Vodacom Tanzania wizi mmeanza lini?

Vodacom Tanzania wizi mmeanza lini?

alma gemela

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
842
Reaction score
280
Wapendwa habarini za asubuhi

Vodacom tanzania ni mtandao nilikuwa nauamini sana, ila jana wamenialibia siku sababu wanakula ela yangu bila kusema sababu ya kula ela yangu.

Nilijaribu kuongea na castomer care sijapata msaada wowote ule zaidi ya kusema matumizi yako hayaonekani piga baada ya masaa matatu, mchana nikapiga tena majibu ni yale yale na usiku pia nimepiga majibu ni yale yale.

Swali kwa nini matumizi ya kukatwa ela yasionekane lakini ya mengine yaonekane?

Wananikata ela wakati sijajiunga na huduma yoyote inayokata ela

Application zangu za blackberry ni za kawaida sana, siku ya jana sijaangalia video ya aina yoyote zaidi ya kupokea mails na kusoma blogs na kuingia jf

Mpaka sasa salio langu ni sh 0 naogopa kuweka hata vocha.

Ni mimi pekee nakatwa ela au kuna wenzangu pia



Alma

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
By default,App ya JF kwenye BB inatumia APN ya WAP/AUTO,badilisha chagua BIS.
 
Mimi nilikatwa 32000 kwa siku bila maelezo .... Wajinga sana sina hamu afu wanakwepa sana simu za matatzo ya kupotelewa na hela au kufidiwa huduma ambayo ulikua haupati
 
Yaani sitamani hata kuweka vocha

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Yaani sitamani hata kuweka vocha

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
hamna haja ya kuongeza salio utaibiwa,siku hizi wanalazimisha utumie ringtone wanakata pesa kila baada ya siku tatu.

Eti ongeza salio ili uweze kupata ringtone nyingine ambayo sijaomba.
 
nimeskia ifikapo april 2014 Blackberry watafungiwa wana bankcrupt,. Kama unayo uza hata kwa bei rahisi kuliko kukosa yote,. Mimi nilikuwa nayo 9700 nikawa nakatwa katwa tu hovyo,.
 
Siku hizi ukizubaa kidogo tu lazima ukatwe kidizaini flani hivi.

Mi nilikuwa nikijiunga bundle la internet nikianza ku_surf tu wanakata kiasi cha pesa kilichobaki badala ya bundle kwa hio nikashtuka. Saiv ni mwendo wa kuweka pesa kamili tu ya kujiunga na bundle.
 
nimeskia ifikapo april 2014 Blackberry watafungiwa wana bankcrupt,. Kama unayo uza hata kwa bei rahisi kuliko kukosa yote,. Mimi nilikuwa nayo 9700 nikawa nakatwa katwa tu hovyo,.

Duh! Sijakuelewa. Yani wana nini?
 
Disappointed AT? Duh!

Wewe ni native wa hii lugha eh...
"Disappointed In someone" suggests that your disappointment really derives from the person's character/personality.
 
Vodacom ni majizi original..wanauza namba zetu kwa makampuni ili watutumie promotion sms
 
Watanzania wanaibiwa na makampuni ya simu ambayo kazi yao ya kwanza ilikuwa kuua kabisa TTCL ili waweze kuwakamua Wananchi sawa sawa. Makampuni ya simu yote wenye hisa ni kina Lowasa, JK, na wezi kama hao, sasa kama mmekubali kuibiwa mchana kweupe msilalamike. Huu ni ujambazi ambao una baraka kutoka Ikulu.
 
mimi tokea jana nikinunua Bando la BB sipati Access ila hela yangu inakatwa
 
wezako wanavohamia 'hakatwi mtu hapa 'wewe ulikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom