Hapa ndo nachokaga siku hizi JF. Mshana j kaweka hoja yenye mashiko inayotakiwa kujadiliwa kwa ueledi. Siamini kuwa hoja hii kaweka kwa msingi wa kiitikadi. Sasa hoja ya mafisiem inatoka wapi? Badilika mkuu.mshana jr , mkuu kama haya yote yametoka kichwani mwako basi wewe ni bora mara 100 ya yule nanilinhii mkurupukaji....
Subir uone povu la mafisiem sasa......
Zaidi ya hilo nchi yetu ina tatizo kubwa sana la vipaumbeleAjabu ni kwamba wewe ambaye haumo hata kwenye serikali umemuelewa Mkuu kuliko hata hao waliopo serikalini,maana ulivyoelewa wewe ndivyo nilivyoelewa mimi,huwa najiuliza siku zote hivi hawa watu utendaji wao wa kazi huwa unaongozwa na nini hasa?unafiki wao? uoga wao?au sera na utaratibu maana sikuona hata sababu ya wao kukurupuka kule ikiwa umemuelewa mkuu wako wa kazi kasema nini,suala ni kuelewa umeambiwa nini na kisha nini kifuate basi,lakini hawa wenzetu unafiki ni mwingi kuliko uhalisia.
Yale yaleeee... MshaanzaHapa ndo nachokaga siku hizi JF. Mshana j kaweka hoja yenye mashiko inayotakiwa kujadiliwa kwa ueledi. Siamini kuwa hoja hii kaweka kwa msingi wa kiitikadi. Sasa hoja ya mafisiem inatoka wapi? Badilika mkuu.
Hahaha. Sawa mkuu. Najua Mshana ni anti ccm lakini hoja zake nazizoma kwa kuangalia content na sio political affiliation yale. Lakini kama kila issues wewe unahusianisha na siasa basi hakuna namna mkuu.Yale yaleeee... Mshaanza
Yale yale naomba nipingane nawe kwa suala la vita..unajua tunaishi kwenye ulimwengu tofauti kabisa leo...yani mtu anakutandika toka mbali huku akitafuna paja la kuku tech ya sasa iko vizuri tuwekeze hukoMkuu Mshana nimekubaliana na wewe kwa kiasi lakini kiasi pia natofautiana na wewe.
1. Kiusalama ikitokea vita (Mungu aepushie mbali) kutekwa kwa mji mkuu ni ishara kuwa nchi/Serikali imeangushwa. Dodoma bado inakuwa sehemu nzuri ikitokea cha kutokea. UUwepo wa Dar kama mji mkuu yenye serikali kandokando ya bahari (maji) ni tatizo.
2. Hoja ya kupanua Dar es Salaam ili mji upumuo haina mashiko. Kinachokosekana mji huu ni mipangomiji, serikali kutokuwekeza kwenye makazi na hulka ya kila mtu kuwa na kiwanja chake. Unapopanua mji zaidi unaongeza gharama za uwekezaji kwenye miundombinu. In fact huu mji haukupaswa kuzidi 20 Km radius kutoka mjini kati ili maeneo mengine watu waendelee kulima na kupanda miti.
Kwangu, suala la kuhamisha serikali Dodoma ni nzuri nina tatizo na huu uharaka basi.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]mawaziri wa jpm ni kama wacheza show kazi yao kucheza anachoimba bosi wao ,hawajipi muda wa kutafakari wala kumuuliza , mkuu wakati anahutubia hata alikuwa hajamaliza sentesi ya kuhamia dodoma jenista mbio na godoro lake
Usijali mkuu tuvumiliane... Bado nina hasira za majibu ya wanaccm walioniapaga hapo nyumaHahaha. Sawa mkuu. Najua Mshana ni anti ccm lakini hoja zake nazizoma kwa kuangalia content na sio political affiliation yale. Lakini kama kila issues wewe unahusianisha na siasa basi hakuna namna mkuu.
Mkuu punguza ukali wa maneno bana.Mimi pia sikubaliani nae lakini namheshimu kama rais wa nchi japo kura yangu sikumpa cz sijawahi kuamini kama ni mtu sahihi kwa hi nchi...Mifano yako mikali sana mkuuMkuu nimekuelewa mzee.
