Hapo kwenye red, shida uliyonayo ni kwamba mtu akikupa simu au kitu kingine chochote under the cover of 'promtion' utachukulia hivyo hivyo! Huu ni uvivu wa kufikiri. Unatakiwa kupanua your thinking na kujiuliza the reason behind hicho ulichopewa na uridhike kweli ni promotion and no other interior motives behind.
Sijui umefuatilia kwa kiasi gani mambo ya telecom. Hizo pikipiki, magari, simu wanazotoa hao unaowatetea wao wanahesabu kama sehemu ya kodi! Really, zomba, akili za mbayuwayu ni lazima uchanganye na zako otherwise utaendele kutetea mambo kwa hizi definations za 1st year. Na ndio sababu nilikuuliza 'promotion' inaweza kuwa rushwa, na wewe ukajibu hapana!
Ni wazi huelewi uwepo wa 'fine line' between promotion, lobbying na rushwa and unless ujifunze na uelewe haya mambo utaendelea kutetea mambo kwa hoja za reja reja.
Kuhusu kazi za kamati ya miundo mbinu, kama unaamini sio chochote si lolote, basi niambie ni kwanini Vodacom waende all the way to Dodoma kukutana nao na sio kamati nyingine? Why this committee? Kuna nini special? Promotion? You dont need to be a brain surgen kujua this is beyond promotion.
Hivyo BB ni sawa na Serengeti ?! Yaani: Tsh 1,500/=, sawa na Tsh 1,000,000/= !!?
Tatizo lako ni kuwa upo brainwashed katika biashara ambazo si za kishindani, sasa hivi biashara ni za kishindani wana masoko huwa na mbinu tofauti.
Biashara za sasa si kama za wakati wa Nyerere ambapo kila kitu kilikuwa mali ya umma (monopoly) na hauna choice wala
Kumbuka ukimtuhumu mtu ni wewe unaetakiwa kuleta ushahidi wa wazi kabisa na si uliemtuhumu. Hapa naona huna ushahidi na unajaribu kuwa mpaka matope. Kila unachokisema ni "hypothesis" hauna "solid evidence" kuwa hiyo ni rushwa.
aaaaaaah ! Tuachane na hayo, hebu tuambie voda wana wateja zaidi ya mil 10, pamoja na M pesa transactions, inakuwaje hawa hawako kwenye top 15 ya TRA ???Usitake kuniaminisha kuwa huwa wanagawa Serengeti moja kwa kila "promotion" ya kwenye bar.
aaaaaaah ! Tuachane na hayo, hebu tuambie voda wana wateja zaidi ya mil 10, pamoja na M pesa transactions, inakuwaje hawa hawako kwenye top 15 ya TRA ???
"wanakwepa kodi kihalali kabisaa..............! " sasa nimekuelewa !Kumbuka, kila unavyokuwa mkubwa, msingi unakuwa mkubwa, muda wa kuurudisha msingi unakuwa mkubwa, na hasara zinakuwa kubwa. Lakini hayo ni ya TRA, wao ndio waje waseme wanatoza vipi kodi zao kwa haya mashirika.
Kumbuka katika kodi, kuna tax evasion na kuna tax avoidance kati ya hizo moja ni halali na moja ni haramu. Mashirika makubwa yana wataalaam wa kutumia loopholes za kisheria kupata hilo la halali bila kufanya makosa, inabidi TRA nao wawe na wataalaam na umakini wa hali ya juu katika hilo na pia watu na sheria wajuwe kuzitunga sheria zipasavyo.
Utakuta wengi wa haya makampuni wanatumia upenyo kufanya Tax avoidance kihalali kabisa.
Kuna kitu hakijakaa sawa kwenye haya masuala ya kodi. Hebu pitia hii kutoka Daily News: DailyNews Online Edition - Mobile phone firm to invest 120bn/-. Sijawasikia TRA wakikanusha habari hii! Sasa kama Voda wanasema wamelipa 700bn lakini kwenye ile taarifa ya waziri mkuu kampuni ya kwanza kwa kulipa kodi ilikuwa na around 165bn kwa miaka mitano (Daily News | Top tax-payers list faulted na Questions surround Prime Minister)!"wanakwepa kodi kihalali kabisaa..............! " sasa nimekuelewa !
"wanakwepa kodi kihalali kabisaa..............! " sasa nimekuelewa !
Duh nimepitia hojaa nyingi na zote za wachangiaji naakubaliana naa hoja nyingi,kweli hata me napata BB ya vadacom kila mwaka tena mpyaa sipo selikarini nina biashara zangu tu nafanya lakini nikirudi kwenye mada bwana Ally Komba Vodacom hii wametoa rushwa ukweli nakwambia Directory promotion ipo. Lkn sio kwa kipindi hiki tusidanganyane pengine ww umeweka na hao hao Vodacom humu jamvini uwatete sasa basi rudi kawambie hii ni RUSHWA sawa!leo hii hakuna taasisi wala shirika la fedha linaalofanya Transaction nyingi zaidi ya M-PESA, yanazunguka mabilioni kwa siku uje useme hapa wanaalipa kodi!!!
Hawa jamaa ni noma nawafahamu vizuri sana kwa ujanja ujanja ni wazuri sana hasa wakipata mtu anayehongeka kama hao waliochukua BB pasipokujua!
Hebu kama kuna wataalamu humu wa TRA watudadavulie mwaka jana hawa jamaa walilipa kodi kiasi gani??tukishindwa kupata jibu basi BB zinafanya kazi sehemu nyingi jamani!
Mwisho kbs Vodacom wamewahonga wabunge!!!!!!!!!!