Vurugu za jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,451
Wanabodi,

Mwaka mmoja uliopita niliwahi kuleta hoja hii humu Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Leo nimeikumbuka kufuatia vurugu za jana bungeni!.

Chanzo cha vurugu zile ni "Ukosefu wa Busara Ndogo Tuu toka kwa Naibu Spika!".

Tangu tumepata uhuru, Tanzania imekuwa nchi ya chama kimoja kwa kipindi kirefu, tulipoingia mfumo wa vyama vingi ile 1992, tulifanya marekebisho tuu ya kanuni, ila hatukuweza kufanya mabadiliko ya "mind set" toka mfumo wa chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi, hivyo hali hii imeendelea mpaka sasa kwa CCM ambayo ndio chama tawala, kuendelea kuonekana ni chama dola kwa sababu ndiyo inayoongoza dola, na nafasi ya vyama vya upinzani kuonekana vipo vipo tuu kwa vile vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria!.

Kufuatia hali hii ya "CCM Supremacy" kunapelekea viongozi wa mihimili mikuu ya nchi, Bunge, Mahakama na Serikali, kutimiza wajibu wake kwa mlengo wa heshima kwa CCM kwa sababu M/Kiti wa chama tawala ndie head of Executive, ambaye ndiye rais wa nchi anaeteua kila mtu!.

Huku kujikomba komba kwa CCM, kumepelekea hata Spika na Naibu Spika ambao walipaswa kutimiza majukumu yao independently, wanajikuta wakiifavour CCM, kwa lengo la kujikomba komba huku wakiliangamiza taifa bila wao kujijua kwa kisingizio kuwa kwa vile CCM ndio chama tawala!.

Kwa mujibu wa uendeshaji wa mabunge ya vyama vingi, Mkuu wa shughuli za serikali bungeni, ambaye ni Waziri Mkuu, na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, KUB, ambaye ni Mhe. Freeman Mbowe, wana hadhi sawa kabisa ndani ya bunge!. Hakuna mmoja ambaye ni mkubwa zaidi ya mwingine wala hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake!. Wako sawa sawa kabisa!.

Vivyo hivyo, hadhi za mawaziri na mawaziri vivuli ndani ya bunge ni sawa kabisa, tofauti pekee ni mawaziri wana means zaidi kutokana na uwezeshaji kiliko hawa vivuli!. Mfano Waziri Magufuli, akishakagua barabara au kuizindua, waziri kivuli alipaswa aifanyie ukaguzi na kutoa mawazo yake kama ni chini ya kiwango etc, etc.

Haki zote za Waziri Mkuu bungeni ndizo pia haki za KUB!.

Japo haijaandikwa kwenye kanuni yoyote kuwa Waziri Mkuu akisimama, "ni lazima spika ampe ruhusa ya kusikilizwa" no matter what!. Spika hana mamlaka yoyote ya kuamua kutomsikiliza Waziri Mkuu anaposimama kwa hoja yoyote!. Vivyo hivyo, spika au naibu spika, "hana mamlaka!" ya kumzuia KUB kuzungumza!.

Naomba wale wenye mapenzi mema na nchi hii, hebu tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, hivi kweli pale bungeni jana, angesimama Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, hivi kweli Naibu Spika angemwambia "Kaa Chini?!". Angeendelea kusimama hivi Naibu Spika angewaamuru askari wa bunge kumtoa nje?!.

Hadhi ya KUB ni sawa kabisa na Waziri Mkuu, kitendo cha Naibu Spika kumzuia KUB asizungumze, kumuamuru akae chini na kisha kuamuru atolewe nje, "that was provocation kwa wapinzani wote wa kweli!", kiliwatia hasira, na kilichofuata ni actions in provocation!. Chanzo ni ukosefu wa busara ndogo tuu wa Naibu Spika!.

Laiti Mhe. Naibu Spika, angelimruhusu KUB kuzungumza na kuisikiliza hoja yake!, naamini 100% kwa 100%, yote yaliyofuatia yasingetokea!.

Bungu letu lina mapungufu makubwa na ya msingi ya kikanuni za uendeshaji mabunge ya vyama vingi!. Kiukweli kila kunapotokea vurugu bungeni, mimi huwa namkumbuka sana Mhe. Samuel Sitta!.

