VODACOM waja na 1\4 shilingi kwa sekunde | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VODACOM waja na 1\4 shilingi kwa sekunde

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lucchese DeCavalcante, Apr 16, 2010.

 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Habari ndiyo hii ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde hivi karibuni.  HIVI karibuni Vodacom Tanzania imezindua huduma ya Cheka Time ambapo mteja atatumia robo shilingi kwa sekunde. Hii ni huduma ya aina yake na hajawahi kutokea katika historia ya mawasiliano hapa nchini.  Kwa mantiki hiyo, Vodacom hivi sasa ndio imekuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa huduma kwa gharama nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine nchini ambazo Watanzania walio wengi wanazimudu.

  Vodacom hivi karibuni pia ilizindua huduma ya HABARI NDIYO HII kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kweye familia yake na kwamba kupitia huduma hii wateja wa Vodacom wanaweza kupiga simu kwa kiwango cha shilingi moja kwa sekunde kwa masaa 20 kwa siku.
  Huduma hii ni Vodacom kwenda Vodacom pekee.Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba amesema kwamba wateja wa Vodacom kupitia CHEKA TIME kwa wale wanaojisajili kwa shilingi 200 na shilingi 500 sasa wanaweza kuongea kwa chini ya robo shilingi kwa sekunde, sawa na senti 0.22 kwa sekunde.
  “Hii inamaanisha kwamba Vodacom sasa ndiyo mtandao unatoa huduma kwa gharama rahisi kuliko mitandao mengine yote nchini”, amesema.Kwa mujibu wa Bi Makamba, huduma hii itaiwezesha familia ya Vodacom kuwasiliana kwa gharama ya chini zaidi na kwamba ana imani kwamba huduma hii itachochea ukuaji wa uchumi wetu kwa maana ya Watanzania wenye shughuli mbalimbali wana uhakika wa kuwasiliana bila kikwazo chochote.
  Anafafanua kwamba mbali na huduma hii viwango vingine vya CHEKA TIME ya shilingi 2000 na 5000 bado vinaendelea kutumika kama kawaida.Bi Makamba amesema kwamba huduma ya Vodajamaa nayo inaendela kama kawaida, ambayo ni mojawapo ya njia inayoiwezesha familia ya Vodacom yenye watu zaidi ya milioni saba (7) kuwasiliana kwa gharama nafuu kwa dakika na mteja anaweza kusajili watu watano kwa mara moja na watu 15 kwa mwezi mmoja.
  Huduma ya hii inamaanisha kwamba zaidi ya wateja milioni saba wa kampuni ya simu ya Vodacom nchini watanufaika na huduma hii mpya ya ‘HABARI NDIYO HII’ itakayokuwa endelevu na sio ya kipindi maalumi”, amesema.
  Kiwango hiki cha malipo kwa watumiaji wa simu wa Vodacom Tanzania ni muendelezo wa utoaji wa huduma na promosheni zinazoambatana na zawadi mbalimbali ambazo huwafanya watumiaji wake kuwasiliana kwa urahisi.


  Bi Makamba ana matumaini kwamba mabadiliko ni hakika, kuanzishwa kwake kutaboresha sekta ya mawasiliano nchini na kuwapa fursa wateja kuongea zaidi na zaidi na hivyo kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo kwani mawasiliano ya uhakika ni injini ya maendeleo.“Wengi wanadhani ni jambo lisilowezekana kwamba Vodacom, ambayo inachukuliwa kuwa inatoza huduma zake kwa gharama za viwango vya juu sokoni, kuamua kutoa huduma zake kwa gharama za chini na kuweza kuendeleza nyingine”, amesema.
  “Vodacom Tanzania inachukua fursa hii kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma na kuleta bidhaa zilizokuwa na ubora wa hali ya juu. Vodacom imekuwa ikitoa huduma za simu kwa muda wa miaka kumi sasa na inatarajia kukua zaidi katika sekta ya mawasiliano kwa mwaka huu na miaka ijayo”, ameongeza.Bi Makamba alifafanua kwamba Vodacom ina shauku kubwa kwa kutoa huduma hii iliyokuwa rahisi na ya bei ya chini katika soko la wakati huu kuliko kampuni nyingine zote za simu hapa nchini.
  Huduma hizi za Vodacom pia ni muafaka kabisa kwa wanavikundi mbalimbali vya uzalishaji mali, wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati, wakulima, wanafunzi,wafanyakazi pamoja na wanafamilia.Kuhusu huduma nyingine kama M-PESA amesema kampuni yake inawashukuru wateja wake zaidi ya milioni mbili ambao wamesjisajili na huduma hii.Amesema hii ni hatua muhimu lakini pia kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri, mathalani kupitia huduma ya M-PESA wateja wa Vodacom kwa kutumia simu zao za mkononi hivi sasa wanaweza kulipia ankara za Umeme, maji na DSTV bila kupanga foleni lakini pia kupata huduma kwenye maduka makubwa.

