Tetesi: Vodacom wameanza maboresho ya kuongeza tozo kwa miamala ya fedha

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
23,519
21,546
INTRODUCTION
Kampuni ya simu ya VODACOM inasemekana leo imeanza rasmi mchakato wa kuongeza tozo kwa wateja wake wanaotumia huduma za MPESA kwa lengo la kukabiliana na gharama za uendeshaji ifikapo 01/07/2016. Serikali iliamua kutoza 10% ya kodi ya miamala, kiasi ambacho ukijumlisha na 18% ya VAT unapata 28%. Ili kuepuka kupata hasara, kampuni imeamua kuongeza 28% ya gharama za utumaji na utoaji fedha kwa wateja wote wanaotumia huduma za MPESA.

USHAHIDI
Zifuatazo ni meseji za KIKATILI ambazo zimetumwa kwa wateja wa VODACOM kuhusu “maboresho” ya huduma za MPESA:

MESEJI NO 1
Ndugu mteja, tunafanya maboresho ya MPESA hadi Jumapili saa 7 mchana. Kutuma pesa kwenda mitandao mingine nenda M-PESA > TUMA PESA > Chagua MITANDAO MINGINE . Time: 6/17/2016 3:01:40 PM

MESEJI NO 2
Leo saa 4 usiku hadi Jpili saa 7 mchana hautaweza kubadili PIN au lugha ya M-Pesa kupisha maboresho ya M-Pesa. Ukihitaji kufanya mabadiliko hayo yafanye mapema. Time: 6/17/2016 3:02:04 PM

TUTANYOOKA
Wale waliokuwa wanatuimbia kwamba “TUTAISOMA NAMBA” ngoja tuisome sote sawia. Huu ni mtego wa panya ambao utanasa waliomo na wasiokuwamo. Hadi ifikapo 2020 tutakuwa tumenyooka. Na bado……mabenki nayo yapo mbioni “kuboresha” huduma zao! Ngoja tunyooshwe hadi tunyooke.



UPDATES
sasa sio TETESI tena....ni dhahiri makampuni ya simu yote nchini Tanzania yameongeza gharama za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu na tayari marekebisho hayo yameishasambazwa kwa mawakala wote. nimebahatika kuona nakala hiyo ila nilishindwa kuipiga picha na kuiattach humu kwa sababu simu yangu feki imefungiwa na TCRA. naomba mdau yeyote atakayeipata nakala hiyo aipige picha na kuitupia humu ili kila mtanzania aangalie maumvivu atakayopata. tafadhali administrators naomba mbadilishe status ya heading ya uzi huu kutoka kuwa TETESI na kuwa BREAKING NEWS. na bado.....mabenki nayo yataongeza gharama za kuchukua fedha na kuangalia salio very soon....satay tuned.....tuko pamoja katika maumivu haya hadi mwisho wa dahari!
 
hapa kama kweli wanajiandaa kuongeza makato, inabidi regulator aonyeshe anafanya kazi kwa maslahi ya wananchi. maana tuliambiwa vodacom/mobile operator
wanakatwa kipato ambacho kilikuwa hakikawi kodi sio kwamba wameongezewa kodi
 
Kwahio maboresho
Yanahusu kuongeza makato?
kwanini mnapenda kupotosha ninyi!!

Ktk m-pesa kulikuwapo kipengele cha kutuma kwenda mtandao mwingine?
Wakati wanafanya maboresho uliongezewa makato?

Kwa ntumiaji wa mara kwa mara wa huduma hizi
kitu maboresho ni chakawaida

Haijawai kufika mwezi mzima voda bila kuwapo na kitu hicho
 
Kwahio maboresho
Yanahusu kuongeza makato?
kwanini mnapenda kupotosha ninyi!!

Ktk m-pesa kulikuwapo kipengele cha kutuma kwenda mtandao mwingine?
Wakati wanafanya maboresho uliongezewa makato?

Kwa ntumiaji wa mara kwa mara wa huduma hizi
kitu maboresho ni chakawaida

Haijawai kufika mwezi mzima voda bila kuwapo na kitu hicho

We inaonekana hata si mtumiaji wa Mpesa ila unabisha tu..hujawahi tuma pesa yako kwenda kwa mtu mwenye tigopesa kupitia Mpesa
 
We inaonekana hata si mtumiaji wa Mpesa ila unabisha tu..hujawahi tuma pesa yako kwenda kwa mtu mwenye tigopesa kupitia Mpesa
Unatuma bila shida

Nilini ulikuta kipengele Tuma kwenda mtandao mwingine
hapo kabla?


1-Tuma pesa
2-Toa pesa
3-Nunua muda wa maongezi(japo kwa sasa kuna maboresho ya Vifurushi)

Kipengele cha kutuma mtandao mwingine kilikuwa namba ngapi hapo kabla?
 
Back
Top Bottom