Vocha Zinatengenezwaje?

Andy Kawa

Senior Member
Feb 21, 2014
124
225
Nafikiri taarifa kuhusu algorithm sahihi inayotumika na kampuni husika haiwezi kupatikana wazi katika mitandao.Bila kujali nitatoa mawazo niliyonayo juu ya topic hii.


Algorithms za Kutengeneza Vocha

Random number generator yoyote nzuri inaweza ikafanya kazi hii, lakini kama wanajaribu kutumia sayansi zaidi kuhusu hili, watatumia algorithm inayozalisha namba zenye certain minimum Hamming distance.

Hamming distance katikati ya maneno mawili yenye urefu sawa ni idadi ya herufi(characters) zinazohitaji kubadilishwa kufanya neno lifanane sawa na lingine.

Mfano:

Hamming distance katikati ya
  • FISH na DISH ni 1
  • MUMBLE na BUBBLE ni 2
Kuna matukio mbalimbali ambapo ukibadilisha herufi au tarakimu moja kwenye code inaweza kupelekea kwenye matokeo yasiyohitajika. Applications za aina hiyo zinafanyia kazi Codes Zinazogundua Error(Error Detecting Codes) ili hata codes isiyosahihi ikiingizwa, mfumo angalau unaweza kuhisi hiyo Error na kuibeba katika tabia ya utulivu (labda kwa kumuomba mtumiaji kurudia upya kuingiza code).

Algorithms za kuzalisha hizo Codes za kugundua Error zinazalisha mpya, codes ndefu kwa kila code original, na minimum hamming distance flani.

Pamoja na yote hayo hii haiwezi kuzifanya codes salama kutokana na shambulizi la bruteforce lakini angalau inahakikisha ukibadilisha tarakimu moja au mbili haizalishi code sahihi. Aidha ni rahisi kuzuia shambulizi la bruteforce kwa kuzuia idadi ya marudio katika kuingiza codes husika.

Unalazaidi kuongezea? Comment hapo chini na wengine wapate kunufaika! Pia kama umeinjoi taarifa hii, SHARE na wenzako wapate kujifunza.

Karibu HackerHub | Forum Board kuendelea kujifunza zaidi mada za Teknolojia hii na utandawazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom