Vodacom wamezidisha wizi

Vodacom wamezidisha wizi

Kwa mfululizo wa takribani wiki kama mbili Vodacom imetulazimisha watumiaje wake/wasio wake kutumia huduma yao ya voice mail ambapo ukimpigia mtu simu ikiita bila kupokelewa automatically voice mail inakuwa activated na unapokata unaambiwa tayari umetumia either 23.2 Tshs (inategemea na umechelewa kukata kwa muda gani) hii haijalishi either ni mteja wa vodacom ama si mteja wa vodacom, Mfano kwa watumiaji wa Airtel ukimpigia mtu wa Vodacom baada ya mawasiliano tu airtel inakupa kimessage kuwa umetumia kiasi gani,


Huu ni wizi wa kulazimishana kulipia huduma ambayo mteja hajaiomba na kwa style hii wanavuna pesa nyingi sana kulingana na wateja walionao,
.Ni kweli kabisa ni wizi wakubwa! swali la kuiuliza mamlamka inayohuka no mawasiliano TCRA wanafanya kazi gani? au si kazi yao.
 
Duh voda ata mimi nimeliwa buku 2,bila ata kupiga simu zaidi ya kutuma msg moja, na hii ni mara ya pili sema tu naondoka tz ila nikirudi nadhani nitawahama hawa jamaa.
 
Wezi sana hawa jamaa, na hiyo TCRA hawajali kitu, utadhani wana ubia nao kutuibia

Kuna kitu makampuni haya ya simu yanajiamini kupita kiasi, ndio maana TCRA ianonekana kama hiko likizo vile!! We kampuni inawezaje kulazimisha mteja services ambazo hawaja-subscribe i.e matangazo yasiyo na tija, yaani hata kama una simu ya emergency unaanza kisikiliza milolongo ya matangazo ya kuhudhi tu, mara una ambiwa umejiunga kwenye voice mail wakati huja toa maagizo ya namna hiyo, mara sijui MAHELA na sijui nani kawapa kibari cha kuchezesha kamari/bahati nasibu wakati kuna Shirika la Taifa linalo husika kuchezesha bahati nasibu!

Kampuni hizi zina-rip off wateja kwa kiwango cha kutisha na hawalipi kodi stahiki ya kuchezesha bahati nasibu - chukulia mchezo huu wa bahati nasibu unao endelea, Vodacom wanasema wana wateja karibu Millioni 12 na ushee kama sikosei, ukijibu maswali yao unakatwa karibu shilling 300 kila jibu na inaonekana wameweka lengo la kukusanya shilling 1,200/- kutoka kwa mteja ambaye anaweza kuingia mtego wa kujibu maswali yao yote kwa siku; sasa kama nusu ya wateja wao wanajibu, hebu piga mahesabu ni kiasi gani cha fedha Vodacom na wenzake wanakusanya kutoka kwa raia masikini kila siku, ni nyingi sana!!

Je watu wa TRA na bahati nasibu ya Taifa wanafatilia vipi swala hili, Je TCRA ina kipengele ambacho kinazungumzia/ruhusu makampuni ya mawasiliano kijihingiza katika biashara ya bahati nasibu? Mbona kuna kampuni ya Kirusi iliwahi kuingiza vifaa vya kuchezesha bahati nasibu kwa njia ya kisasa kabisa lakini Shirika la bahati nasibu ya Taifa likavikamata vifaa hivyo na kuviteketeza eti hawaruhusiwi, ukija makampuni ya simu hayo ni ruksa!! Kuna umuhimu wa TCRA kudhibiti mwenendo wa makampuni haya ya simu nchini kwa manufaa ya wananchi.
 
Tunaaataaka Haaki zeeetuu.... Kipindi hicho niko sam wea. Unga nyuma tuelekee ofisi za tcra.
 
Samhow maoni yamesaidia naona km voicemail ya lazima imetolewa vile from voda, washavuna hizo billion walizokuwa wanahitaji!! Na hii ndo Tz
 
Mimi siwaelewi kwenye hii kitu 'caller tune". Jamaa huwa wananikata karibu mara nne kwa mwezi, sijui nijinasue vipi! Sasa hivi huwa naweka sh.500/- na kujiunga na cheka mara moja vinginevyo,wanaikomba yote eti kwa ajili ya caller tune.

hahahahahaha
 
kwa vile wewe ni chakupewa kila kitu na baba/mama ako ndo mana huon hasara ukiona jitu kubwa kama wewe kubwa ziima unaongea utumbo kama huo basi ujue hadi dawa ya meno babaako ndo anaekununulia pole sana mvi zitakuota hujui gharama hata ya chupi.

kubwa jnga hlo lpotezee
 
naomba msaada nataka kupost madayangu nianzie wapi ?
 
Sasa ''utazani'' mpaka lini badala ya kuchukua hatua. Maisha ya ki-nyumbu nyumbu

Unachangia unekane na wewe upo? tumetangaziwa kuwa kupiga cm mtandao A kwenda B ni Tsh.34 kwa dakika je kunafanyika? tafakari
 
Nashukuru Kiongozi. Nimejaribu kutuma ujumbe huo lakini mara zaidi ya mia, majibu yanakuwa hivi kila mara:"dear customer,we are experiencing a technical probe, in processing your request at the moment. please try again later". Ni try again later kila siku!

Wapigie CC mkuu watakuondoa kupitia system, 100 au 15366.
 
Na kautaritbu walikoanzisha ya kuwapigia wateja simu ukipokea unasiliza tangazo nayo ni usumbufu mkubwa sana, unaweza uko unafanya kazi zako au hata usiku umelala simu inaita ukipokea unasikilizishwa tangazo lililorekodiwa, na kwakua ni namba mpya katika hali ya kawaida mtu huwezi kuacha kupokea simu. hii tabia wanayo tigo na voda imekua kero kubwa kwa wateja.

kama wateja tawataka waache hii tabia mara 1, cc ndy watumiaji wa huduma sasa kama huduma inakua kero badala ya kuvutia w
ateja، je kuna haja gani y
a kuendelea nayo?......
 
Duh voda ata mimi nimeliwa buku 2,bila ata kupiga simu zaidi ya kutuma msg moja, na hii ni mara ya pili sema tu naondoka tz ila nikirudi nadhani nitawahama hawa jamaa.

hawa jamaa kila cku ni kiamka huwa wamesha kata pessa kwenye simu ukiwapigia wanakuambia ndani ya saa 24 zitarudi halafu hakuna kitu,mbaya zaidi sijajiunga na huduma yao yoyote,
 
.Ni kweli kabisa ni wizi wakubwa! swali la kuiuliza mamlamka inayohuka no mawasiliano TCRA wanafanya kazi gani? au si kazi yao.

Ss km TCRA wana percent zao watafanya unavyoona
 
Ama kweli watakuwa wamevuna thamani kubwa ya Tsh katika muda mfupi sana na hapo bado TCRA wahusika waliopo wanakenua tu!
 
afadhali umeiona maana wamezidi sijui wanafanya kazi gani mtandao unasumbua sana,voice mail kwa sana yahani ni shida tupu.
 
Back
Top Bottom