Kwanza kabisa naomba kuwasalimu wote,
Baada ya hapo kama kichwa cha uzi kinavyojieleza naomba kueleza jinsi ilivyokuwa hadi mimi kufikia hatua ya kusema kuwa VodaCom wamevujisha taarifa zangu za mawasiliano
Leo majira ya saa nane mchana, niliwasiliana na mwenye nyumba wangu kuhusu tatizo la shoti ya umeme hapa nyumbani, kwanza nilipigia simu hakupokea, nikajua huenda amebanwa na shughuli zingine hivyo nikamtumia SMS ili atakapoiona anitafute, katika sms hiyo nilieleza kuhusu tatizo lililopo.
Baada ya kama dakika 10-15, nikapokea simu (naomba namba iliyonipigia niihifadhi) huyo aliyenipigia akanijulisha kuwa yeye ni fundi umeme ameagizwa aje kutatua tatizo lililopo hapa nyumbani, kwa hiyo nikamwambia sawa nitamsubiri, na hivyo akanihakiishia kufika hapa nyumbani baada ya muda mfupi, lakini ikabidi nimtafute mwenye nyumba kuthibitisha taarifa hizo maana sikuweza kuaminin kama mwenye nyumba amewasiliana na fundi moja kwa moja bila kunipigia mimi nimweleze hali ya tatizo,
Sasa baada ya kuwasiliana na mwenye nyumba akakataa kuwa yeye hajaongea na mtu yeyote kuhusu suala la umeme zaidi ya kupokea sms ambayo mimi nimemtumia, lakini pia mimi sikuwasiliana na mtu yeyote zaidi yake kuhusu suala la umeme lililotokea nyumbani.
Hivyo moja kwa moja nikapata kujua kuwa mawasiliano hayo yamevujishwa na mtandao wa simu ninaotumia (VODACOM), baada ya hapo nikapiga simu huduma kwa wateja kuwaeleza kuhusu malalamiko yangu hayo hata hivyo walichoweza kunijibu hakikuwa na mashiko, kwa kuwa alinijibu tuu kwa kifupi kuwa wao hawana uwezo wa kuona taarifa za mtumiaji wa mtandao wao
hadi hapa nikapata wasiwasi mkubwa kuhusu uvujishwaji wa taarifa zetu watumiaji wa mtandao huu, kwa kuwa ikiwa taarifa yangu ndogo kama hiyo wamevujisha, najiuliza swali Je, ni watu wangapi wametapeliwa kwa sababu ya tabia hii, ni watu wangapi wamevamiwa kwa kuvujishwa kwa taarifa zao za safari, fedha, biashara n.k,
Tutawezaje kuwa salama kama mitandao ya simu inavujisha taarifa za watumiaji na hakuna anayesema, wote tunajua kuwa dunia ya sasa inaongozwa na taarifa/data na kama tutaacha tabia hii iendelee hatuwezi kuwa salama VODACOM BADILIKENI