Tatizo la serikali hii wao kazi yao ni kukurupuka na kutoa matamko tu.
Hawajui wala kutaka kupembua mambo kwa kutumia akili.
Akili ya Magufuli ni sawa na mtoto kaona nzi kwenye bakuli la uji. Badala ya kuchukua kijiko na kutoa yule nzi,atampiga nzi kibao na kumwaga uji wote,mwisho wake kumuunguza.
Yetu sisi macho. Anajifanya kucheza ba maisha ya watu na amani. Ubabe yeye,matamko yasio na tija ni yeye. Huyu mtu ana aakili timamu kweli?
Kwanza hukuelewa muktadha mzima wa hii madaMimi nafikiri kabla ya kuanza kutoa lawama na shutuma kwa Rais JPM na safu yake ya uongozi juu ya uamuzi wake wa kuhamisha makao makuu ya nchi na serikali yakutoka jijini Dar hadi mkoani Dodoma ni vizur tukajiuliza haya maswali machache
1. Dhumuni hasa la muasisi wa nchi yetu Mwalimu JK Nyerere kuhamia Dodoma lilikuwa nini hasa?
2. Kwa nini mataifa makubwa duniani hayajaweka makao makuu ya nchi zao kwenye maeneo ambayo ni pembezoni mwa bahari mfano Marekani - washington DC, Uingereza - London, China - Beijing, South Afrika - Pretoria, Majirani zetu kenya nao wameweka Nairobi iliyopo katikati ya nchi na sio Mombasa iliyopo pwani mwa nchi yao?
3. Kiusalama ni vizuri makao makuu ya nchi yakae pwani au yakee katikati mwa nchi?
4. Kuleta maendeleo yenye usawa sawa katika nchi ni je vizur makao makuu ya nchi yabaki Dar au tuamie dodoma?
5. Ili kuweka karibu kuweka huduma za kiserikali karibu na wananchi ni vizur makao makuu ya nchi yaendelee kuwa dar au tuamie dodoma?
Mwenye majibu mujarabu wa haya maswali ndio anaweza kuendelea kukosoa uamuzi wa serikali kutoka Dar kwenda dodoma.
Note:
Kuna kosa ambalo alifanya mwalimu JK Nyerere la kuruhusu kutumia Dar kama makao makuu ya nchi, kwani ule uamuzi ndio ulipelekea mikoa mingine iendelee kudumaa nchini Tanzania hadi sasa, hivyo watanzania naomba tumuunge Rais JPM kwa dhumuni la kusahihisha makosa yaliyofanywa na mwalimu JK Nyerere, ambapo watangulizi wake kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete walishindwa.
Pili watanzania inabidi tuvumilie maumivu tutakayopata kwa sasa baada ya zoezi la kuhama kutoka Dar kwenda dodoma litakapoanza, kwani badae hali itatengamaa na pia nchi yetu itakuwa katika nafasi nzuri ya kukua strategical.
Jiandae kwenda Dodoma...!!Habari za magazetini leo imethibitika kuwa kuhamia Dodoma si kitu lelemama Si Jenista wala Chizeba wenye dalili ya kusogeza hata kiti
TAMISEMI iko Dodoma tayari lakini pia imekuwa vigumu kuhama sembuse wizara ambazo zina ofisi ndogo tuu
Yangefanyika maandalizi kwasasa Dar ipanuliwe kuelekea Morogoro kuelekea kusini nk
Jiji kwasasa limesongwa linatawikiwa kupanuliwa ili lipumue, tayari kuna miundombinu mingi yenye sura ya makao makuu ya nchi ni swala la kuboreshwa tu kwasasa kuliko kung'ang'ania ndoto isiyotekelezeka na yenye gharama kubwa huku kukiwa hakuna faida za moja kwa moja
Shukrani mkuu asomaye na afahamu.NISICHUKULIWE KAMA MKOSOAJI
Magufuli aliongea vizuri sana kuwa atahakikisha serikali yake inahamia/itahamia Dodoma kabla kipindi chake cha kuwa madarakani kwisha, amebakiza miaka minne na ushee
