Vodacom Nitawashtaki

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Leo nimechafukwa kupita maelezo!

Hivi nyie Vodacom Tanzania kwanini mnaniibia? Kwanini mnaniunga na huduma bila ridhaa yangu na kuanza kufyeka salio langu? Cha kusikitisha nilipowapigia watoa huduma wenu (customer care) wanasema eti nilijiunga na huduma inaitwa SOKA LETU, jamani Vodacom Tanzania mimi nina akili timamu sijawahi kujiunga na huduma hizi za ajabu ajabu maana najua zinagharimu pesa na sina pesa za kuchezea,simu yangu sijawahi kumpa mtu tangia huu mwaka uanze mpaka unaelekea kuisha,uenda mngesingizia kuna mtu nilimpatia simu akajiunga!!

Kujiunga na huduma hizi za ajabu ni process,hivyo sina muda huo wa kukaa na kuanza kujiunga na huduma za wizi hizi!.

KWANINI MMENIIBIA? KWANINI MMENIUNGA NA HUDUMA NA KUANZA KULAMBA SALIO LANGU BILA IDHINI YANGU?

Vodacom Tanzania tafadhali naombeni majibu, la sivyo hili litawagharimu! Na mmeendelea kuwaliza Watanzania wangapi kwa huduma za wizi hizi? Kwanini mnafanya hivi?

TCRA tafadhali naombeni msaada
 
Hiyo michezo mbona ipo sana hata Tigo wanayo hiyo michezo.
Hapo cha kufanya, ingia kwenye huduma extra
Sitisha matumizi bila bando Calls, Sms + Data. Hapa hata ukiweka hela ukawasha data utaikuta hela yako. Hawalambi hata mia
Wezi wakubwa hawa,mkuu huwezi amini sijawahi jiunga na huduma hizi za kijinga kwasababu huwa naelewa zinakula salio bila sababu ya msingi!,na wameshajua watanzania wengi hawafuatilii na hata wakifuatilia watabaki kuumia tu moyoni,hivyo wanakuungwa bila wewe kujua na wanaanza kufyeka salio.

Hebu fikiria waungwe watu hata milioni 1 kwa mara moja na wafyekwe kila mtanzania 100,Huu wizi mkubwa sana na haukubaliki,na uenda hata viongozi wa serikali wasiyo waaminifu wana mkono hapa!
 
Hili hata mimi limenikuta! Jana tu nimepokea message toka Voda ikinipa hongera kwa kuniunga na huduma ambayo mimi binafsi sijajiunga! Walishaniunga na huduma kinguvu hivi hivi na nilipoweka salio wakalifyeka kulipia huduma hiyo! Playinc07!!!
 
Hiyo michezo mbona ipo sana hata Tigo wanayo hiyo michezo.
Hapo cha kufanya, ingia kwenye huduma extra
Sitisha matumizi bila bando Calls, Sms + Data. Hapa hata ukiweka hela ukawasha data utaikuta hela yako. Hawalambi hata mia
Na voda wananitumia sms kila saa, niruhusu hiko kitu.

Kuwa bando likiisha waendelee na salio, nawashangaa sana.
 
Hili hata mimi limenikuta! Jana tu nimepikokea message toka Voda ikinipa hongera kwa kuniunga na huduma ambayo mimi binafsi sijajiunga! Walishaniunga na huduma kinguvu hivi hivi na nilipoweka salio wakalifyeka kulipia huduma hiyo! Playinc07!!!
Hawa wajinga wameshatuona watanzania mabwege sana,yaani pamona na rundo la huduma mbovu bado wanatuibia,we ngoja najua ipo siku itawagharimu na hawataamini wanachokifanya
 
Hiyo michezo mbona ipo sana hata Tigo wanayo hiyo michezo.
Hapo cha kufanya, ingia kwenye huduma extra
Sitisha matumizi bila bando Calls, Sms + Data. Hapa hata ukiweka hela ukawasha data utaikuta hela yako. Hawalambi hata mia
Hata ukisitisha matumizi bila bando, voda wanakata salio. Kwa mfano ukiwa na salio kwenye simu, usipotumia, baada ya kila siku moja utaona imepungua tsh 99 hadi salio linaisha.

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Wahuni sana na wamekuwa wezi wakubwa!,mimi nilikuwaga nikiona watu wakilalamika nilikuwa nachukulia poa sana nikidhani uenda watakuwa wanawasingizia,kumbe ni kweli tunaungwa kwenye huduma ambazo hatuzielewi na wanalamba salio!!,huu uhuni haukubariki
Watu wana ungwa kimya kimya mtu anakatwa 150,250 tatizo watu wanachukulia poa
Kumbe mamilion ya watu wanaungwa kilazima
Na kulipishwa hela hiyo
Kuna uhuni sana inafanyika na makampuni ya sim tanzania

Ova
 
Mkuu pole sana!! Iliwahi nitokea Mimi niliwawashia Moto nikawaambia waache ungese, daily walikua wanakata mdogo mdogo, ila baada ya kuliwasha me nko piece nao!

Kiukwel inaumiza sana!!
 
Back
Top Bottom