Viwanja vinauzwa Ilala (Kipawa Mpya) bei milion 6 - vimepimwa

Kazakuku

JF-Expert Member
Jun 6, 2011
354
110
Habari njema kwa watanzania,viwanja vinauzwa maeneo ya kipawa mpya mbele kidogo ya kigogo fresh waliko hamishiwa watu waliokuwa wnaishi kipawa na kigilagila,vimepimwa. Bei hadi milioni 6,kwa wale wanaohitaji tuwasiliane kupitia namba hii.
 
ukubwa ni upi?
ukisema vimepimwa,na nani?
vina hati?
ya wizara ya ardhi au serikali ya mitaa???????
 
ukubwa vya aina nyigi,vimepimwa na wizara na vina hati mkuu,ni viwanja vilivyotolewa na serikali kwa watu waliohamishwa toka kipawa na kigilagila.
 
kipawa mpya kama unaenda chanika.yaani baada ya kupita kigogo fresh
 
kipawa mpya ukitokea wapi?
ukitoka kariakoo unapita barabara zipi?
 
ukitokea kaliako unapita nyerere road,unapita gongo la mboto,pugu mpaka unafika kinyamwezi mbele yake kigogo flesh na mwisho ndo unafika kipawa mpya.
 
Ebu kuwa muwazi ndg, umeulizwa vina ukubwa gani ukasema ni vingi... ebu taja hivyo vingi na size yake, taja size ya kiwanja na bei yake, halafu tuambie wewe ni kama nani kwenye hivyo viwanja?
Dalali?
Mmiliki?
Mjomba wa mwenye kiwanja?
au nani?
 
kama unatokea kariakoo unapita nyerere road,unapanda magari ya chanika...hivyo utapita uwanja wa ndege,banana,gongo la mboto,pugu,kigogo fresh,kinyamwezi kituo kiachofuata ndo kipawa mpya.
 
mi ni rafiki na kama dalali wa wenye viwanja na ni mkazi wa huku thus why nikaamua ku post humu.
 
hufiki chanika,chanika inakua bado ni mbali...vipo wewe tu hapo.
 
Ni vema kuwa waangalifu, kuna malumbano makubwa sana eneo lile, kt ya wahamiaji toka Kipawa na wenyeji waliokutwa pale. Ni sehemu nzuri na nimeshawahi kufika maeneo yale, matapeli wanaweza kuanzia huko huko wizarani na siku ya siku ukauziwa kiwanja hewa, kwa nini viwe vingi kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom