Vodacom Mpesa ni wezi.

Vodacom Mpesa ni wezi.

Mimi ni wakala wa Mpesa.

Leo kuna mteja kaja kutoa pesa, kabla ya kutoa pesa salio lilikuwa ni 1,183,900.
Baada ya mteja kutoa 3500 salio likawa ni 1,183,000.

Hapo kuna pungufu ya 900+3500=4400.

Nimejarbu kuwapigia simu. Wamenijibu kuwa hawaoni tatizo lolote.

Acheni wizi. Nirudishieni pesa zangu.

====_==================
Inaonekana kuna watu Hesabu za kutoa na kujumlisha zinawasumbua sana.

Ok!

Ni hivi kabla mteja kutoa
pesa salio lilikuwa Milioni
moja mia themanini na tatu
elifu na mia tisa i.e
1,183,900.

Baada ya mteja kutoa pesa,
Salio likapungua na kuwa
Milioni moja na mia
themanini na tau elifu i.e
1,183,000.

Ingepaswa iwe hivi:
Baada ya mteja kutoa pesa
ingepaswa salio langu
liongezeke kwa kiasi
alichotoa i.e 3500

Salio jipya lingekuwa
1,183,900+3500=1,187,400.
Baada ya mteja kutoa pesa:
Baada ya mteja kutoa pesa
salio langu jipya likawa ni
1,183,000

Ikiwa na maana kuwa
wamekata 900 ktk salio la
mwanzo + 3500 aliyotoa
mteja

NB.
Nilipokea sms kuwa mteja
ametoa 3500.
Nadhani nimeeleweka.

Waambie wasome zaburi ya 49..
 
Mteja wake ndiye aliyetoa hicho kiasi; ili muamala ukamilike unahusisha watu wawili, mwenye kibanda cha mpesa ambaye ndo huyu anayelalamika na mteja wake ambaye alitoa hicho kiasi, kama mtoa mada anasema ukweli kuna tatizo ambalo halijulikani; lakini kwa ufahamu wangu inawezekana kabisa mtoa mada kuna kiasi alichokuwa anadaiwa. hii hutokea mara nyingi sana unakuta mteja anatoa hela halafu anakosea namba ya wakala badala ya kuingiza namba ya wakala alipo anajikuta anaingiza namba ya wakala mwingine, sasa aliyekosea akilalamika lazima hicho kiasi kivutwe kutoka kwa wakala ambako kimeingia kwa makosa kurudishwa kwa mteja aliyekosea. nadhani inawezekana kimetokea kitu kama hicho kwa mdau lakini si kweli kwamba Vodacom wamwibie kwa jinsi hiyo, kama ni kweli afuatilie maana system zinaonyesha kila kitu ikiwezekana wamprintie aangalie tatizo liko wapi asione kwamba ni hela ndogo sio ujinga kuuza mbuzi kwa kesi ya kuku kama unachotafuta ni haki.

Kwenye bluu, ukidaiwa wanakujulisha na unapo refund wanakujulisha huku shukurani za ushirikianao zikitolewa.
Kwenye nyekundu, hilo lisingemgusa Mzee, angehangaika nalo aliyekosea.
Kwenye kijani kula tano Masuke.
Mwisho, kwa nini utoe pesa kwenye muamala wenye mashaka?
 
Last edited by a moderator:

Kwenye nyekundu maana yangu ilikuwa ni kwamba kuna mteja mwingine some where ambaye nadhani alikosea badala ya kuingiza namba ya wakala ya alipokuwa yeye akaingiza namba ya mtoa mada kwa hiyo hela ilivyovutwa ikasababisha balaa kwa mtoa mada.
Muamala maana yake ni transaction, ni mchakato wa kutoa na kuweka hela na kwa maelezo ya mtoa mada transaction ilikamilika ndo maana hata yeye alipata message kwa hiyo muamala haukuwa na mashaka yoyote.
 
Wewe vipi? Huko some where huko, hata kama pesa ilikuja kwa mtoa mada kwa makosa kwa kawaida kiasi hicho huzuiliwa kwa saa zisizopungua 24. Haitumiki aidha kwa wakala ilipokosewa ama kwa mteja aliyekosea kwa kipindi chote mpaka kuwepo na mwafaka. Wote WATAPIGIWA simu ku indicate scenario hiyo na baada ya saa hizo 24 pesa itarudishwa kwa aliyekosea ilihali kwa huyu wakala zinakotoka akipewa message ya notification ikiwa na transaction ID number. Umenisoma jembe?
 
Vija JF, topic closed.

Tatizo limekwisha, ilikuwa hivi.

Mwanzo kabisa salio lilikuwa ni 1,132,500.
Kuna mteja akatoa 47000, Salio jipya likawa ni 1,183,900 badala ya 1,179,500. Ikiwa na maana kuwa kuna ongezeko la 4400. Hili si kulitambua- Ni rahisi kugungundua pungufu kuliko nyongeza. Hizo ni tabia za kibinadamu tu.

Baada ya Mteja mwingine kutoa 3500 nikaona kuna pungufu ya 4400. Hatua ya kwanza, niliwapigia Vodacom customer care, hawakuwa na jibu sahihi. Nilipiga zaidi ya maramoja: Hawakuwa na jibu sahihi.

Nashukuru baada ya kuweka bandiko langu hapa. Voda wanekuja, tumewasiliana na kutrace tatizo lilipo na kuondoa wasiwasi.

