Vuai anena kuhusu Muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vuai anena kuhusu Muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagwell, Sep 29, 2012.

 1. b

  bagwell Senior Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Mapinduzi Zanzibar, kimesema ikiwa itatokea kuvunjika kwa Muungano wa Serikali mbili kutokana na shinikizo la baadhi ya wanasiasa ‘mapepe’ kutaibuka vuguvugu la kujitenga kwa visiwa vya Unguja na Pemba .

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alitoa matamshi hayo katika mahojiano na NIPASHE yaliofanyika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa jana.

  Vuai alisema tukio lolote litakalotoa mwanya wa kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar linaweza pia kusababisha visiwa vya Pemba na Unguja kujigawa na kuwa mbalimbali.

  Alisema hakuna mwanasiasa au kiongozi wa aina yeyote atakayemudu kulizuia wimbi hilo lisitokee huku akieleza kuwa nje ya Muungano anaamini visiwa vya Pemba na Unguja ‘ima faima’ havitabaki pamoja kama ilivyo sasa.

  “Wanaoshabikia Muungano uvunjike wasome alama za nyakati,Muungano ikiwa utavunjika leo, kesho au kesho kutwa, Pemba na Unguja si hasha kila upande ukabaki kwake,” alisema.

  Alisema anaamini wapo wanasiasa wanaotumia mwamvuli wa ukabila na ubaguzi ili kuficha madhambi yao kwa kuamua kuwagawa watanzania bara na wazanzibari kwa lengo la kuatamia maslahi yao bila kujali uzito wa umoja wa kitaifa.

  Akikumbusha matamshi ya baadhi ya viongozi yaliowahi kutolewa kuanzia mwaka 1995 na baadae mwaka 2005, alisema tayari wanachama wa CUF waliojiita wazee kutoka Pemba wakiongozwa na Hamadi Ali Mussa na Ali Makame waliwasilisha ombi maalum UN la kutaka Pemba ijitenge.

  “Serikali za CCM zinatambua ubaya na madhara ya jamii kujitenga hivyo jambo hilo lilipuuzwa kwa kukosa mashiko ila naamini nje ya Muungano, Pemba na Unguja ni vigumu kubaki salama,” alisema.

  Alisema wanaotaka kuvunja Muungano wamebeba ajenda tete ya kutetea ulwa na maslahi binafsi kwa kisiingizio cha kuwepo kwa kero za Muungano ambazo alidai CCM inaamini zinarekebishika na kuzungumzika.

  Akizungumzia matamshi yaliotolewa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhusu uchaguzi wa Bububu kuvurugwa na baadhi ya wanasiasa toka CCM, Vuai alisema hakutarajia kusikia maelezo hayo yakitoka kwenye kinywa cha kiongozi huyo.

  Vuai aliwatupia lawama viongozi wa CUF ambao waliojibebesha kazi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uchaguzi huo huku akidai makundi ya wanachama wao waliwazuia wananchi wasijitokeze kutumia haki ya kupiga kura kutokana na kukithiri vitisho.

  Alisema vitendo vilivyofanywa na viongozi wa CUF katika uchaguzi wa jimbo la Bububu Septemba 16 i havikuwa vya kiungwana na kueleza vilikwenda kinyume na misingi ya demokrasia pia maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa.

  Hata hivyo akihutubia wanachama wa CUF katika uwanja Kijichi kwa Geji mwishoni mwa wiki Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, alisema vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Bububu zilisababishwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya SMZ na kumtaka Rais wa Zanzibar kuchukua hatua dhidi ya watu waliohusika.

  Maalim Seif ambaye pia Makamu wa kwanza wa Rais, alisema hatakubali kuona Zanzibar ikirejea katika machafuko na kutaka SMZ iwashughulikie watu wote wanaotaka kurudisha machafuko ya kisiasa visiwani humo.

  Kuhusu Muungano, Maalim Seif alisema kwa mtazamo wake mfumo wa muungano wa mkataba ndiyo unafaa kuzingatiwa wakati huu wa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania.

  Hata hivyo waasisi wa Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Visiwani wameibuka na kupinga hoja ya muungano wa mkataba kwa madai ina ajenda ya siri ya kuvunja Muungano wa Tanzania.  Wewe Vuai ni kama kibaraka tu wewe kumbuka kua ipo siku utajuta kwa kuwasaliti wazanzibari wenzako dhidi ya hao mabwana zako wa upande wa Bara....Mana huo Muungano kuvunjika sio dhambi mana sio lazima kua nao maana haupo katika Qur-an wala Biblia sawa bwana mdogo
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Anatuambia maneno tunayoyafahamu. Kimsingi ana akili za kufanyia mtihani.
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Angekuwepo nyerere wale wote wanaoupinga muungano wangekuwa kaburini sasa! au kigamboni kwenye kizuizi maalum!
   