Kiukweli huko nyuma nimewahi kulalamikia sana uendeshaji wa bunge wa Madam Spika, Mhe. Anna Makinda, lakini sasa sasa nakiri, pamoja na mapungufu yake yote ya kibinaadamu, Mhe. Anna Makinda is better of 100 times than Mhe. Job Ndugai!. This man is a disaster!.

Wabunge tumieni kanuni namba 135-(1) Kutuondolea mtu huyu, japo najua wabunge wa CCM watautumia wingi wao vibaya kutoipitisha hoja hiyo, ile tuu process ya "kukataliwa!" ni funzo tosha!.

Mwaka mmoja uliopita nilitoa angalizo hili, na leo nalitoa tena! Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Wasalaam.

Paskali
 
Sikubaliani na mleta mada kwenye hili la kumuita NS dikteta. Kama kweli hoja yako ina mashiko, hilo la kuhusu udikteta, basi malalamiko yangetolewa na wabunge wapinzani wengi pale bungeni juu ya mwenendo wa bwana Job Ndungai kuhusu namna ambavyo anaendesha bunge. Lakini jambo la kushangaza ni kuona kijikundi kidogo cha wabunge ndicho chenye fujo, ukaidi na kibuli katika kutii kanuni za bunge. Hivyo mleta mada uchambuzi wako kwenye hili ni mwepesi mno kukufanya uhitimishe kuwa Job Ndungai ni dikteta.
 
Mkuu Pasco hapa ndio alipotelezea huyo janga la Taifa Ndugai.....Laiti Mhe. Naibu Spika,
angelimruhusu KUB
kuzungumza na kuisikiliza
hoja yake!, naamini 100%
kwa 100%, yote
yaliyofuatia yasingetokea!.
 
Last edited by a moderator:

Bunge HALIENDESHWI kwa matakwa ya Mbowe au mbunge mwingine yeyote. Bunge huendeshwa kwa kanuni za bunge na ni wajibu kwa wabunge kutii kanuni hizo.
 
Last edited by a moderator:
vyote kwa pamoja, ni dikteta na inawezekana hazijui kanuni vizuri, anaogopa hoja mtu wa jazba, nilimwona the other day wakati wanahojiwa wakiwa na Lissu, alitia huruma, weredi una mapungufu.
 
Mimi naona Watanzania wote ni janga la taifa. Tupo tupo tu, ilimradi liende. Hata hatujui tunataka nini, tumekuwa tukilalamika sana kama watoto wachanga wanaponyimwa nyonyo na mama zao na kuishia kulia. Tukiamka, JN atajua kuwa hii nchi si ya CCM, CDM, TLP etc, atajua ni ya Watanzania, na Watanzania tunataka nini.
 
Sikubaliani na mleta mada kwenye hili la kumuita NS dikteta. Kama kweli hoja yako ina mashiko, hilo la kuhusu udikteta, basi malalamiko yangetolewa na wabunge wapinzani wengi pale bungeni juu ya mwenendo wa bwana Job Ndungai kuhusu namna ambavyo anaendesha bunge. Lakini jambo la kushangaza ni kuona kijikundi kidogo cha wabunge ndicho chenye fujo, ukaidi na kibuli katika kutii kanuni za bunge. Hivyo mleta mada uchambuzi wako kwenye hili ni mwepesi mno kukufanya uhitimishe kuwa Job Ndungai ni dikteta.
Jibu hoja angesimama waziri mkuu Ndungai Angemwambia kaa chini?au askari wamtoe?
 
Wanabodi,

Mwaka mmoja uliopita niliwahi kuleta hoja hii humu Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Leo nimeikumbuka kufuatia vurugu za jana bungeni!.

Chanzo cha vurugu zile ni "Ukosefu wa Busara Ndogo Tuu toka kwa Naibu Spika!".

Tangu tumepata uhuru, Tanzania imekuwa nchi ya chama kimoja kwa kipindi kirefu, tulipoingia mfumo wa vyama vingi ile 1992, tulifanya marekebisho tuu ya kanuni, ila hatukuweza kufanya mabadiliko ya "mind set" toka mfumo wa chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi, hivyo hali hii imeendelea mpaka sasa kwa CCM ambayo ndio chama tawala, kuendelea kuonekana ni chama dola kwa sababu ndiyo inayoongoza dola, na nafasi ya vyama vya upinzani kuonekana vipo vipo tuu kwa vile vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria!.

