Raia Mtata
JF-Expert Member
- Feb 4, 2017
- 334
- 634
- Thread starter
-
- #61
INATEGEMEA UPO ENEO GANI MKUU, MIMI ENEO NILIPO INTERNET YA HALOTEL INA SPEED KULIKO YA VODACOM ILA UMEME UKIKATIKA TU NA INTERNET YA HALOTEL INAKATIKA.
Mkuu hivi bado mpaka leo unatumia vodacom?, vodacom ilikuwa zamani skuiz haipo, tumia ttcl, tigo na halotel ndo mitandao yenye viwango tz ya leo.
Hao wajuba nishaachana nao mda
Na uliweza kuongea na mtoa huduma?
Hizo zitakua za hao hao customers care....wana wahuni kinoma
OLE WAKO UKOPE PESA SONGESHA [emoji317]
Duh! Kumbe ni kweli? Hili tatizo la kulazimishwa mkopo nimelisikia hapa kitaa muda huu mtu akilalamika 🤣🤣🤣🤣🤣😆😆😆😆😆
vodacom mtuambie mmekwama wapi?
Hamia Zantel mkuu. Mimi siku hizi Voda naitumia kwa M-PESA tu. Bundle zao za internet ni majanga. Unaweza kununua Gb moja baada ya nusu saa unaambiwa kifurushi kimeisha na wala hujadownload hata video yoyote labda umeperuzi website mbili tatu tu. Mhh!
I think you mean stupid
Halotel ina speed kubwa sana! Pengine upo sehemu za Madaba vinginevyo halotel is super!
Milijua ni simu yangu aise..kwenye simu yangu nimefunga apps karibu zooote zimebaki nne tu..lakini hizo mb zinavyomwagika hadi huruma[emoji3064][emoji3064]
Bora mihamie Halotel au Zantel.
@ Vodacom Tanzania mje mjibu tubum huku[emoji3064][emoji3064]
Internet yao ni majanga. Jaribu Zantel uone
Hii nakupongeza alafu wanakuwekea sauti na nyimbo kwenye kompya record hadi unakata tamaa .kingine ukiweka vocha ya kukwangua wanaifyeka alafu unaambiwa eti ulikuwa unadawa.Na ukipiga huduma wa wateja wale wadada wanaonekana wengi hawana experience au wengi wao hawajui kazi zao, mtu unampigia simu anapokea anakwambia wewe huna mkopo, wakati yeye yupo kwenye system na anaona, nikampigia mwengine hapo hapo customer care huyu anajibu kirahisi kabisa eti wewe umekopa mwenyewe nikamwambia ningekuwa nimekopa ningepiga simu hapa ofisini kwenu? They are so Poor
Voda ujinga walioufanya nikwenye vifurushi vya maongezi voda to voda dakika unapewa mpaka zingine huwezi maliza, ila voda tomitandao mingine, ndio changamoto ni ghali sana
Voda mambo gani haya,
Nanunua kifurushi cha social bundle cha mwezi mzima, MB bado zipo za kumwaga lakini bundle halifanyi kazi ( siwezi kulitumia, lipo tu) ila nikijiunga bundle jipya inakubali ila hili la mwezi ni kama maua tu siwezi tumia.
Unachosema ni kweli, mimi mwenye nipo mbeya maeneo ya mjini unapata 4G ila ukiwa nyumbani hamnakitu, hatamimi natumia voda hasakwenye internet
Hii nakupongeza alafu wanakuwekea sauti na nyimbo kwenye kompya record hadi unakata tamaa .kingine ukiweka vocha ya kukwangua wanaifyeka alafu unaambiwa eti ulikuwa unadawa.
Ni kweli sasa kama GB inaisha kwa masaa 2 badala ya wiki sasa kwa wiki nitatumia GB ngapiBora huyo kobe kwakuwa GB zetu zitakuwa salama.
Hapo umesoma tu SMS what's appHamia Zantel mkuu. Mimi siku hizi Voda naitumia kwa M-PESA tu. Bundle zao za internet ni majanga. Unaweza kununua Gb moja baada ya nusu saa unaambiwa kifurushi kimeisha na wala hujadownload hata video yoyote labda umeperuzi website mbili tatu tu. Mhh!
[emoji23][emoji23] nacheka kama vizuri, Mimi ilitokea nikajiuliza mbona huwa sijiungi na takataka zenu eti labda mtu mwingine alitumia mambo ya ajabu haya nishaacha mambo ya kukwangua vyocha upuuzi mwingi sana.Hii nakupongeza alafu wanakuwekea sauti na nyimbo kwenye kompya record hadi unakata tamaa .kingine ukiweka vocha ya kukwangua wanaifyeka alafu unaambiwa eti ulikuwa unadawa.
Mitandao ya simu yenyewe wanaweza kukuunganisha na huduma fulani kwa kutumia system yao bila wewe kujua au bila hata wao wenyewe kujuaKwa akili ya kawaida simu haiwezi kujiunga kwenye huduma yenyewe..
Pengine umejiunga bila kukusudi/bila kujua... Mfano kuna code ukiweka zilizoko kwenye matangazo inajiunga direct. Au
Mtu katumia simu yako akajiunga kwa maksudi au bahati mbaya