Vodacom Mpesa ni wezi.

Vodacom Mpesa ni wezi.

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,863
Mimi ni wakala wa Mpesa.

Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.

Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.

Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.

Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.

====_==================
Inaonekana kuna watu Hesabu za kutoa na kujumlisha zinawasumbua sana.

Ok!

Ni hivi kabla mteja kutoa
pesa salio lilikuwa Milioni
moja mia themanini na tatu
elifu na mia tisa i.e
1,183,900.

Baada ya mteja kutoa pesa,
Salio likapungua na kuwa
Milioni moja na mia
themanini na tau elifu i.e
1,183,000.

Ingepaswa iwe hivi:
Baada ya mteja kutoa pesa
ingepaswa salio langu
liongezeke kwa kiasi
alichotoa i.e 3500

Salio jipya lingekuwa
1,183,900+3500=1,187,400.
Baada ya mteja kutoa pesa:
Baada ya mteja kutoa pesa
salio langu jipya likawa ni
1,183,000

Ikiwa na maana kuwa
wamekata 900 ktk salio la
mwanzo + 3500 aliyotoa
mteja

NB.
Nilipokea sms kuwa mteja
ametoa 3500.
Nadhani nimeeleweka.

=======================~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Vija JF, topic closed.
Tatizo limekwisha, ilikuwa
hivi.

Mwanzo kabisa salio
lilikuwa ni 1,132,500.
Kuna mteja akatoa 47000,
Salio jipya likawa ni
1,183,900 badala ya
1,179,500. Ikiwa na maana
kuwa kuna ongezeko la
4400. Hili si kulitambua- Ni
rahisi kugungundua
pungufu kuliko nyongeza.
Hizo ni tabia za kibinadamu
tu.

Baada ya Mteja mwingine
kutoa 3500 nikaona kuna
pungufu ya 4400. Hatua ya
kwanza, niliwapigia
Vodacom customer care,
hawakuwa na jibu sahihi.
Nilipiga zaidi ya maramoja:
Hawakuwa na jibu sahihi.
Nashukuru baada ya
kuweka bandiko langu
hapa. Voda wanekuja,
tumewasiliana na kutrace
tatizo lilipo na kuondoa
wasiwasi.

Matokeo:
Inavyoonekana kuna mteja
alijarbu kutoa pesa kwangu
kiasi cha 4400. Pesa
haikutoka, ila kwangu
iliongezeka. Baada ya muda
pesa ilirudi kwake na
akaitoa kwa Wakala
mwingine.

Poleni sana kwa usumbufu
uliojitojeza, ila
mmeyasababisha wenyewe
na Kitengo chenu cha
Huduma kwa Wateja
kushindwa kunipa jibu
sahihi.

Asanteni sana.
Mingu ibarki Jamii Forum
 
Yaani customer services ya voda wanatia kichefuchefu.Bora tu tuhamie ...! Juzi nilihamisha salio kwa mtu, ikaingia kwengine.Nikapiga voda kuomba msaada, hawakutaka hata kunisikiliza! Wakabakia na kamsemo chao '..aksante sana kwa kuchagua vodacom..'nadhani wanabweteka na customer base walionayo! Ole wao, ipo siku..
 
Yaani customer services ya voda wanatia kichefuchefu.Bora tu tuhamie ...! Juzi nilihamisha salio kwa mtu, ikaingia kwengine.Nikapiga voda kuomba msaada, hawakutaka hata kunisikiliza! Wakabakia na kamsemo chao '..aksante sana kwakuchagua vodacom..'nadhani wanabweteka na customer base walionayo! Ole wao, ipo siku..

Kwetu-Mbagala

Wamenikera sana. Hawa jamaa ni wajinga sana, wametuona mapoyoyo.
 
Last edited by a moderator:
kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.

Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.
.
Kama sijaelewa kwa point hizi tu, mkuu unaweza kunifafanulia vizuri hapa...
 
Mi ni mhanga pia, waliniibia Sh. 5,000 basi mpaka leo siwaamini hata chembe, maana kwa njia waliotumia kufanikisha wizi wao, ipo siku watakula zaidi. Sasa natumia huduma hiyo pale kunapokuwa na ulazima tu wa kufanya hivyo na si kama awali niliichukulia kama sehemu nyingine pia ya kuhifadhi vijisenti.
 
Mimi ni wakala wa Mpesa.

Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.

Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.

Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.

Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.

Kidato cha nne? Au kuna tatizo mahali?:help:
 
Kama sijaelewa kwa point hizi tu, mkuu unaweza kunifafanulia vizuri hapa...

Ok!
Ni hivi kabla mteja kutoa pesa salio lilikuwa Milioni moja mia themanini na tatu elifu na mia tisa i.e 1,183,900.

Baada ya mteja kutoa pesa, Salio likapungua na kuwa Milioni moja na mia themanini na tau elifu i.e 1,183,000.

Ingepaswa iwe hivi:
Baada ya mteja kutoa pesa ingepaswa salio langu liongezeke kwa kiasi alichotoa i.e 3500
Salio jipya lingekuwa 1,183,900+3500=1,187,400.

Baada ya mteja kutoa pesa:
Baada ya mteja kutoa pesa salio langu jipya likawa ni 1,183,000
Ikiwa na maana kuwa wamekata 900 ktk salio la mwanzo + 3500 aliyotoa mteja

NB.
Nilipokea sms kuwa mteja ametoa 3500.

Nadhani nimeeleweka.
frema 120
 
Last edited by a moderator:
Haya mahesabu yako kiboko. Hiyo mpesa unauza mwenyewe ama wewe ndo tajiri? Manake kama wewe uko hivi sijui huyo anaesimamia biashara ana akili gani! Go home, you are drunk!
 
mbona mnakuwa na dharau kwa vitu msivyovijua?

Mkuu,
Watu wasichojua ni kua Mteja akitoa hela kwenye M-Pesa, basi kwa wakala salio linaongezeka. Maana ni sawa na Mteja anamuuzia wakala salio lake.

Sasa kwa kutokuelewa huko wanafikia kumshambulia mleta mada bure. Pole Mkuu Mzee.

Meanwhile umeadimika sana kule siasani kaka (Out of Topic & Joke)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Watu wasichojua ni kua Mteja akitoa hela kwenye M-Pesa, basi kwa wakala salio linaongezeka. Maana ni sawa na Mteja anamuuzia wakala salio lake.

Sasa kwa kutokuelewa huko wanafikia kumshambulia mleta mada bure. Pole Mkuu Mzee.

Meanwhile umeadimika sana kule siasani kaka (Out of Topic & Joke)

unajua watu hawataki kudadisi na kutaka kujua mambo..ndiyo maana wanaishia kutoa kejeli tu!!
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni wakala wa Mpesa.

Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.

Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.

Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.

Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.

Form 4 masalia...wakikufungulia kesi uthibitishe wizi huo utapona wewe,kati ya mia 9 na elf tatu 500 ipi ya kumtoa mwenzake.
 
Bora kukaa kimya kama hujui kitu. Ndo mana waswahl wasema ukitaka kujua upumbav wa mtu mwache aongee
 
Back
Top Bottom