Vurugu za Bungeni: Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Pasco,

Si sahihi kusema kuwa Tundu Lissu ni 'mtundu'. Hata kwa maelezo uliyotoa ni wazi Lissu havumilii kabisa ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu. Mtindo wa kufanya mambo kwa maujanja-ujanja ni mwiko kwa huyu bwana.
 
Last edited by a moderator:
Mama Spika anatakiwa kutafuta mbinu tofauti na ambazo zimekwishatumika tangu akiwa mtoto kumthibiti bila mafanikio. Akitumia kanuni za kibunge kumthibiti atamuweza kwani ni mwanasheria mwenye kipaji na akili sana wanaomjua wamewahi kumuona akijenga hoja mahakamani ni TUNDU aliyeongoza kwa mabishano ya kisheria. kafanya kazi pale Mahakama Kuu kwa muda mrefu.
Kesi ya Lema alivyoingia Lisu kila mtu anajuwa ni nini kilichofuatia.
 
Wenye akili nyingi darasani wakilivuta wanakuwa ni walipukaji sana. Kwa trend ilivyo Bungeni sasa, wavutaji ni wengi.
hahahahahahahahahaaha!
mkuu tukubaliane kuwa KITI kinalipukaji kama ilivyo kwa tundu lissu kama unavyotaka iwe,
lakini ulipukaji wa Lissu una maslahi kwa taifa na ule ulipukaji wa kiti una maslahi ya watu wachache....
 
KATUNI(715).jpg
 
Truth be told...you can't silence a strong man like him by that approach...lets wait and see
 
Tundu Lisu ana hoja nzuri, weakness yake kubwa ni communication skills and wisdom....
 
Lissu,Mnyika,Mdee,Msigwa kidogo Mbatia na Kafulila ni baadhi ya wabunge wanao wanyima ma-speaker raha sana yaani wakisimama tu, Jasho lishawatoka ma-speaker.
 
Mh. Tundu Lisu ananikumbusha mbali! Mwaka 1961 tukiingia Form 1, haikuchukua muda darasa letu, pamoja na kuwa vinyoya, likajulikana kama "siasa kali" (wakati huo hatujapata uhuru). Bahati mbaya wengi wa vipanga darasani walilazimika kuchukua masomo ya sayansi kwani huo uhuru wa kuchagua haukuwapo sana. Nina hakika mtu kama Tundu Lisu, angesoma wakati huo, labda siasa angeisikia tu kwa mbali...sana sana angeishia kuwa Injinia au dakitari! Linalosikitisha ni kuwa wengi wa viongozi wa baadaye kutoka kundi letu (Wabunge na Mawaziri) ni wale ambao somo la "additional & applied mathematics" walikaa nao mbali kama ukoma. Kweli mambo yalikuja kubadilika!
duuuh 1961 upo sec? khaa mimi ni wa sita kwetu hata wa kwanza alikuwa hajazaliwa ,wala wazazi wetu walikuwa hawajuani,na tumepishana miaka minne minne. duuuh kweli jf ni pana.sitanii tena mtu huku. naahidi kuwa na adabu.shikamoo mzee
 
Bunge letu limekosa viongozi..wote spika na naibu wake wanapwaya vibaya..!
 
Mh. Tundu Lisu ananikumbusha mbali! Mwaka 1961 tukiingia Form 1, haikuchukua muda darasa letu, pamoja na kuwa vinyoya, likajulikana kama "siasa kali" (wakati huo hatujapata uhuru). Bahati mbaya wengi wa vipanga darasani walilazimika kuchukua masomo ya sayansi kwani huo uhuru wa kuchagua haukuwapo sana. Nina hakika mtu kama Tundu Lisu, angesoma wakati huo, labda siasa angeisikia tu kwa mbali...sana sana angeishia kuwa Injinia au dakitari! Linalosikitisha ni kuwa wengi wa viongozi wa baadaye kutoka kundi letu (Wabunge na Mawaziri) ni wale ambao somo la "additional & applied mathematics" walikaa nao mbali kama ukoma. Kweli mambo yalikuja kubadilika!

thikamooo,,,,,,,,
 
Umenifurahisha sn yani madame spika ni spika wa majaribio ya usawa wa kijinsia, bas tujiandae kupata narais wa majaribio ya kijinsia aliyeshindwa kaz un
 
mkuu,
huoni kama maelezo yako yanajichanganya............kwanza unamsifia mh.sitta, halafu hapo hapo unasema alikuwa anayumbishwa na dr. Slaa, tena huoni soni, kama mh. Sitta alikuwa anayumbishwa na mtu mmoja, kwa nini usione kama kulikuwa na tatizo kuliko la mh. Makinda kuyumbishwa na watu wengi wasomi walioingia bungeni ........sasa sijui nielewe lipi............jaribu kujenga hoja inayoeleweka.


By the way, wewe ni kabila gani?.

alikuwa analiyumbisha bunge kwa facts ambazo sitta alikuwa mara nyingi analazimika kuzikubali,huyu bibi ni mbabe hakubali facts za wapinzani..usichoelewa wewe nini hapo!!
Unataka kujua kabila kwani unataka kutambika?
 
Du yote ni NENO,let me cross my fingers
God Bless Tanzania,God bless the Tanzanians
 
Halafu bangi ilivutwa sana Ilboru miaka hiyo.
Mkuu WC, O-level nilisoma Tambaza, jamaa walikuwa wanapiga sana hiyo kitu kule juu kunaitwa summit, wengi waliibuka na misonge ya nguvu!, hivyo nilipokwenda Ilboru, nilijaribu, ili na mimi nipasue, purely on academic acellence!, very unfortunately mimi ilinituma vibaya!. Nilipowaeleza wenzangu, wakasema kosa ni langu, mimi ndio niliwaza hayo mabaya!, wakaniambia kabla ya kupuliza, dhamiria kwanza kupiga biku usiku kucha!, nikadhamiria, na kujaribu tena!, vile vile inantuma kusaka huduma fulani na ukikosa unaweza kubaka!.