Baada ya hotuba ile tu ukatokea mlipuko wa matamko ya kuhamia Dodoma na mishemishe zikawa nyingi
-Aliaza Chizeba
-Akafuatia Jenista Mhagama
-Mambo ya ndani na wengineo
Hawa wote wakasema ni kabla ya mwezi wa tisa
ATHARI ZA MATAMKO HAYA
maandalizi lipulipu yakaanza Dodoma
Wapangaji wa CDA wakafukuzwa
harakati za kutafuta nyumba na viwanja zikawa nyingi
Wazabuni mbalimbali wanaoidai serikali wakafurika kwenye wizara walizofanyia kazi kudai chao
Shughuli nyingi za ki serikali zikavurugika mpaka mkuu wa mkoa wa Dodoma akasitisha matamko yote ya kuhamia Dodoma kwa wiki mbili
MITANDAO YA KIJAMII YANENA
Vumbi la kuhamia Dodoma lilikuwa kila mahali..mitandaoni kukawa na mijadala ya kila aina lakini wengi wakijikita kwenye haya
.uharaka wa kuhamia Dodoma bila maandalizi
.bajeti ya kuhamia huko
.miundombinu mbinu ya Dodoma
.maisha mapya huko nk
Hapa wengi tulitukanwa kuwa tunakurupuka na kukosoa kila kitu. tukawa wavumilivu kwakuwa tuliona wazi kuwa tuko sahihi
MAHITAJI YA NYAKATI
Ishu ya kuhamia Dodoma iliasisiwa na mwalimu Nyerere, aliona Dodoma kama iko katikati ya nchi hivyo kuwa rahisi kufikika kutoka pembe zote za nchi HII NDIO ILIKUWA SABABU PEKEE KUBWA ya kuhamishia makao makuu ya nchi kwenda Dodoma, kama zipo nyingine ni ndogo ndogo
Kwa dunia ya wakati ule mahitaji ya nyakati yalikuwa sahihi kabisa lakini si sasa na hata baadae , ulimwengu umekuwa kijiji, mambo yamerahisishwa mno maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yanaifanya hoja ya kuhamia Dodoma kutokuwa VALID kwasasa, siku hizi hatuhitaji posta wala kusafiri masaa mengi kufuata huduma, siku hizi maendeleo yamesogezwa mikoani wilayani na hata sehemu ambazo mwanzoni hazikufikiriwa kabisa....Nyerere angekuwa hai bado angebatilisha huu uamuzi kwa hakika
BAJETI YA KUHAMIA DODOMA
Wakati wa Mkapa ulifanyika upembuzi yakinifu wa bajeti ya kuhamia Dodoma....ilikadiriwa kuwa zilihitajika kiasi cha shilingi za kitanzania TRILIOM MOJA NA BILIONI MIA MBILI...Ni pesa nyingi kwa nchi maskini kama yetu...Mkapa akashindwa
Leo hii tukitaka kwa hakika kuhamia Dodoma sijui bajeti yake itakuwa shilingi ngapi na hiyo pesa itapatikanaje
Lakini je kuhamia Dodoma kwasasa ndio kipaumbele? Faida zake ni zipi kiuchumi? Sio kwamba tunataka tu kuwatajirisha watu wachache?wengi wakiwa ni raia wa nje...kwakuwa miundombinu mingi watapewa wao kujenga
Je tumeshajitosheleza kwenye huduma zetu muhimu za kijamii? Elimu afya miundombinu nk?
Bandari zetu bado zinahitajika ukarabati mkubwa reli zetu pia nk ...tuwwkeze huku kwanza kunakotuingizia chochote
HITIMISHO
Mkuu wa nchi alisema atahakikisha serikali yake inahamia kabla muhula wake haujaisha na akasema AKIHAMA yeye wengine watafuata
Ina maana watendaji wake hawakumuelewa ama ni nidhamu ya uoga au ni upungufu wa kufikiri?
Hivi rais akisema ataenda Uganda kwa mfano mwezi ujao wewe mtendaji wake ukasema utaenda kabla yake atakuelewaje?
Tujifunze kusikiliza na kutafakari kabla ya kutenda...ishu ya Dodoma itupe somo na kutufumbua macho tusije tukaja kuchukua maamuzi ya kukurupuka yatakayoligharimu Taifa
Mungu ibariki Tanzania