Kufuatia hali hii ya "CCM Supremacy" kunapelekea viongozi wa mihimili mikuu ya nchi, Bunge, Mahakama na Serikali, kutimiza wajibu wake kwa mlengo wa heshima kwa CCM kwa sababu M/Kiti wa chama tawala ndie head of Executive, ambaye ndiye rais wa nchi anaeteua kila mtu!.

Huku kujikomba komba kwa CCM, kumepelekea hata Spika na Naibu Spika ambao walipaswa kutimiza majukumu yao independently, wanajikuta wakiifavour CCM, kwa lengo la kujikomba komba huku wakiliangamiza taifa bila wao kujijua kwa kisingizio kuwa kwa vile CCM ndio chama tawala!.

Kwa mujibu wa uendeshaji wa mabunge ya vyama vingi, Mkuu wa shughuli za serikali bungeni, ambaye ni Waziri Mkuu, na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, KUB, ambaye ni Mhe. Freeman Mbowe, wana hadhi sawa kabisa ndani ya bunge!. Hakuna mmoja ambaye ni mkubwa zaidi ya mwingine wala hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake!. Wako sawa sawa kabisa!.

Vivyo hivyo, hadhi za mawaziri na mawaziri vivuli ndani ya bunge ni sawa kabisa, tofauti pekee ni mawaziri wana means zaidi kutokana na uwezeshaji kiliko hawa vivuli!. Mfano Waziri Magufuli, akishakagua barabara au kuizindua, waziri kivuli alipaswa aifanyie ukaguzi na kutoa mawazo yake kama ni chini ya kiwango etc, etc.

Haki zote za Waziri Mkuu bungeni ndizo pia haki za KUB!.

Japo haijaandikwa kwenye kanuni yoyote kuwa Waziri Mkuu akisimama, "ni lazima spika ampe ruhusa ya kusikilizwa" no matter what!. Spika hana mamlaka yoyote ya kuamua kutomsikiliza Waziri Mkuu anaposimama kwa hoja yoyote!. Vivyo hivyo, spika au naibu spika, "hana mamlaka!" ya kumzuia KUB kuzungumza!.

Naomba wale wenye mapenzi mema na nchi hii, hebu tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, hivi kweli pale bungeni jana, angesimama Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, hivi kweli Naibu Spika angemwambia "Kaa Chini?!". Angeendelea kusimama hivi Naibu Spika angewaamuru askari wa bunge kumtoa nje?!.

Hadhi ya KUB ni sawa kabisa na Waziri Mkuu, kitendo cha Naibu Spika kumzuia KUB asizungumze, kumuamuru akae chini na kisha kuamuru atolewe nje, "that was provocation kwa wapinzani wote wa kweli!", kiliwatia hasira, na kilichofuata ni actions in provocation!. Chanzo ni ukosefu wa busara ndogo tuu wa Naibu Spika!.

Laiti Mhe. Naibu Spika, angelimruhusu KUB kuzungumza na kuisikiliza hoja yake!, naamini 100% kwa 100%, yote yaliyofuatia yasingetokea!.

Bungu letu lina mapungufu makubwa na ya msingi ya kikanuni za uendeshaji mabunge ya vyama vingi!. Kiukweli kila kunapotokea vurugu bungeni, mimi huwa namkumbuka sana Mhe. Samuel Sitta!.

Kiukweli huko nyuma nimewahi kulalamikia sana uendeshaji wa bunge wa Madam Spika, Mhe. Anna Makinda, lakini sasa sasa nakiri, pamoja na mapungufu yake yote ya kibinaadamu, Mhe. Anna Makinda is better of 100 times than Mhe. Job Ndugai!. This man is a disaster!.

Wabunge tumieni kanuni namba 135-(1) Kutuondolea mtu huyu, japo najua wabunge wa CCM watautumia wingi wao vibaya kutoipitisha hoja hiyo, ile tuu process ya "kukataliwa!" ni funzo tosha!.

Mwaka mmoja uliopita nilitoa angalizo hili, na leo nalitoa tena! Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Wasalaam.

Pasco.

Mhh! Hii ni taabu ya viongozi wa kiafrica,they don't think outside the box! Ndugai na wana ccm wenzake wanaamini wataiongoza Tanzania mpaka mwisho wa duni!! Never on earth! The guy i.e Ndugai, is too pompassy! Anafikiri atakuwa spika miaka yote! Amuulize Samweli Sitta Pamoja na kujenga ofisi ya bunge kwenye jimbo lake bado alipigwa chini!!
 
