VODACOM wana maanisha nini kwenye hili?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,468
Jamani mimi nina wasiwasi na hawa VODACOM kwenye kadi za kuongeza salio. Kadi yao ya shilingi elfu tano ina expiry date/ muda wa kuisha matumizi. Nilinunua kadi kutoka wa wakala wao katikati ya mwezi wa tatu mwaka huu na kukuta kadi imeandikwa 'tumia kabla/ use before' 03/01/2011; lakini cha ajabu ukiongeza salio inakubali, je haiwezi kuwa credit hizo zitapukutika kama kuku wanapopata kideli au mdondo kwa kutuma sms chache au kupiaga simu chache tu? Kwa nini wanauza voucher zilizokwisha expire au kuisha muda wake? Production ilikuwa kubwa kuliko demand? Au demand imeshuka?

Kwa upande wa tIGO kadi zao ziko safi kwa maana ya kwamba expiry date ni 14/08/2014 kwa kadi za elfu tano nilizonunua mwezi machi mwaka huu kutoka kwa wakala wao.

Nafikiri wote watuandikie date of manufacture and expiry date lakini hasa expiry date ya ukweli kama ya tIGO ili tusiumizane; VODACOM sina imani nao kwa ili!!!
 
Back
Top Bottom