VodaCom Vipi? Please chew what you can bite | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VodaCom Vipi? Please chew what you can bite

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ByaseL, Oct 6, 2009.

 1. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya Simu za Mikononi VodaCom sasa hivi wanaendesha kampeni kabambe ya Tuzo Points. Kampeni hii inauhusisha mteja ku-redeem points zako na kuweza kupata zawadi mbali mabali kuanzia na SMS za bure hadi kupata laptop n.k.

  Lakini kwa sasa kuna tatizo katika wateja wanao redeem points 10,000 ili kupata kile wanachokiita Simu namba 1. Ukisha redeem hizo points 10,000 VodaCom wanakuletea message nzuri inayosema hongera umejishindia Simu namba 1. Fika katika ofisi yoyote ya VodaShop ukaoneyeshe reference namba uchujue simu yako. Good stuff.

  Wateja wa voda kama mimi waliojishindia simu 1 kwa muda wa wiki mbili sasa tumekuwa tunakwenda VodaShop kujipatia "zawadi" zetu bila mafanikio. Kila tukienda tunaambiwa "njoo kesho" labda simu yako itakuwepo. "Njoo kesho" inanikumbusha zamani ambapo msemo huu ulikuwa ni msamiati wa kila ofisi hapa nchini. Kila ukifuatilia jambo lako uliambiwa "njoo kesho"!! Mwishowe unakata tamaa.

  Kusema kweli ni jambo la aibu kwa Kampuni kama VodaCom kuweka promotion ya zawadi alafu wateja wanapata zawadi lakini inachukua zaidi ya wiki mbili kila wakienda wanaambiwa "njoo kesho". Kuna wengine tumeulizia kama tunaweza kurudishiwa points zetu tuachane na hiyo "zawadi hewa" au kwa kihaya "ekichupuli" lakini unaambiwa hiyo haiwezekani ila subiri "zawadi" zinatakuja tu. Lini? "hatujui" wanajibu customer services agents ambao kusema kweli lugha yao haina u-customer service hata punje!

  But why did VodaCom chew what it could not bite? What a shame!! KICHUPULI ZII.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,021
  Trophy Points: 280
  Tukiwaambia karibuni TiGo mnatuona tumefulia. Poleni!
   
 3. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli mkuu. Ni vibaya kwa kampuni ya kimataifa kama VodaCom kuweka promotion ambayo ni vigumu ku-deliver kwa wakati muafaka. Kuwambia wateja njoo kesho ni dalili kwamba Idara ya masoko haikujipanga vilivyo. Kuna haja ya VodaCom kupata somo toka kwa wengine kama Tigo na Zain.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Siipendi sana kampuni hii.

  Hawa jamaa huwa wanatoa zawadi kwa kinyongo sana, nadhani wanaumia kishenzi.

  Actually hawako friendly kabisa as far as business is concerned. Mi nawalaumu watu wanaowang`ang`ania hadi leo.
   
Loading...