  Wateja wa Vodacom wanaunganishwa na Vodafone M-PESA, huduma inayotolewa kwa ushirikiano na kundi la Makampuni ya Vodafone.

  Ametoa mfano wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Dawasco, imeanzisha huduma ya bure ya kulipia maji, ambapo wateja wa Vodacom Tanzania sasa wanaweza kulipia ankara zao za maji kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma ya Vodafone M-PESA.
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Ndo manaaaaaakeeeeeeeeeee!!!
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Bado si kweli kimantiki.......tigo takes the lead..........weka senti zako hizo kwa watu wote na si mpaka ukatwe 200
   
 4. Bon

  Bon Senior Member

  #4
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 107
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa hawako wazi,lazima kuna hidden cost hawazitaji.
  Tigo bado iko juu.
   
 5. R

  Renegade JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,075
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ni wajanja wajanja ,TIGO.
   
 6. b

  bwanashamba Senior Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aya makampuni ya simu yanatuzingua tu
  sisi tunataka kampuni ambayo itatoza kiwango
  kidogo kwenda kwenye makampuni yote na
  si tigo to tigo'au voda to voda,au zantel to zantel ayo ndo ma
  wasiliano tunayotaka'kwetu sisi walalahoiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 7. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hiyo cheka time yenyewe ya Tshs 500 inapatikana kwa tabu sana.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Jamaa walioko huko home wananambia kuwa kuna congestion dunia nzima kupata line kaaazi kweikwei, tumerudi enzi zile za simu za kukoroga kwa operator!
   
 9. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Asanteni tigo, mmesababisha wanyonyaji watupunguzie gharama.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Voda weziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii tupu. Nilishawishika nihamie huko mara ya kwanza hiyo cheka ilipoanza nikaipata kirahisi sana lakini sikuweza kuitumia vizuri maana wengi nilio na simu zao ni makampuni ambayo si voda kwa hiyo ikaniwia vigumu hata kuzungumza nusu saa.
  Mara mbili nilikuwa ninajiunga katika hiyo chekatime tena kuanzia saa 6 usiku ndio ilikuwa rahisi kupata mchana si rahisi. Hata hivyo Baada ya kuhangaika sana, maana mara nyingi nilijaribu kati ya mara ishirini na hamsini ili nipate kusajiriwa cheka time. Lakini mara ya tatu niliumia sana maana mbali na kutumia saa moja na nusu kujisajiri cheka time mke wangu alikuwa anahitaji kuzungumza na mtu wa voda na kwa kuwa nilikuwa naamini nina hiyo cheka, nilimpa lakini baada ya kuzungumza kwa dakika 5 ilikuja message kwamba pesa imekwisha. Tangu siku hiyo nimekoma kupoteza muda wangu.
  Nimeamua bora niendelee kufurahia huduma ya tigo ambayo ni nafuu hata kama unaunga na simu za mtandao mwingine.
  HAWA NI MATAPELI TU HAMNA LOLOTE. Mtandao ni tigo bwana.
   
 11. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Bila kuwepo kwa TIGO hao Voda,ZAIN.WANGEENDELEA KUTUNYONYA TU,SA WAMEZINDUKA BAADA YA KUONA WANAZIDI KUPOTEZA WATEJA........ILA TIGO BADO INAGHARAMA NAFUU SANA TENA....HAINA MASHARTI...........WE UNAPIGA TU................UNALONGA TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU..................
   
