Vodacom mmesababisha ndugu yangu kufariki, nawaletea maiti ofisini

UKAWAA

JF-Expert Member
Apr 18, 2014
216
85
Naandika haya kwa uchungu dhidi ya huu mtandao wa vodacom.Tarehe 25/4 saa 7 na robo mchana nilipigiwa simu dada kazidiwa tena kutoka kwa majirani, niliwaomba watafute gari wamkimbize hospital mimi niombe ruhusu kibaruani nitawakuta huko.

Kwenye akaunti yangu ya mpesa nilikuwa nina 416,000 tena niliiweka mda mfupi tu baada ya kupewa haki yangu ya mwezi na boss hivyo ikanipasa nimrushie 400,000dada kwenye no yake ili walipie usafili na matibabu,nilipotuma ile hela vodacom wakanitumia ujumbe kuwa "Samahani, muhamala wako haukukamilika kwasababu za kiufundi"japo hela kwenye akaunti yangu haikuonekana tena wala nilikotuma hakufika.

Baada ya masaa kadhaa wahospital wananipigia wameshafika hela haijafika ikabidi nipige voda huduma kwa wateja nilijibiwa kuna tatizo la mtandao mafundi wanashughulikia hela itafika nilikotuma nisiwe na wasiwasi, ikabidi niwaambie wale wa hospital kule nilichojibiwa ikabidi wajipapase wao wamlipe wa gari maana mimi sikuwa na hata senti tena,Nashukuru hospital alipokelewa vyema na kuanza matibabu japo mchana wa leo Mungu kamuita.

Tangu tarehe 25/4 hadi leo tarehe 3/5/2017 hiyo hela haikufika sehemu husika wala kwenye akaunti yangu haikurudishwa licha ya juhudi kubwa niliyoifanya ya kuwapigia kila siku bila mafanikio zaidi ya kuniahidi niwe mvumilivu.Leo asubuhi nilipopiga tena wamenitumia meseji hii"Tumepokea ombi lako lenye namba A7-TTEB-RF7L4 . Tutakujulisha punde litakapotatuliwa kabla ya 11-MAY-17 . Piga *106# kuhakiki usajili wa laini yako."

Kusudio la hela ilikuwa kumsaidia dada lakini VODACOM mkaamua kuikalia,sawa sina la kuwafanya basi naiomba mnirudishie itumike kwenye taratibu za kumpumzisha au niwaleteeni maiti ofisini mkamzike wenyewe?.

NOTE:
Baadhi ya maongezi na wahudumu nimeyaweka kama sehemu ya ushahidi.

MREJESHO:
Kwanza nawashukuru uongozi wa JamiiForums kwa kuanzisha hili jukwaa limesaidia wanyonge tumepata pakuongelea.

Pili nawashukuru wachangiaji mlionipa pole, kunitia moyo na wengine kunipa miongozo ya hatua za kuchukua. Dhamira yangu haikuwa kushitaki ili nilipwe ila uongozi wa VODACOM usikie UMUNGU MTU walio nao wafanyakazi wao na kwa kuchukulia mambo kirahisi.

Tatu niwashukuru UONGOZI WA VODACOM kwa kuzungumza na mimi na kudhibitisha malalamiko yangu na leo tar 4/5 nadhibitisha kurudishiwa pesa yangu kama walivyoniahidi.
Hela itasaidia kukamilisha mahitaji na taratibu zilizo salia za kumuandalia dada nyumba yake ya milele makaburi ya kibamba leo.

Asante.
 

Attachments

  • VODACOM 2.amr
    366.3 KB · Views: 55
  • VODACOM day 6(a).amr
    334.5 KB · Views: 45
  • VODACOM day 6(b).amr
    153.3 KB · Views: 57
Nimejisikia vibaya sana ukizingatia waliofanya ushenzi huo hawajaitolea jasho hiyo pesa, wa husika kama mnapita humu oneni machungu mnayo sababisha kwa tamaa zenu za kisen*e.
Muwe mnauliza basi hao wanaotuma pesa kama anatumia kwa wagonjwa kama huyu muwe mnakausha ila kama wanawatumia michepuko yao mnaweza kuwapiga mtapata na baraka kwa kuzuia uzinzi lakini sio kwa wenye matatizo kama. mleta mada mtapata laana.
 
Lakini ndg katika maelezo yako naona kama voda hawahusiki na kifo cha mpendwa wetu kwani ingeleta maana kama hospitali wangekugimea katakata kumpokea mgonjwa na kumtibia. Matatizo ya mitandao yapo wengi tumeyapitia kwani ni macomputer ndo hufanya kazi ss inapotokea tatizo ndipo wafanyakazi huanza kuhangaika kulitatua.

Lakini nakupa pole sana ww na familia yote kwa kuondokewa na ndg yetu. Mungu awatie nguvu na kuwafanya imara zaidi ktk kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana...wamekua hivyo tangu waanze kuuza hizo his a zao sijui ndo kila MTU anachukua chake
 
Pole sana kwa msiba. Sababu yako ni dhaifu sana. You did it at your own risk.
 
Back
Top Bottom