 4. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,497
  Trophy Points: 280
  Haya anayoyasema bwana Vuai kila mtu nadhani anayajua, hata Mwl. J. K Nyerere aliwahi kutuasa juu ya suala hili, na aliwahi kusema, historia haiwezi kutuacha salama, swali ambalo nimekua nikijiuliza muda mrefu za chochoko za muungano (has hutoka upande wa pili kule, wengi wakiwa ni wafuasi wa KAFU) ni hili, kwanini walioko kwenye system hasa tokea ccm ndo huushabikia sana muungano kuliko wananchi wa kawaida na wanasiasa wasioko kwenye system? Je? is it because wanafaidika kimaslahi au wanategemea siku moja kuwepo kwenye hayo maslahi? nasema hivi kwasababu, siamini hata kama viongozi wa ccm Zanzibar wanaufurahia muungano toka katika mioyo yao, kama wangekuwa wanapenda, how comes wabara waishio Zanzibar eti wanatakiwa kuwa na vitambulisho vinavyo fanana na watu toka nje ya nchi? kwanini ubaguzi huu?
   
 5. b

  bagwell Senior Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanoushabikia Muungano kwa upande wa CCM ni waoga sana wanaogopa mabwana zao wa upande wa bara mbona kuna wengine upande wa CCM hawautaki muungano huu hii inaonesha kua wanaotaka Muungano huu wanapata chochote kitu na wale wasioutaka Muungano huu wana sababu zao binafsi ila kwa upande wangu napenda kusema kwa Muungano huu hauna faida kwa upande wa Zanzibar, mna wazanzibari tunanyimwa kila lenye faida kwa upande wetu ila ipo siku kitanuka tuuu
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280

  Hapo kwenye
  red; hebu tutajie angalau mmoja. Hapo kwenye red-underlined; pia taja angalau mmoja badala ya kuleta mipasho hapa.
   
 7. peri

  peri JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  zambi ya ubaguzi ni mbaya sana na athari yake ni vigumu kuifuta.
   
 8. p

  protox Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una umri gani? umeanza kufatilia siasa kuanzia 2010? nini
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sitaki hata kukisikia hiki kizee. tabu tulizonazo waTz yeye ni sehemu ya tatizo.
   
 10. Kilimo

  Kilimo JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  huu muungano nahata uvunjike, wabara wananufaika na nini?? wabara hawathaminiwi kabisa kule visiwani na hata ktk zoezi la vitambulisho litakalo kuja huko zenji, wabara watajulikana kama wageni sawa na mataifa mengine, sasa kulikoni huu muungano kwa wabara!!! inatosha uvunjike tu!
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wanachokifanya ni kuoingea tu ila ukweli haki ndio itaimarisha muungano wala sio mbinu chafu za kuziba watu kuongelea muungano
   
 12. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ajiulize vuai muungano huu una miaka 50 je zanzibar na wazanzibar wameishi unguja na upemba kwa miaka mingapiii mbona hawaja pigana ccm kwabaguwa wapemba kuwapiga vibaya ndio maana wapemba walitaka kujitenga sababu watanganyika kupitia mwavuli wa vibaraka wao zanzibar waliwatesa sana wapemba
  CHUKUWA mfano mkapa kafanya nini pemba
  wewe kwa nini usiseme hao watanganyika ndio watakao pigana sababu kuna udini ukabila sensa tu ndio hivyo tena necta ndio kunapikwa sasa mfumo kristo waisilamu wameushitukia sasa
  vuai huna njia ya kukimbia mabadilikooo time will tl us:rockon::rockon: zanzibar oyeeee
   
 13. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  1. Mimi nahisi huyu Vuai "mpumbavu", kakopia zile sera za baba yake wa taifa la ‘anatuLLwaahi Nyrere za kusema kua nje ya Muungano hakuna Zanzibar,haya ni maneno ya kijinga ambayo mtu mwenye uchungu na nchi yake hawezi kuyasema, kwanini asijuilize suali moja la kitoto sana, kwamba kabla ya Muungano ilikuepo zanzibar au haikuwepo? na hapo ndipo atapata jibu rasmin.
   Na hata ikiwa mambo yatakua hivyo anavyosema yeye, na ayaache hivyo yatakavyokua lakini kwa sasa tumechoka, na Wazanzibari hatukubali tena kudanganywa.
   Na kama hii haitoshi Unguja na Pemba haziwezi kudai kutengana kwa sababu hakuna siku waliungana mpaka ifikie kudai kutengana, kama hajui hii Unguja na Pemba ni moja.
   Kwa maneno yake, hata kama kuna watu kutoka pemba waliwahi kupeleka maombi UN ili kujitenga hii ni kutokana na madhila yaliokua yakiwapata watu kutoka pemba na hii ilitokana na mfumo ambao uliandaliwa makusudi na viongozi wa chama tawala CCM kwa wakati ule.
   Pia huyu Mpumbavu anadai eti kero za Muungano ni jambo linalozungumzika, sasa mbona kwa miaka zaidi ya 48 hakuna mazungumzo yaliyofanywa ya makusudi na yakazaa faida kwa Zanzibar na Wazanzibari kwa jumla na badala yake tunashuhudia kila siku zikiendelea mbele dhuluma, uonevu mauaji kwa Wazanzibari yanapewa baraka zote na wanaojiita ndugu zetu "Watanganyika".
   Hapa inajidhihirisha wazi ya kwamba viongozi wa CCM Zanzibar, wao ndio wanaotetea ulwa na madaraka yao binafi na kuwakandamiza ndugu zao, na tumekua tukishuhudia kwamba lolote wako tayari kuona linatendeka kusudi tonge zao ziende vinywani mwao, na tumewashuhudia baadhi ya viongozi ambao wanapigania maslahi ya wengi jinsi wanavyobaguliwa na kupigwa zengwe humo ndani ya chama tawala CCM.
   Lakini za mwizi ni arobaini na sasa nahisi zimekaribia InshaAllah kwa uwezo wake Allah hatowapa nguvu wote wenye nia mbaya na Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla.
   Tunakuomba yaa Allah utusaidie……Amiin


