Juzi nimeingia mkenge, yaani hapa tumbo linawaka moto mda wote. Jamani juzi 22 August 2016 nimenunua kifurushi cha mwezi kwa njia ya M-pesa, elfu kumi nimepewa dakika 300. Niliongea max dak 30, jana nimeongea max dak 20, leo nimeongea na mtu hazijafika hata dakika 20 naletewa sms eti kifurushi kinakaribia kuisha dakika zipo chini ya 10. Natamani kufakufa wala sielewi, nahitaji faraja ya moyo wangu maana huu mtandao unanifilisi sana..........Sijui ibilisi gani aliniingia juzi hadi kujiunga!!!!!!, yaani halotel wananipaga dakika 1200+ na huwa sizimalizi kwa mwezi mzima. Huko nje nikimuona mtu ametaja voda moyo wangu unatenda dhambi maana namtukana sana kimoyo moyo tena matusi mazito mazito.........Kuna mitandao kama huu wa Voda haufai kuendelea kuwa nchini!!!!!!!