Vodacom wamenipora 50,000

Vodacom wamenipora 50,000

Hawa jamaa siwaelewi niliweka shs laki 1 kwa muda tofauti, nikaenda zangu India nikawaunganishwa na roaming,nilituma msg 10, nikapokea simu kwa muda mfupi sana,pesa yote ikaondoka
 
Vodacom you people are thieves. Bado ninahasira na nyie ... niliweka sh. 10,000 muda wa maongezi, nikatumia sh. 900 ( mia tisa tu ) baada ya siku 2 kucheki salio naambiwa ni sh. 0. Kupiga customer care naambiwa eti ilitumika kwenye data! Ilitumikaje kwenye data wakati cmu yenyewe haina uwezo wa data au Internet? Baadaye nikapigiwa cmu tena na mtu wa customer care eti anataka kunifundisha jinsi ya kuzima data service kwenye cmu... halafu eti anatumai hili swala tumefikia 'closure ' nisije nikaenda kushitaki TCRA! Vodacom ni wezi kweli kweli.
 
Nadhani hawa Vodacom na Tigo wanashindana ni nani mwizi zaidi...
 
habari, kama ulitumiwa pesa hiyo na mteja mwingine ana haki ya kurudishiwa pesa yake endapo ataripoti kuomba kurudishiwa. Tunaomba namba yako ya simu pm kwa msaada zaidi.

hivi unawezaje kutoa fedha kwenye ac ya mtu bila kuwasiliana naye kwanza, mi naona fedha hiyo ingezuiliwa isitolewe halaf ukatafutwa ukweli wa mmiliki halali wa fedha. Mi mwenyewe ni wakala wa mpesa kuna siku alikuja mtu kutoa pesa nikapata ukumbe toka mpesa kuwa amefanikiwa kutoa pesa. Baadae salio halikuongezeka kwangu nilipo wasiliana na vodacom wakasema hiyo transaction haitambuliki kuwa kuna matapeli ndo wanafanya hivyo. Hiyo inaleta mashaka makubwa kwa usalama wa fedha yetu
 
Vodacom Tanzania WAMENIPORA elfu hamsini kama mchezo. Huu mtandao hakika ni majizi walioshindikana.

Nina zaidi ya mwezi sijapokea wala kuweka Mpesa. Nimeshangaa ghafla napata meseji eti TRANSACTION REVERSED. Nikadhani utani, kucheki account yangu wamekomba 50,000.

Vodacom ni kwamba hizo fedha mnazodai kuwapa watu mamilioni ndio mnaziiba kwetu? Hata kama mnawahonga TCRA hii nawafikisha mbali.

==========

Majibu kutoka Vodacom Tanzania
transaction reverse kivipi !'? Na hujapokea wala kutumiwa pesa sijakuelewa mkuu
 
Last edited by a moderator:
siweki zaid ya jero kwenye cm yangu na tena naunga bundle kabisa ukilaza pesa kwenye simu asubuh huikuti
 
Hata mimi ninamalalamiko na voda na nileishapiga simu lkn hakuwa msaada wowote walionipatia zaidi ya kunizungusha tu..ni hivi, mimi no wakala wa mpesa sasa huwa kuna kamisheni zinatoka kila mwisho wa mwezi lkn cha kushangaza walituma kamishen ktk 2nd na mm kuihamishia kwenye akaunt ya kazi fedha hiyo haijafika mpaka leo hii na nikiwapigia cm wala ooh..wasiliana na wakala mkuu na nikimpigia wakala ananambia ntakupigia baadae yani imekuwa ni kama nawakera vile..sasa uamzi niliofikia ni kupata msaada wa kisheria ili niweze kuwafungulia mashtaka maana walicho kifanya ni wizi mtupu..

Nilishaambiwa kuna watu wa sisiem wanamaslahi vodacom, mnataka hela za kampen wazitoe wapi? Labda mniambie km hampend kofia, tshet na kanga mwaka huu!
Badiliken chukuen hatua
 
Vodacom Tanzania najua hampo tena Jamiiforum lakini ushauri huu utawasaidia ... boresheni kitengo chenu cha huduma kwa wateja, ni bure kabisa na hii inawezakuwa ni matokeo ya kutotoa training za kutosha, job rotation na maslahi duni. Kubwa wanaloweza kujibu ni kukuambia uende kwenye VODA SHOP iliyokaribu yako ... kitu ambacho hata mtoto mdogo anaweza kujibu

Wapeni wahudumu wenu uwezo wa tutatua shida za wateja kabla simu haijakatika na si tu kuwapa notebook na wao kazi yao kuwa kurekodi na kukueleza uende kwenye ofisi iliyo karibu yako. Kwa hali hiyo, huwa sioni kwanini mmewaajiri hao watu kwani tayari tunajua tukiwa na shida tuende kwenye ofisi zenu za karibu kwa utatuzi ....
 
ni hivi kama pesa imeingia kwako kimakosa inarudishwa kwa mwenyewe sasa wewe sijaelewa ikawaje ukatwe na umechukua hatua gani pole mkuu
 
Ngoja niende halotel aiseee....salio linakatwa eti unatumia bundle wakat iko kwenye tochi
 
Nasikia hii ni part two ya Makontena ya bandari. Baada mianya kule kuzibwa, sasa wamehamia huku, nilishawahi kuuliza, kuhani Vodacom kwann Tcra, na serikali imefyata mkia, inapotezea, Vodacom Kuna mkono wa nani?
 
Back
Top Bottom