Programmers Only: Application ya Kuingiza neno moja na kupata maneno mengine

Afisa Mteule Drj 2

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,587
3,936
Application hii ambayo nimeitengeneza ikiwa ni sehemu ya kujifunza Computer programming ,inawezesha kuingiza neno moja halafu,herufi za hilo neno zinaweza kutumiwa kuunda maneno mengine.Mfano ukiingiza neno cat herufi 3 za neno cat zitatumiwa kuunda maneno mengine.Hesabu inaonyesha neno lenye herufi tatu linaweza kuunda maneno 6 tofauti

mfano neno cat,herufi zake zinaweza kuzalisha maneno yafuatayo
cat
tca
atc
tac
act
cta

Ifuatayo ni idadi ya maneno inayoweza kuzalishwa kutokana na idadi ya herufi katika neno

Neno lenye herufi 2 linaweza kuzalisha maneno 2
Neno lenye herufi 3 linaweza kuzalisha maneno 6
Neno lenye herufi 4 linaweza kuzalisha maneno 24
Neno lenye herufi 5 linaweza kuzalisha maneno 120
Neno lenye herufi 6 linaweza kuzalisha maneno 720
Neno lenye herufi 7 linaweza kuzalisha maneno 5040
Neno lenye herufi 8 linaweza kuzalisha maneno 40320
Neno lenye herufi 9 linaweza kuzalisha maneno 362880
Neno lenye herufi 10 linaweza kuzalisha maneno 3628800

Application hii haifanyi kazi na maneno tu peke yake bali hata na namba mfano namba zenye tarakimu tatu zinaweza kutumika kutengeneza namba nyingine,mfano namba 345 tarakimu zake zinaweza kutengeneza namba zifuatazo.

345
534
453
543
435
354

Apllication hii inaweza kuprocess namba zenye tarakimu kuanzia 1 mpaka 10 na maneno yenye herufi 1 mpaka 10

Application hii mfano ukiingiza namba kama 0754901234(namba ya simu) inakupa namba zote zinazoundwa na hizo tarakimu mfano

0754904132
0754901423
0754901344

kwa kuwa 0754901234 ina tarakimu 10 ina maana namba zinazoweza kuzalishwa ni 3,628,800
matapeli wanaotuma meseji kwa watu kwamba "ile hela itume kwenye namba hii" watakuwa wananielewa kuhusu utajiri huu wa namba

Application hii inaweza kuzitumia tarakimu za kwenye namba za vocha kutengeneza namba nyingine zenye tarakimu kama za kwenye vocha

application hii inaweza kutumika kugeuza maneno hata yasieleweke mfano neno tanzania lina herufi 8,hizo herufi nane zinaweza kutengeneza maneno mengine mfano

tanzania
atinanza
atinazan
aznanati

Application hii pia inaweza kutumika kutengeneza password nyingi zenye urefu wa harufi kadhaa

Haya twende kazi

Matokeo ya neno dar lenye herufi tatu

dar3L.jpg



Matokeo ya neno Rais lenye herufi nne
Rais5L.jpg


Matokeo ya neno boom lenye herufi nne
boom4L.jpg


Matokeo ya neno ma**** lenye herufi sita
Malaya6L.jpg


Matokeo ya neno tanzania lenye herufi nane
tanzania7L.jpg


Matokeo ya neno computer lenye herufi nane
microsoft9L.jpg



Matokeo ya namba 634563 yenye tarakimu sita
6DN.jpg




Matokeo ya namba 0753810022 yenye tarakimu Kumi
10DN.jpg
 
Application hii ambayo nimeitengeneza ikiwa ni sehemu ya kujifunza Computer programming ,inawezesha kuingiza neno moja halafu,herufi za hilo neno zinaweza kutumiwa kuunda maneno mengine.Mfano ukiingiza neno cat herufi 3 za neno cat zitatumiwa kuunda maneno mengine.Hesabu inaonyesha neno lenye herufi tatu linaweza kuunda maneno 6 tofauti...
Mwanzo mzuri mkuu big up. Kukuongezea tu mawazo unaweza kuilink kwa nfano na database yenye maneno ya kiswahili au kiingereza ili ikitoa result iyoe maneno yenye kufahamika kilugha.

Vitu vingine sitapenda kukwambia nahofia nisije kukukatisha tamaa ukaona programming ngumu. Keep it up
 
Mwanzo mzuri mkuu big up. Kukuongezea tu mawazo unaweza kuilink kwa nfano na database yenye maneno ya kiswahili au kiingereza ili ikitoa result iyoe maneno yenye kufahamika kilugha. Vitu vingine sitapenda kukwambia nahofia nisije kukukatisha tamaa ukaona programming ngumu. Keep it up
Hapana mkuu wewe mwaga madini,hiyo idea ya database nimeikubali
 
Hapana mkuu wewe mwaga madini,hiyo idea ya database nimeikubali
Nashindwa kwenda mbali maana sijajua kama language nyingine umeshapitia ambazo unaweza kuintegrate na VB kama vile mySQL etc. Kwa sababu app yako inahusu zaidi number na maneno jaribu kutengeneza simple games kama vile sudoku au word scrambles.

Umenikumbusha mbali sana zaidi ya miaka 13 wakati huo tunafundishwa VBA. Yaani mwanzo mwisho ni kuandika code tu. Afadhali sasa hivi framework ya .Net imewarahisishia mambo. Kichwa kikitulia ntajaribu kukupa idea kulingana na level uliyofikia.

Kwa sasa hebu fanya kupitia vbforums.com humo utatoka na madini mengi sana.
 
Inatumia factorial method because Ni permutation and permutation uses factorial notation in the recursive function
 
Mwanzo mzuri mkuu big up. Kukuongezea tu mawazo unaweza kuilink kwa nfano na database yenye maneno ya kiswahili au kiingereza ili ikitoa result iyoe maneno yenye kufahamika kilugha.

Vitu vingine sitapenda kukwambia nahofia nisije kukukatisha tamaa ukaona programming ngumu. Keep it up
Hivi hapa unamaanisha maneno mfano ya kiswahili au kingereza yanayoshare herufi
Mfano
Mali na Lima
Ashura na Arusha
Item na mtei

Huu ni mfano tu najaribu kuona kama nimeipata point yako.Yaani mfano likichukuliwa Neno la kiswahili kwente database,application itoe maneno mengine tuseme ya kiswahili yanayoundwa na herufi za hilo neno la kiswahili .Katika orodha ya hayo maneno tuangalie ni neno lipi linalotumika kwenye lugha yetu ya kiswahili.Sijui ndio hivi unamaanisha mkuu
 
Back
Top Bottom