Tangu pale sikujaribu tena kuitumia kusemea!, nilifikia stage hata nikipita mahali nikasikia tuu harufu!, jamaa huyo!.

Kiukweli nawajua baadhi ya watu ambao wameitumia for good use and it has worked well for them!, O-level wametoka na point 7!, A-level point 3!, sijui kama mpaka chuo waliendelea ila sasa wako ik kabisa in life!.

Kuna kitabu kuhusu narcotics nilikisoma siku za nyuma, nikakuta kati ya madawa yote ya kulevya, jani ndilo lenye kilevi kidogo kabisa na addtiction yake haina withdrawer symptoms!.

Hata sigara za kawaida zina sumu ya nicotine wakati jani halina sumu!.
Kahawa ya kawaida ina sumu ya caffeine ambayo ni verry addictive, jani halina!.
Mimi ni supporter mkubwa wa ku legalize hii kitu but only kwa wale ambao wamekuwa proved kuwa itawatuma vizuri!.
Pia mimi ni supporter wa "pro choice" katika life na pia naunga mkono ile "the oldest professional" iwe legalized!.

Pasco.
 
Mi ningependa kuuliza, adhabu yoyote itakayotolewa kwa Tundu je itakuwa fair na ni hatua gani mh. huyu anaweza kuzichukua? Ukizingatia Bi Kiroboto alishasema mapema kuwa yeye ndiye kinara japo hakuwepo bungeni pengine hakupata muda wa kufuatilia kiundani jambo hilo, kwangu mimi ni kama the judgement has made even before the trial! japo sina shaka naye anafahamu kanuni za kibunge,
 
Wanabodi,

Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kwa kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya utulivu, amani na usalama wa bungeni, bali pia kumepelekea Spika kufuta baadhi ya ratiba za bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye order paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi.

Jana kika cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali hiyo na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali ya papo kwa papo na maswali na majibu! ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.

Swali la kwanza la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanza cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi?, kama anavyoelezwa na Madam Speaker?, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali uzingatiaji wa kanuni za Bunge, kufuatia Mhe. Spika, kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?.

Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu Mhe. Tundu, Tangu akiwa Shuleni, naomba kuchukua fursa hii kumfariji Mhe. Spika, kwa kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mheshimiwa Tundu Lissu kuhusu kanuni za bunge, wala wasipoteze muda kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa na udhaifu unajulikana tangu chanzo chake, ulipo na labda utaendelea kuwepo, hata akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.

Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa kuwa lile jina lake la Tundu, sio jina tuu, huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kweli pale kanuni zinapopindishwa ili kutoa mteremko kwa upande fulani!.

Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule moja kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za Mkuu mmoja aitwae Bino!. Huyu Bino alikuwa ni mwalimu mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu, alinyanyua mikono juu na kwisha kuishusha juu baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.

Tundu Lissu alijiunga shule ya vipanga ya Ilboru akitokea Galanos, wakati huo akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na duka la kwa "Akwii".

Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma saa ngapi, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya!. Moja ya maeneo ambayo jamaa alikuwa ni ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Jamaa akishakuwa na uhakika yuko on the right track, ni mbishi hakuna mfano!. Hata nami nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya Chapa Ng'ombe, unapokutana na vibinti vya Vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukijumlisha na lilke baridi la kule, tena wakati huo, "bwawa halijaingia luba!'...

Tundu lissu kama livyoingia Ilboru, vivyo hivyo ndivyo alivyoondoka na wani kali, akaenda UDSM na sisi vilaza wengine tuykaishia vile vyuo vya mashenzini!. Tulipoteana kwa kipindi cha miaka 10!, tulikuja kukutana tena mjini Atlanta, yeye akiwa na yeke nami na yangu, ndipo akanieleza yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsubu bila huruma!.

Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
  1. Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndio anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
  2. Au ni Spika ndiye dhaifu hadi kushindwa kumdhibiti Tundu Lissu na utundu wake?.
  3. Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni, zikikiukwa, na kupindishwa?, hivyo kumpatia fursa Mhe. Spika kujiendeshea bunge anavyotaka, ili kudumisha utii, na nidhamu, bunge liwe la amani?.
  4. Hivyo Mhe Spika kuwathibitishia Watanzania kuwa hata yeye ambaye ni Spika wa majaribio ya "jinsia" "ameweza" kuliendesha bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo jee, 2015, tukamilishe majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia?, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia?.

Wasalaam

Pasco.
(Skulu Meti wa Toto T).
Hivi ukiwa unatetea haki yako au ya wapiga kura wako ndiyo kuitwa Mtundu? Hapa ndiyo naanza kuona ule usemi usemao ukitaka ubaya dai Chako.
Mara ya kwana kumuona Tundu kabla yakuwa mbunge nilitamani siku aje kuwa mbunge na niliomba sana hilo na imekuja kuwa hivyo .Bravo Mh Tundu





Hivi kwa Tanzania yetu
 
mkuu, Tundu kasoma A'level Galanos. Ilboru kasoma O'level. Sasa alihama kutoka Galanos kwenda Ilboru kivp?. Tuliosoma pale Galanos japo hatukumkuta ila rekodi zinaonesha amesoma HGE pale. Naona umechapia kidogo mkuu.
Mkuu Don-Oba, thanks!, mistake regretted!, first post updated!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom