Vurugu, nyumba zachomwa malipo ya korosho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vurugu, nyumba zachomwa malipo ya korosho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Crashwise, Aug 3, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MKUU wa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, Ponsiano Nyami amesitisha kwa muda malipo ya tatu ya mauzo ya korosho kwa wakulima wilayani humo baada ya kutokea vurugu zilizosababisha kuharibiwa kwa mali na baadhi ya watu kujeruhiwa.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu huyo wa Wilaya alisema malipo hayo ya tatu yalitawaliwa na vurugu katika baadhi ya vijiji na vyama vya msingi vya ushirika wa kilimo na masoko hali iliyotishia usalama wa watu na mali zao.
  Alisema katika vijiji vya Lyenge, Mtandavala, Ntegu, Maundo na Nahyanga, nyumba za baadhi ya viongozi wa vyama hivyo zimechomwa moto na zingine kubombolewa, huku wengine waliofungiwa katika maghala wakituhumiwa kuwapunja malipo hayo.
  Malipo ya tatu ya mauzo ya korosho maarufu kama ‘bonasi’ hutolewa na vyama vya msingi vya ushirika baada ya kupata faida katika biashara ya zao hilo. Malipo hayo hutofautiana kutoka chama kimoja hadi kingine kulingana na bei ya mauzo ya korosho katika soko.
  “Nimeamua kusimamisha kwa muda malipo hadi pale chama husika kitakapohitaji kufanya hivyo kulingana na hali ya makubaliano na usalama katika eneo lao…malipo haya yameiweka katika hali tete ya kiusalama wilaya yangu. Wapo viongozi wa vyama vya msingi ambao wamebomolewa, kuchomewa nyumba zao, wengine wamepigwa” alisema Nyami.
  Aliongeza “Polisi walipambana na wananchi hao na kufanikiwa kuwatia mbaroni 31, kati ya hao 26 wamefikishwa mahakamani…katika mapambano hayo polisi wawili walijeruhiwa. Kwa nia njema malipo yasimame ili kuweka mazingira sawa”.
  Katika taarifa yake kwa Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Abdallah Njovu alishauri vyama vya msingi vya wilaya hiyo kuajiri makatibu waliohitimu kidato cha nne na kupata cheti cha miezi mitatu ya uhasibu ili kurahisisha suala la hesabu.
  “Wengi wa makatibu hawawezi kuandaa hesabu kwa ajili ya kubandika kwenye ofisi zao ili wakulima wajue hali ya biashara ya korosho zao, hali hii imezua hisia kuwa viongozi wa vyama hivyo wanafuja fedha za wakulima,” alisema Njovu.
  Alifafanua “Kukabiliana na tatizo hili nashauri vyama hivyo viajiri makatibu wenye elimu ya kidato cha nne na taaluma kidogo ya uhasibu…hali hiyo itatoa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili.”
  Baraza hilo liliafiki ushauri huo na kuomba utekelezaji wake uanze mara moja ili kutoa tiba ya vurugu zinazojitokeza katika vyama vya msingi ambazo huchagizwa na kukosekana kwa hesabu sahihi ya biashara ya korosho. Hii ni mara ya pili kwa Wilaya ya Tandahimba kukumbwa na vurugu zinazohusu masuala ya Korosho.
  Aprili mwaka huu, wakulima wa korosho walifunga shule, kuvamia kituo cha Polisi na kuwapiga askari wakishinikiza Serikali iwalipe malipo ya pili ya mauzo ya mazao yao.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  pole zao maana miongozi ya kibongo inaboa kama nini..
   
 3. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,224
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 280
  Mmh!Haya kaka tunaomba uendelee kutupa updates!!
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Mnonge Mnyongeni lakini Haki yake Mpeni...Korosho zake Uzichukue umuahidi Pesa then unamzungusha! Ndio matokeo yake haya.. na Huu Mpango wa Kila Siku swala lipo mahakamani lisizungumziwe kuna Siku litawahs aMoto usiozimika....

  Watoeni Ndani hao mliowakamata na muwatie Ndani waliochelewesha Pesa za Watu kwani ndio Waliosababisha Matukio ya Wadai Haki...

  Hapa Nchini Machafuko yakizidi na kuwa Mabaya atakayetizamwa ni Raisi
   
Loading...