Chadema wanawalea sana hawa CCM na spika wao, Ilipaswa jana zipigwe ngumi kweli kweli ili kama mbaya iwe mbaya kweli.Watakuwa wanawaitia Polisi kihuni kila siku huku nyie mnaishia kulalamika tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!

Haiwezekani Hoja kujibiwa kwa kutumia polisi, bunge lina kinga zake na Polisi hawaruhusiwi kuingia bila kuwepo kwa uhalifu!

Chadema acheni kulalamika chukueni hatua ngumu maana sasa kinachowatokea ni fedheha sana!!! Hiyo jana mngewatandika hata hao askari wanaotii amri za kishenzi!!

Chadema acheni busara mbuzi huku mnadhalilishwa!!!
 
Angepoteza nini kwa kumruhusu KUB? Yangetokea kwa Pinda ingekuwaje? ****** is purely haunted by evil spirits.
 
Sikubaliani na mleta mada kwenye hili la kumuita NS dikteta. Kama kweli hoja yako ina mashiko, hilo la kuhusu udikteta, basi malalamiko yangetolewa na wabunge wapinzani wengi pale bungeni juu ya mwenendo wa bwana Job Ndungai kuhusu namna ambavyo anaendesha bunge. Lakini jambo la kushangaza ni kuona kijikundi kidogo cha wabunge ndicho chenye fujo, ukaidi na kibuli katika kutii kanuni za bunge. Hivyo mleta mada uchambuzi wako kwenye hili ni mwepesi mno kukufanya uhitimishe kuwa Job Ndungai ni dikteta.
na kwa kuwa kwa uchache wao ndiyo maana wanawanyanyasa , sasa subirini mbele ya safari hata CDM wakikosa uraisi watakuwa na wabunge wengi mno na ndiyo mtakapo taka suluhu ambayo mliikataa. watanzania waliowengi wanalaani vitendo hivyo vinavyofanyika bungeni , lakini wanaimani kuwa hawa CDM hawana dola ndiyo maana wananyanyaswa. ndiyo muono wa watanzania walio wengi tofauti kabisa na viongozi wanavyoona kuwa hawa wapinzani ni wakorofi tu na wataadhibiwa na wananchi kwa tabia zao, uliza watu mbali mbali na wa mikoa mbali ,hiyo ndiyo picha iliyopo
 
Wanabodi,

Mwaka mmoja uliopita niliwahi kuleta hoja hii humu Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Leo nimeikumbuka kufuatia vurugu za jana bungeni!.

Chanzo cha vurugu zile ni "Ukosefu wa Busara Ndogo Tuu toka kwa Naibu Spika!".

Tangu tumepata uhuru, Tanzania imekuwa nchi ya chama kimoja kwa kipindi kirefu, tulipoingia mfumo wa vyama vingi ile 1992, tulifanya marekebisho tuu ya kanuni, ila hatukuweza kufanya mabadiliko ya "mind set" toka mfumo wa chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi, hivyo hali hii imeendelea mpaka sasa kwa CCM ambayo ndio chama tawala, kuendelea kuonekana ni chama dola kwa sababu ndiyo inayoongoza dola, na nafasi ya vyama vya upinzani kuonekana vipo vipo tuu kwa vile vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria!.

Kufuatia hali hii ya "CCM Supremacy" kunapelekea viongozi wa mihimili mikuu ya nchi, Bunge, Mahakama na Serikali, kutimiza wajibu wake kwa mlengo wa heshima kwa CCM kwa sababu M/Kiti wa chama tawala ndie head of Executive, ambaye ndiye rais wa nchi anaeteua kila mtu!.

Huku kujikomba komba kwa CCM, kumepelekea hata Spika na Naibu Spika ambao walipaswa kutimiza majukumu yao independently, wanajikuta wakiifavour CCM, kwa lengo la kujikomba komba huku wakiliangamiza taifa bila wao kujijua kwa kisingizio kuwa kwa vile CCM ndio chama tawala!.

Kwa mujibu wa uendeshaji wa mabunge ya vyama vingi, Mkuu wa shughuli za serikali bungeni, ambaye ni Waziri Mkuu, na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, KUB, ambaye ni Mhe. Freeman Mbowe, wana hadhi sawa kabisa ndani ya bunge!. Hakuna mmoja ambaye ni mkubwa zaidi ya mwingine wala hakuna aliyebora zaidi ya mwenzake!. Wako sawa sawa kabisa!.

