA asiwe Mbunge... ujinga huu utakoma. Anatumia nguvu kuwatoa nje na mara baada ya kugundua kachemsha anajidai nimewasamehe, CCM badilikeni, Wapinzani badilikeni.
 
nakereka na hili swala kila mtu anachangia upande wa chama chake embu tuangalie tanzaina kama
tanzania huyu ndugai huyuuuuuuuu ipo siku yake tuuuu we subiri tuuu,
 
Mbona Lukuvi huwa anasimama muda wowote anaotaka na ndugai hamwambii kaa chini. Ameshaingilia hotuba nyingi tu za kambi ya upinzani na ndugai hasemi neno. Acha maneneo yako yasiyotaka kujenga bali kubomoa.

Simama na tetea hoja sio 'mbona'. Bunge linataratibu zake kama Lukuvi aliingilia hotuba ndio nini sasa? Mbowe nae afanye ivo.
 
Guys, historia ni mwalimu mzuri sana, hivi ndugai na makinda (hizo herufi ndogo kwenye hayo majina ni makusudi na sio bahati mbaya) walichaguliwa na nani vile?
 
kama ndugai angekuwa na akili kama za sugu bunge lingepigana kabisa lakini ndugai ni mstaarabu ndiyo maana jimbo likabaki salama wewe unachofanya ni umajinuni kwa kujifanya hujui ukweli japo unaujua,
 
Ndugai ana inferiority complexion na imemfanya awe aggressive when it comes to challenges from opposition. Nachokiona, huwa anaathiriwa na hisia za ukomozi kiasi ana-loose control.

Wabunge wa CCM na wa chama mke chao ni wanafiki na hawana wanacholenga bungeni zaidi ya kukataa kila litakalosemwa na CDM, liwe lenye msaada ama lah, wao jukumu lao ni kulikwamisha.

Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, leo hii unaunda Bunge Maalum kwa ajili ya makundi mbali mbali ya kijamii, halafu wawakilishi wa makundi hayo wasichaguliwe na wenye makundi wenyewe bali wachaguliwe na mtu ambaye wanaenda kupingana na mamalaka yake, ni nini hicho kama sio unafiki mbaya uliopitiliza mahitaji ya unafiki ya nchi nzima?

CCM walipoona ongezeko la wabunge wa CDM bungeni, walifanya kila njia kuona kuwa Samwel Sitta hawi spika ili waweze kuweka such unfit persons on chair waweze kupitisha hoja dhaifu kwa ubabe.

Na kuna kitu kinanishangaza sana: MBONA NAIBU SPIKA ANAENDESHA VIKAO VINGI VYA BUNGE AS IF SPIKA HAYUPO?
Bunge linaendesha na sheria na kanuni haliendeshwi kama disco.

Tatizo kubwa la Mbowe ni elimu hauwezi kuwaongoza watu wakati hauna elimu.

Akili ndogo kuongoza akili kubwa.
 
Bunge HALIENDESHWI kwa matakwa ya Mbowe au mbunge mwingine yeyote. Bunge huendeshwa kwa kanuni za bunge na ni wajibu kwa wabunge kutii kanuni hizo.
kanuni hizo ni pamoja na kutoa nafasi kwa KUB kuzungumza. Sio hisani ni kanuni!
 
chadema bwana mlitanka ndungai afanye nini,

kama zoezi la kupiga kura lilienda vizuri nini tena mlitaka, ahairishe bunge ili kila siku mdiskasi mada ile ile,
 
ni mauaji aliyofanya ******, yanamuandama

'Gonjwa la kudumu, na mauaji aliyofanya'!!! Taifa linongozwa na watu wenye DHAMBI MBAYA ktk maisha yao, hatuwezi pata busara, hekima wala weledi. Wameoza kwa kila kitu.
 
With a light touch - makosa ni kumwalika bondia Francis Cheka Bungeni maana aliwahamasisha kupigana ngumi! hata hivyo nakuunga mkono kabisa kuwa mabadiliko ya mfumo kuingia vyama vingi hayajabadilisha 'mind-set' ya watu wengi na hasa walioko kwenye Chama tawala kwani bado wnatembea na Party Supremacy. Naibu Spika anashangili na kujisifu kutoa amri inayozua vurugu bungeni na kuona kwake kashinda! Ni ajabu! Lakini ukiangalia matukio yenyewe ni dhairi pande zote zilikuwa zimeandaa yaliyotokea. Upinzani walidhamiria kusimamisha mjadala na watawala (kwa kutumia naibu Spika) walikuwa tayari kwa kuwatoa nje, na askari waliandaliwa kabisa kwa shughuli hiyo.

Tatizo kuu na la msingi ndio liko hapo....laiti kama ubadilishaji wa kanuni ungebadilisha pia fikra zao...hii hegemeny ya chama tawala inaleta maafa makubwa kama haya....na hii inaakisi hali ilivyo pia uraiani kuhsuu utendaji wa viongozi
 
Bunge limeingia katika historia ya kuwa na viongozi wapuuzi kuliko ilivyowahi kutokea/kudhaniwa itakuwa.
 
Ndugai ni Mtu Wa hatari sana anaye lazimisha apate u speaker full kwa kuwanyanyasa wapinzani.kwa uelewa wangu kiongozi Wa kambi ya upinzani bungeni ni sawa na waziri Mkuu ktk shughuli za bunge
 
Wana JF, mara nyingi ikitokea sintofahamu na ngumi kupigwa, Job Ndugai huwa ndiye alikalia kiti, hii inatokana na nini. Ni mara chache sana kutokea kuwa kubwa kama ya jana kama Makinda akikalia kiti.
 
Kwanza kabisa kaka spika ndo mkuu wa bunge kwa kifupi bunge ni himaya yake. Waziri mkuu ni msimamizi wa shughul za serikali bungeni kumbuka excative na parliament ni vitengo tofauti excutive kinaongozwa na rais na bunge n spika... kwa hiyo hata kama ni wazir mkuu akiambiwa akae bungen hana budi akae..ingawa nauhakika wazr mkuu hawez kungangania kusimama kutoa hoja. Pili sina uhakika na suala la waziri mkuu kuwa sawa na Kiongoz wa kambi ya upinzan hyo ni nonesense mkuu. Tatu na mwisho bungeni kuna kanuni nadhan kila mbunge anazijua kwa nn usifike wakati wa kusema ukwel kuwa mbowe angetakiwa kukaa chini afuate kanuni? Spika amruhusu kuongea ndo asimame. Acheni ushabiki vijana hausaidii ni wakati wa vyama pinzani kuwa makini na matendo yao ili tuwaamini na kuwapa nchi. Hatuwezi kuwapa nchi watu wanaokurupuka na kufanya mambo kitoto.
 
Back
Top Bottom