Wizi Vodacom!

Kirchhoff

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,621
8,293
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale ya Wateja wa Vodacom Tanzania. Malalamiko haya si kwa watumiaji wa airtime tu, Bali Vifurushi vya data na hata watoaji wa Huduma ya M-PESA pia.

Mimi nitoe ushahidi wa nilivyoibiwa na Vodacom. Japo bado nautumia mtandao huu, ni vema wahusika wakaurekebisha kwa kufuatilia kwa ndani zaidi mienendo ya wafanyakazi wao ili tuendelee kupata Huduma bora.

Mie niliwahi kuibiwa 1GB. Yaani nimejiunga ikaja Meseji nimefanikiwa kujiunga dakika 150, SMS bila kikomo na 1GB kutumia wiki nzima kisha nikawasha data nashangaa sipati internet. Nikadhani labda tatizo la mtandao nikajaribu baada ya robo saa kimya. Nikachukua simu ya my dear lara1 kucheki anabrows tu bila shida yeyote. Basi nikapiga *149*60# kujua Salio.

Hee nikakuta nina dk 150, SMS bila kikomo na 0MB!
Wiki nzima Vodacom wanaishia kuniambia kifurushi kinarudishwa Wateja ni wengi mno. Sasa nikajiuliza Kama mie tuu sijarudishiwa je ni wangapi hawajarudishiwa na wizi huu tuvumilie hadi lini?

Ila bora Voda hivyo hivyo hata Kama saa nyingine wanakwiba. Huko kwingine malalamiko ni mengi Sana.

Nb: lara1 katumika kumuwakilisha mupenzi tuu.
 
Ndugu zanguni VODA sio wezi bali ni MAJAMBAZI! mie huwa naweka 30,000 kwa mwezi najiunga na CHEKA na bado mwezi haishi kinakwisha! Naomba tu ule mtandao wetu wa TTCL uanze tuachane na hawa MAJAMBAZI!
 
Hivi inakuwaje dakika za voda za cheka ya wiki zinaisha fasta hivyo?
 
Back
Top Bottom