Vivyo hivyo, hadhi za mawaziri na mawaziri vivuli ndani ya bunge ni sawa kabisa, tofauti pekee ni mawaziri wana means zaidi kutokana na uwezeshaji kiliko hawa vivuli!. Mfano Waziri Magufuli, akishakagua barabara au kuizindua, waziri kivuli alipaswa aifanyie ukaguzi na kutoa mawazo yake kama ni chini ya kiwango etc, etc.

Haki zote za Waziri Mkuu bungeni ndizo pia haki za KUB!.

Japo haijaandikwa kwenye kanuni yoyote kuwa Waziri Mkuu akisimama, "ni lazima spika ampe ruhusa ya kusikilizwa" no matter what!. Spika hana mamlaka yoyote ya kuamua kutomsikiliza Waziri Mkuu anaposimama kwa hoja yoyote!. Vivyo hivyo, spika au naibu spika, "hana mamlaka!" ya kumzuia KUB kuzungumza!.

Naomba wale wenye mapenzi mema na nchi hii, hebu tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, hivi kweli pale bungeni jana, angesimama Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, hivi kweli Naibu Spika angemwambia "Kaa Chini?!". Angeendelea kusimama hivi Naibu Spika angewaamuru askari wa bunge kumtoa nje?!.

Hadhi ya KUB ni sawa kabisa na Waziri Mkuu, kitendo cha Naibu Spika kumzuia KUB asizungumze, kumuamuru akae chini na kisha kuamuru atolewe nje, "that was provocation kwa wapinzani wote wa kweli!", kiliwatia hasira, na kilichofuata ni actions in provocation!. Chanzo ni ukosefu wa busara ndogo tuu wa Naibu Spika!.

Laiti Mhe. Naibu Spika, angelimruhusu KUB kuzungumza na kuisikiliza hoja yake!, naamini 100% kwa 100%, yote yaliyofuatia yasingetokea!.

Bungu letu lina mapungufu makubwa na ya msingi ya kikanuni za uendeshaji mabunge ya vyama vingi!. Kiukweli kila kunapotokea vurugu bungeni, mimi huwa namkumbuka sana Mhe. Samuel Sitta!.

Kiukweli huko nyuma nimewahi kulalamikia sana uendeshaji wa bunge wa Madam Spika, Mhe. Anna Makinda, lakini sasa sasa nakiri, pamoja na mapungufu yake yote ya kibinaadamu, Mhe. Anna Makinda is better of 100 times than Mhe. Job Ndugai!. This man is a disaster!.

Wabunge tumieni kanuni namba 135-(1) Kutuondolea mtu huyu, japo najua wabunge wa CCM watautumia wingi wao vibaya kutoipitisha hoja hiyo, ile tuu process ya "kukataliwa!" ni funzo tosha!.

Mwaka mmoja uliopita nilitoa angalizo hili, na leo nalitoa tena! Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!

Wasalaam.

Pasco.

Hili limeeleweka.
 
Ndugai alipania kumtoa Mbowe nje kwani the previous day alishaonya kuwa bila shaka wabunge wa upinzani wanamfahamu. Alimaanisha nini? Wanamfahamu alivyo mbabe na asivyozingatia kanuni siyo? Kamati ya maadili imwulize alichomaanisha. Ndugai anashindwa kusimamia kanuni kutokana na ubabe na ushabiki wa chama chake.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mbona Lukuvi huwa anapewa fursa mara kwa mara bila ya utaratibu? Ingekuwa busara tu kumsihi Mbowe amsubiri Mrema then atamruhusu kuongea kuliko kumwambia kaa chini kwa dharau!!!
 
With a light touch - makosa ni kumwalika bondia Francis Cheka Bungeni maana aliwahamasisha kupigana ngumi! hata hivyo nakuunga mkono kabisa kuwa mabadiliko ya mfumo kuingia vyama vingi hayajabadilisha 'mind-set' ya watu wengi na hasa walioko kwenye Chama tawala kwani bado wnatembea na Party Supremacy. Naibu Spika anashangili na kujisifu kutoa amri inayozua vurugu bungeni na kuona kwake kashinda! Ni ajabu! Lakini ukiangalia matukio yenyewe ni dhairi pande zote zilikuwa zimeandaa yaliyotokea. Upinzani walidhamiria kusimamisha mjadala na watawala (kwa kutumia naibu Spika) walikuwa tayari kwa kuwatoa nje, na askari waliandaliwa kabisa kwa shughuli hiyo.
 
Back
Top Bottom