mlikatazwa kwenda baada ya kifo cha ayubu au kabla ya ayubu kufariki poleni it was sad indeedah sio poa, mama sasa alivyokua analia, dogo alikua anaitwa Ayubu, mama aliletwa na defender ya magereza Karanga, gari lipo speed imewasha taa, ametua tuu pale mama ni mayowe, "uuwih mwanangu Ayubu, mbona wenzako waliweza kukimbia, tuseme wewe ndo ulishindwa kukimbia kati ya hawa wote?" hapo tupo Parade tunamsikiliza RPC na mkuu wa wilaya, huku ugeni wa waziri wa elimu ukiwa njiani.
.
.
aisee na ubishi wangu mimi na wa jamaa mmoja hivi kiranja wa ulinzi, tulilia!! yaan tulijiona na hatia, maneno yale yameshindwa kutoka kichwani miaka 12 sasa, hizi ni story tuu, ila ungetazama tukio ungeshangaa, hizi roho madogo wametolea wapi,
.
.
asubuhi watu wamefunga mashati kama kundi la kigaidi la alqaeda, wanasalimiana kwa lugha za Code kama majasusi, saa kumi usiku kibosho na zile kahawa ni giza, tunakutana na kina mama wa kibosho wanatulilia, jamani wanangu rudini, mmezaliwa na wanawake kama sisi, msiende! hakuna anaelewa!!