 12. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa jamaa zangu Vodacom bado hawana jipya. Hiyo senti 0.22 kwa sekunde maana yake mpaka uisajili kwa sh. 200. Kama wajanja si waiachie moja kwa moja
  Hiyo sh. 200 ni dakika 15, kwa ukigawa 200/dk15 ndio unapata sekunde moja kwa senti 0.22. Halafu ndio wanasema ndio mtandao wenye gharama nafuu, hakuna lolote. Kwa mtindo huo tuje kwa hawa waasisi TIGO,

  Wao wana mini extrem sh. 250 kwa dakika 25, ukigawa 250/dk25 ndio unapata senti 0.17 kwa sekunde. Sasa hapa nani nafuu zaidi? TIGO oyeeee!!!!!

  Vodacom msitubabaishe bwana.
   
 13. M

  Madevu Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hizi zote ni faida za soko huria, thanks to TCRA, mawasiliano yameendelea kuwa na nafuu sana nchini...na bado tutaona makubwa zaidi...
   
 14. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hayo ni maneno tu tigo ndo hawana longo longo
   
 15. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tigo usipime imetuokoa sana, kuna jamaa walikuwa wanasema tigo ya wanafunzi ofisini kwetu maana mimi nilikuwa na tigo mwisho wa siku nikawaona wana wana vichip vya tigo wanaweka wanawasiliana na baadae wanaweka voda eti kwa sababu watun wengi wanajua simu zao za voda. Cha kuchekesha wajameni kuna baadhi ya wafanyakazi wa voda na celtel wana line za tigo hahahhhahaha !
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  lengo si kupiga kelele nani mwizi kwani jinsi watavyoshindana ndio nafuu kwa watanzania najua tatizo kubwa voda kuchukiwa ni Rostam
  lakini kwa mwenendo tunaoenda nadhani ni wakati wa serikali kuyabana na kuchukua kodi stahiki kwani wanaweza kuchunguza simu
  zinazopigwa kupitia katika mkongo wake, pili kampuni ya tigo nayo ije na jipya zaidi lengo ni kuboresha huduma za simu na ni wakati muhafaka
  wa kutunga sheria zitazowabana tigo na voda kuuza hisa kwa wananchi ni lazima at least 40% ya kampuni zote za kigeni zimilikiwe na wazawa
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nadhani Zain ndo wana nafuu kuliko wote. Wao ni sh 1 kwa sekunde mchana kutwa halafu shilingi 1 kwa dakika usiku kucha!Shilingi moja kwa dakika ni sawa na sh 0.017 kwa sekunde. Hii utaipata wapi kwengine?
   
 18. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Tunataka affordable unlimited internet jamani
   
 19. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha kushangilia hiyo tariff hawajaiweka kwa kupenda walikuwa wapi siku zote? Hii ni janja ya tukose wote wanataka kuwakomoa Tigo,nauliza tena siku zote walikuwa wapi au sasa ndio Vodacom imeanza kuwajali wananchi,,kwa taarifa hawa jamaa wanataka kuvuta wateja wengi then wa walock kwenye mtandao wao na baada ya kufanikiwa wataongeza tena bei ya kupiga simu kwani wakichukua wateja wengi kampuni hizi ndogo haziwezi kushindana. Kwa hiyo tariffu ya robo shilingi,narudia tena hakuna kampuni itakayoshamiri kwa kutumia hicho kiwango ,ni hasara tupu.Najiuliza TCRA wako wapi ?lakini ngoja tujionee hii picha,I wish haya mambo yangetokea kwenye Kampuni za Bia,soda na Tanesco hasa Tanesco watuletee washindani wengine
   
 20. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama wanadhani hapo ndo watavuta wateja wa tigo wamenoa!
  Tigo hoyeeeeeee, tunasubili jambo moja tu, nyie shusheni kwenda mtandao mwingine bac! Japo mfanye nusu gaharama ya sasa, chip za voda na zain nawambieni zitachomwa moto!

  Ila asanteni sana tigo, hadi mmewafanya wezi hawa warudi huku tulipo. Jitahidini tigo muongeze wigo wa mtandao wenu huko mikoani. Tuko pamoja!
   
Loading...