Vipi kuhusu maneno ya Nasor Moyo! Naye ni Nyerere?
Vipi kuhusu usaliti wa Maalimu Seif dhidi ya Jumbe, naye ni Nyerere.
Mtu akisema ukweli huyo si MZNZ kama ulivyomkana Mzee Moyo, eti hajawahi kuwa waziri kiongozi au Rais.
Jusa hakuwepo wakati wa Mapinduzi na wala hana uchungu wa ZNZ kwasababu ni Mwarabu, tumwamini huyo.
Leo mumefika mahali mnakana maneno ya Nasor Moyo, mumeshamaliza kumkana Ahmed, mnajua mnachokitaka ninyi WZNZ ? Mimi nadhani tatizo si muungano, tatizo ni kubwa sana hasa katika weledi, nbajeti ya elimu iangaliwe.
Jibuni hoja za Vuai siyo kumshambulia kwa matusi, WZNZ mbona tunasikia ustaarabu kitovu chake ni ZNZ, lakini haionekani kama ni hivyo! Acheni matusi shambulieni hoja.
Nakusaport kaka watu waache jazba. Lakini vijana wanatoa hoja ingawaje na jazba zimo ndani yake kutokana na kuchoshwa na propaganda za wahafidhina wa CCM.
Mimi naamini kwamba CCM inajua wazanzibar wa kawaida walio wengi, be it CCM, CUF, wasio na vyama na wa vyama vingine hawataki muungano. Kwanini nasema hivi: kama CCM ina confidence kwamba walio wengi wanautaka muungano, basi wangelikuwa wa kwanza kuasisi kura ya maoni ili kuwaadhiri wanaoupinga!. However, ukitaka kujua kwamba wanajua hilo fika, hata Kikwete alizuia hoja ya muungano kujadiliwa katika utafutaji wa maoni ya katiba mpya. Jiulize alikuwa akiogopa nini na katiba ni mali ya wananchi?
Kwa hiyo Vuai mwenyewe hakutoa hoja, analalamika tu. Angekuwa na hoja, angevunja hoja za wanaotaka muungano ufanyiwe marekebisho, sio kutisha watu wazima!