kenethedmund
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 347
- 89
Kuna tatizo kubwa ambalo ni la hatari kwa Mfumo mzima wa Mpesa, Unatuma fedha kwa bahati mbaya ile hela inaenda kwa mtu mwingine ambae sio mlengwa, na unapopiga simu kwa huduma kwa wateja namba 15000 ambayo unasikilizishwa mziki kwa dakika 10 ndio wanakuhudumia kiasi cha kwamba unakuta ile hela imeshatolewa na huyo mteja ambaye sio muaminifu na matokeo yake unaambiwa endelea kutupigia atakapoweka pesa ndio tutamkata. Fikiria umetuma laki tano alafu inaenda kwa mtu ambae kwa mwezi ela inayowekwa kwenye simu yake aizidi elfu hamsini lini utapata hiyo ela?
Pendekezo ni bora wangeweka kiwango kuanzia laki moja na kuendelea mtu akitumiwa hiyo pesa asiweze kutoa mpaka either dakika 10 au 15 ziwe zimepita ili kuruhusu mtumaji kuweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kusitisha muamala endapo alituma hio pesa kimakosa waweze kumsaidia na kuzuia huo muamala usifanyike.
Naomba tujadili
...wamekuja kuahidi kurekebisha, nasubiri kauli yao ya mwisho mwanasheria wangu apate pa kuanzia...Mkuu tuko tayari kwa mapambano elekeza usaidiwe vipi ,nimenuna mbaya wameshatapeli wife hhao kima!
kitu chochote ambacho kina idadi kubwa ya watz ujue hamna k2. anza na chama cha siasa, kampuni ya cm n.k. tafakari
...mkuu MZAWA JF sikuelewi..! ngoja tukomae nao unajua hiyo namba ipo sehemu nyingi za muhimu kwetu, kama hawataki kuturudishia waifute kabisa kuliko kumpa mtu...
Makomredi,
karibu wote mmelipuka kwa jazba mkimtuhumu kuwa mlalamikiwa ni mwizi na ndiyo tabia yake. Safi kabisa. Hata mimi nimejisikia vibaya sana kusikia wengi wetu tunalizwa na wajanja wajanja wasiotaka kufuata taratibu za kibiashara.Lakini Je, wangapi kati yetu tumechukua hatua stahili? Huenda tunapuuzia au hatufahamu nini cha kufanya. Ushauri wangu kwa aliyeporwa namba ni huu:
1. Mkondo wa kisheria wa kushughulikia malalamiko ya kampuni za simu unaanzia TCRA. wapigie simu au ingia kwenye website yao ujaze fomu za malalamiko ukielezea kile kilichotokea. TCRA ana wajibu wa kisheria wa kuchunguza suala hilo, kuwaita wewe na Vodacom, ka kukusaidia haki yako ipatikane. Unaweza kudai namba yako pamoja na malipo ya usumbufu ulioupata wakati namba imeporwa.
2.Ikiwa hutaridhika na namna TCRA wanavyoshughulikia suala lako, basi unakata rufaa Fair Competition Tribunal, ambako watachunguza namna haki yako ilivyobinywa na Voda, na TCRA, na hatimaye utapewa haki yako. Kuna mzee mmoja wa Mtwara mwaka juzi alifanyiwa hivyo hivyo, na hatimaye FCT waliamuru alipwe fidia ya sh milioni 3 hivi.
Twende zaidi ya kulalamika. Huna hata haja ya kuchangisha pesa za wakili mkuu...
That good,just know that we are ready to set an example so that this shall never happen again in future!...wamekuja kuahidi kurekebisha, nasubiri kauli yao ya mwisho mwanasheria wangu apate pa kuanzia...
Kuna tatizo kubwa ambalo ni la hatari kwa Mfumo mzima wa Mpesa, Unatuma fedha kwa bahati mbaya ile hela inaenda kwa mtu mwingine ambae sio mlengwa, na unapopiga simu kwa huduma kwa wateja namba 15000 ambayo unasikilizishwa mziki kwa dakika 10 ndio wanakuhudumia kiasi cha kwamba unakuta ile hela imeshatolewa na huyo mteja ambaye sio muaminifu na matokeo yake unaambiwa endelea kutupigia atakapoweka pesa ndio tutamkata. Fikiria umetuma laki tano alafu inaenda kwa mtu ambae kwa mwezi ela inayowekwa kwenye simu yake aizidi elfu hamsini lini utapata hiyo ela?
Pendekezo ni bora wangeweka kiwango kuanzia laki moja na kuendelea mtu akitumiwa hiyo pesa asiweze kutoa mpaka either dakika 10 au 15 ziwe zimepita ili kuruhusu mtumaji kuweza kuwasiliana na huduma kwa wateja kusitisha muamala endapo alituma hio pesa kimakosa waweze kumsaidia na kuzuia huo muamala usifanyike.
Naomba tujadili
Habari kenethedmund tunapenda kukukumbusha kuhakiki jina la mpokeaji kabla hujathibitisha kutuma pesa ili kuepukana na makosa yanayoweza kujitokeza. Ahsante
Kwa mawazo kama haya tutaendelea kuibiwa na kunyanyaswa.Key board imeteleza au unamaanisha utachangia mawazo maana mie ndio mkusanyaji wa hela za wakili, kwa ujumla jamaa wasanii hawa alafu ukiwaendea wanachulia simple kabisa line yako amepewa mtu mwingine ingia hapo andikisha line nyingine. Alafu vitu vingine si lazima kwenda mahakamani ifike mahala serikali itusimamie kwa kuweka dawati maalumu za case hizi kujadiliwa na watu maamlumu kisha wanafanya maamuzi maana na mahakama zetu milolongo kibao ukichanganya na wakili wetu kupenda kuangalia weakness point wakati wa kufungua madai na kuikomalia ili mradi siku ziende na wewe ukate tamaa
Habari Gefu, endapo namba hii aliitumia kwa muda kisha akaacha kuitumia kwa zaidi ya miezi 3 namba hufutwa taarifa za awali na pesa yake inatunzwa akaunti maalum ambapo mteja atatakiwa kwenda Vodashop kujaza fomu na atapatiwa pesa kwenye namba mpya atakayokuwa ameijaza katika fomu.
Tunaomba namba ya simu kwa msaada zaidi tafadhali.