Vodacom kuwaburudisha wabunge ijumaa hii!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom kuwaburudisha wabunge ijumaa hii!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsunza, Jul 21, 2011.

 1. N

  Nsunza Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 21, 2008
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NDUGU ZANGU,
  HILI SUALA MNALIONAJE MAANA NAONA SASA “LOBBYING” INACHUKUA PICHA TOFAUTI KABISA KATIKA NCHI YETU. GHAFLA INAYO ANDALIWA NA VODACOM KUHUDHURIWA NA WAZIRI MKUU AMBAYE NAFASI YAKE KATIKA SERIKALI NA BUNGE INAELEWEKA, SPIKA WA BUNGE, MAWAZIRI NA WABUNGE WENGINE…..SASA WATAWEZAJE KUJADILI MSWADA WOWOTE WENYE LENGO LA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAWASILIANO?? HILI SWALA LAZIMA TUPIGANE NALO IPASAVYO!!!

  BOFYA HAPA: MICHUZI: VODACOM KUWABURUDI​SHA WABUNGE IJUMAA HII
   
 2. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Hii ni RUSHWA! Nani kasema Ofisi ya Bunge haina pesa ya kuwaburudisha wabunge wake kama ikitaka. Na kwenye bajeti ya Ofisi ya Bunge pesa hizo zipo. Yaani hapo kwa kifupi hawa wazungu wanatafuta jinsi ya kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi. Lobbying at its best!!
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Waache wale maisha, kama unaona donge na wewe gombea ubunge MANEROMANGO
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Baada ya 'upitishwaji' wa bajeti kwa njia ya 'Ki-jairo' wabunge na hasa Spika wanatakiwa wawe makini. I see no reason kwa sasa hivi Vodacom kuwapa chakula wabunge wenye posho kila kona ili hali robo tatu wa watanzania wanakabiliwa na njaa! Kama wizara itachangisha bilioni na ushee kupitisha bajeti yake Vodacom wanatafuta nini? Na nani anaweza kusema kwa nini makampuni ya simu mpaka sasa hivi hayajawa registered kwenye soko la hisa la Dar es Salaam?

  Tujukumbushe, mara baada ya saga ya Nyamongo, Ubalozi wa Canada uliandaa chakula "maalum" kwa wabunge Dodoma kwa kisingizio cha kusheherekea siku ya Canada. Ubalozi huo uli-fast forward maana siku ya Canada ilikuwa bado haijafika. Hadi leo sio Bunge wala serikali imetangaza uchunguzi wa mauaji ya watu wa Nyamongo na maiti kutupwa barabarani! Mbaya zaidi hata pale mbunge (Mh.Lissu) alipojaribu kuuliza swali Spika Makinda alijipa kazi ya USEMAJI wa serikali na kujibu kuwa kesi iko mahakani kwa hiyo swala hilo haliwezi kuongelewa! Maajabu hakuna hakuna mahakama yeyote ndani ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ilikuwa na kesi ya Nyamongo wakati huo!

  No such thing as free lunch. Wabunge wote (nasisitiza WOOTE) wanatakiwa watudhihirishie sisi wapiga kura kuwa miswaada yenye utata, ububu wa bunge kusimamia sheria walizotunga hauna elements za MA-LOBBYISTS.

  Jairo ni tone ndani ya bahari. Bunge limeoza!
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wameshajuan moto so wanatafuta njia ya kuuzia watu wasihoji bei kubwa za mawasiliano yao.Anyway yetu macho tuone mwelekeo ukoje .
   
 6. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kuna FOUNDATION ya Mama Maajar imezinduliwa juzi. Lengo lake ni kuhahakisha kwamba watoto wote wa shule za sekondari na shule za msingi wanakaa kwenye madawati na si chini ndani ya miaka mitatu. Ukiuliza wanahitaji pesa kiasi gani kutimiza lengo hilo, unaambiwa ni shs. 3 billions.

  Kumbe kuna Wizara inatumia zaidi ya shs. 1billion ku-facilitate bajeti yao ya magumashi ipite. Hapo ndipo unaona kwamba nchi imeoza, maslafu binafsi yamewekwa mbele na hakuna uwajibikaji kabisa! Yaani serikali inashindwa kupata shs 3billions za madawati(!?) Kumbuka Ofisi ya Rais imetengewa shs. 135 billions kwa mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya ''Matumizi ya Kitaifa''. Hii haina BREAKDOWN!! Basi JK angetafuta sifa kwa kutoa walau 1 billion kutoka kwenye fungu hilo ''kusaidia'' hiyo NGO inayochangisha pesa za madawati!
   
 7. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kusema kweli something is wrong with our politician, yaani nchi iko kwenye giza wananchi ni kama wako kwenye matanga, wao kweli wanaona fahali kwenda kujimwaga? Huyu spika amekubali kweli kitu kama hiki kufanyika kwa wakati kama huu???
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Waandishi wa habari tupeni picha za wabunge na viongozi wengine wataoudhuria huu mlo wa Vodacome. We want to know who & how our politicians are betraying us! Hii ni kama saga ya Rupert Murdoch na wanasiasa wa Uingereza!
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  vodacom = ROSTAM AZIZ unategemea nini?
   
Loading...