Bakeza
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 350
- 200
'You have received Tsh 3000 from Nipige Tafu. Total loan is Tsh 3600 inclusive of fees. Dial *149*01*99# now to borrow more!'
Nimekuwa muhanga wa kulazimishwa kukopeshwa salio na Kampuni ya Vodacom kila mara. Hali hii imenitelea kero kubwa sana maana nalazimishwa kulipa deni ambalo kimsingi silitambui.
Mara ya kwanza nilivyokopeshwa niliona kawaida ikajirudia kama mara mbili nikaona isiwe tabu nikaamua kuwapigia Vodacom custumer care majibu niliyopata ndo yakanichosha zaidi. Kwanza waliambia mfumo unaonyesha nimeomba mwenyewe mkopo nikawaambia mm sio kichaa niombe mwenyewe alafu nije kulalamika.
Basi kuna namba nilipewa nikaambiwa nitume sms ya kujitoa kwamba utakuwa umejiotoa kwenye hii huduma. Na kweli nilituma na kupokea ujumbe nimejitoa. Sijakaa sawa kama baada ya wiki mbili mchezo ukajirudia nikawapigia tena.
Ajabu yule mhudumu akaniambia huduma hiyo hauwezi kujiondoa mwenyewe bali wao ndo wanaweza kukuondoa. Basi nikamwambia niondoeni na kweli nilipokea ujumbe kwamba nimendolewa. Lakini bado alisisitiza kuwa mm ndo nimeomba mkopo kitu ambcho si kweli. Kwanza mimi nachukia sana kukopa especially mikopo ya mitandaoni sembuse salio?
Nimekaaa kama miezi kadhaa naona wamerudia kunitumia mkopo kama text inavyosomeka hapo juu.
Najiuliza inawezekana vipi mteja awe hajaomba mkopo alafu Vodacom wanamkopesha kwa lazima na bado hao hao customer care wanakwambia mfumo unaonyesha umeomba mkopo mwenyewe?
Naomba Waziri husika aingilie kati hili jambo maana ni kero kubwa sana. Kwanza nalazimishwa kulipa riba ambayo sikutaka. Pili nalazimishwa kuweka salio ambalo sikupanga maana inanilazimu kulipa deni alafu ndo niweze kupata salio jingine la ziada.
Ombi langu kwa vile taharifa zangu zote zipo ninakusudia kuwapeleka mahakamani ili iwe fundisho kwa huu wizi wanaotufanyia ninaamini wapo watu wengi sana wanaokutana na hii kadhia lakini wanaamua kufumbia macho.
Naomba mwanasheria yeyote aliye tayari tuwasiliane chemba tuone namna ya kuwashikisha adabu.
Niko Kibaha kwa sasa Mpanda