   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hivi Muungano bado upo? Kwa jina labda!! Mheshimiwa Karume sijamsikia!!
   
 15. C

  COMRADE CHRIS HANI Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuvunjika kwa muungano wa zanzibar na bara si dhambi na mana sio lazima kua "nao" maana (ati) haupo ktk qur'an wala biblia, basi ni halali pia kuungano wa pemba na unguja kuuvunja manake na wenyewe pia si lazima ati...haupo kwenye qur'an wala biblia..!
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri huyu kijana Hana weledi wowote kuhusu uchumi bali ameshinikwa kisiasa tu kwani ndio Sera ya Chama chake. Na kumbukeni kuwa kiongozi yoyote anaapa kutetea na kulinda katiba ya chama chake. Tumpe pole sana.

  Lakin kwa mtu makini kama alivyokuwa Nyerere alijua fika bila Znz basi uhuru wa tanganyika hakuna kabisa.

  na ndio maana alihakikisha Mzee Aboud jumbe anatolewa madarakani pale alipoanza kuhoji kuhusu Muungano wenu.

  lakin Nyerere hakuishia hapo alisafiri toka Butiama kwenda Dodoma bungeni kwenda kuzima hoja binafsi ya kuanzishwa kwa serikali ya TANGANYIKA.

  Je mnajua kwanini Nyerere alijitahidi kwa gharama zote kuhakikisha Serikali ya Tanganyika haitokei tena Duniani.

  Kwa mwenye akili atagundua kuwa alijua udhaifau wa tanganyika hususan UDINI na KUKOSA UZALENDO bila kusahau UFISADI utaangusha Serikali tya Tanganyika.

  Pole sana
   
 17. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Political propaganda ya CCM kama kawaida, juzi tuliwasikia wakisema same kuhusu chadema, kuwa wataunda nchi yao na kuivunja Tanzania. Ingelikuwa vyema kukawa na ushahidi kwa anayoyasema, tatizo kubwa ni kwa utawala wa juu Tanzania wa upendeleo kwa upande mmoja Zanzibar na kufumbia macho makosa kwa hofu ya kutowauzi waheshimiwa wana mapinduzi. Hilo ndilo kosa kubwa la kuwapo kwa anti union sentiment, siku union gov itapoact kwa uadilifu na haki basi union itakuwa imefikiwa lengo na hutokuta section ya watu kuukataa. Azma ya union haijafikiwa kwa wote, inawafaidisha wachache. Propaganda machine ya CCM conservatives ni sawa ma hadithi za Abunuwasi, tamu kuzisikiliza lakini hazina ukweli.
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Muda mfupi baada ya mpinduzi ya Zanzibar ya 1964, kisiwa na Pemba kilijitenga kikaunda serikali iliyoitwa Peoples Republic of Pemba wakiwa na bendera hii:
   
 19. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eti Wareno wanaidai Zanzibar yaoundé Irudi? Eti waliibiwa na Waarabu wende njaaa
   
 20. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu maneno ya Nasor Moyo! Naye ni Nyerere?
  Vipi kuhusu usaliti wa Maalimu Seif dhidi ya Jumbe, naye ni Nyerere.

  Mtu akisema ukweli huyo si MZNZ kama ulivyomkana Mzee Moyo, eti hajawahi kuwa waziri kiongozi au Rais.
  Jusa hakuwepo wakati wa Mapinduzi na wala hana uchungu wa ZNZ kwasababu ni Mwarabu, tumwamini huyo.

  Leo mumefika mahali mnakana maneno ya Nasor Moyo, mumeshamaliza kumkana Ahmed, mnajua mnachokitaka ninyi WZNZ ? Mimi nadhani tatizo si muungano, tatizo ni kubwa sana hasa katika weledi, nbajeti ya elimu iangaliwe.

  Jibuni hoja za Vuai siyo kumshambulia kwa matusi, WZNZ mbona tunasikia ustaarabu kitovu chake ni ZNZ, lakini haionekani kama ni hivyo! Acheni matusi shambulieni hoja.
   
Loading...