Matokeo:
Inavyoonekana kuna mteja alijarbu kutoa pesa kwangu kiasi cha 4400. Pesa haikutoka, ila kwangu iliongezeka. Baada ya muda pesa ilirudi kwake na akaitoa kwa Wakala mwingine.

Poleni sana kwa usumbufu uliojitojeza, ila mmeyasababisha wenyewe na Kitengo chenu cha Huduma kwa Wateja kushindwa kunipa jibu sahihi.

Asanteni sana.
Mingu ibarki Jamii Forum.
 
Hesabu ni janga la taifa.
Usikute huyu ni mtu kaajiliwa serikalini alafu ni ticha.chezea maths????
Tekinolojia pia ni janga.
 
Form 4 masalia...wakikufungulia kesi uthibitishe wizi huo utapona wewe,kati ya mia 9 na elf tatu 500 ipi ya kumtoa mwenzake.

Waerevu wamegundua kati yangu na wewe nani mwehu.

Jarbu kadri ya uwezo wako kuficha ujinga wako.
 
Hesabu ni janga la taifa.
Usikute huyu ni mtu kaajiliwa serikalini alafu ni ticha.chezea maths????
Tekinolojia pia ni janga.

Ficha Ujinga wako.

Hiyo hesabu imekosewa wapi¿
 
Wewe vipi? Huko some where huko, hata kama pesa ilikuja kwa mtoa mada kwa makosa kwa kawaida kiasi hicho huzuiliwa kwa saa zisizopungua 24. Haitumiki aidha kwa wakala ilipokosewa ama kwa mteja aliyekosea kwa kipindi chote mpaka kuwepo na mwafaka. Wote WATAPIGIWA simu ku indicate scenario hiyo na baada ya saa hizo 24 pesa itarudishwa kwa aliyekosea ilihali kwa huyu wakala zinakotoka akipewa message ya notification ikiwa na transaction ID number. Umenisoma jembe?

Werevu wamekuelewa, wajinga wachache bado wanahaha.

Pamoja kiongozi.
 
Mzee na Tindikali, kulingana na post #46 inaonyesha wazi kuwa mnapenda kukurupuka na kutoa lawama bila kufanya research exhaustively. Nampongeza sana Masuke kwa kuwa composed kwenye michango lakini nimfurahie Rogie na wengine wote kwa kupinga wazi lawama za mleta mada.
 
Mzee na Tindikali, kulingana na post #46 inaonyesha wazi kuwa mnapenda kukurupuka na kutoa lawama bila kufanya research exhaustively. Namponeza sana Masuke kwa kuwa composed kwenye michango lakini Rogie na wengine wote kwa kupinga wazi lawama za mleta mada.

Chizi Fureshi
Nafikiri umenielewa. Nimejarbu kuwasiliana Huduma kwa wateja ili wanipe jibu sahihi.

Nimewasiliana nao zaidi ya mara moja,
 
Last edited by a moderator:
Habari,ninachoamini ni kuwa pesa haiwezi kupotea kwenye M-PESA,lazima kuna mahali salio litajulikana lilipo.Pia kabla hatujaanza kusema tumeibiwa tujaribu kwanza kupata suluhisho,Vodacom haiwezi kuiba salio na kama inafanya hivyo basi wateja wangeshaacha kutumia mtandao huo.

Rogie
Hebu tueleze mahala pa kupatia ufumbuzi zaidi ya kupitia kitengo cha "Huduma kwa Wateja"???.

Hilo nimefanya.
 
Last edited by a moderator:
Rogie
Hebu tueleze mahala pa kupatia ufumbuzi zaidi ya kupitia kitengo cha "Huduma kwa Wateja"???.

Hilo nimefanya.
piga 15366, ingawa kuna makato, tena ukitumia line yako unayofanyia biashara ni rahisi zaidi kusaidiwa.
 
Mzee,
Nisaidie tafadhali ingawa wewe ni wakala tu. Hivi nahitaji kutimiza vigezo gani lil nipewe uwakala. Natamani kufanya kazi hiyo na Vodacom.
 
piga 15366, ingawa kuna makato, tena ukitumia line yako unayofanyia biashara ni rahisi zaidi kusaidiwa.

Masuke
Nilifanya hivyo zaidi ya mara moja ila sikupata jibu sahihi.
 
Last edited by a moderator:
Mzee,
Nisaidie tafadhali ingawa wewe ni wakala tu. Hivi nahitaji kutimiza vigezo gani lil nipewe uwakala. Natamani kufanya kazi hiyo na Vodacom.

Kwa kuongezea nami naomc kueleweshwa namna faida inavyopatikana kwa uwakala wa mpesa, tigo pesa ama airtel money maana ninaplan kua wakala siku za usoni.
 
Yaani customer services ya voda wanatia kichefuchefu.Bora tu tuhamie ...! Juzi nilihamisha salio kwa mtu, ikaingia kwengine.Nikapiga voda kuomba msaada, hawakutaka hata kunisikiliza! Wakabakia na kamsemo chao '..aksante sana kwa kuchagua vodacom..'nadhani wanabweteka na customer base walionayo! Ole wao, ipo siku..
mshahara wa 280000 wanaolipwa hao customer care bila benefit zozote unategemea watatoa huduma gani hapo
 
Una uhakika na hili mkuu?? Unaweza kusimama Mahakamani??

Nina uhakika sana tu mkuu kwani nimejaribu sana kuandika ile miamala nikaona kila mwezi napoteza hela nimejaribu kufuatilia lakini wapi.
 
Back
Top Bottom