Viwanja vya Vijiji!!

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Ningependa kujua utaratibu wa uuzaji wa viwanja kupitia vijiji.
Unafanywa vipi?ni jinsi gani ya kuhakiki Mwenye kiti wa vijiji?
Na ni njia zipi sahihi?kusije kukawa na watu wanafanya utapeli!
 
Ningependa kujua utaratibu wa uuzaji wa viwanja kupitia vijiji.
Unafanywa vipi?ni jinsi gani ya kuhakiki Mwenye kiti wa vijiji?
Na ni njia zipi sahihi?kusije kukawa na watu wanafanya utapeli!

Mkuu nenda huko kijijini utapata majibu safi. Hapa jamvini utapewa majibu ya vijiji-mji ( mfano Vigwaza ni kijiji au kijiji-mji?) Mi kijijini kwetu unaomba kiwanja ktk kamati ya ardhi ya kijiji, wao wanakupa siku ya kwenda kukupimia, mwaka juzi tulikuwa tunalipia Tsh 2000/ tu. Kiwanja hicho unakatiwa ktk shamba la mtu na hakuna fidia kwa mwenye shamba. baada ya miaka mitatu kama hujaendeleza unapokonywa na anapewa mwingine,na buku mbili yako hairudi.

Kuingiza maji ya bomba ni Tsh 1500/ na unalipia bill ya jumla kwa mwaka mzima Tsh 2400/.
Kwa vyo vyote majibu yatatofautiana toka kijiji kimoja na kingine. Kuna kijiji kimoja huko kwetu kama unataka kujenga,basi unachagua mahali unafyeka pori na kuanzisha mji basi.
 
Back
Top Bottom