Viwango vya TBS kwenye ukubwa wa matofali

Mapango ya Amboni

Senior Member
Apr 12, 2013
105
109
Wakuu niko katika mchakato wa biashara ya matofali ila ningependa kujua usahihi wa vipimo vinavyotakiwa katika matofali yasiyo kuwa na matundu (solid blocks) na kwa yale yenye matundu (hollow blocks).

Watengenezaji mbali mbali na wanunuzi wamekuwa wakisema tu "Tofali za nchi 5, 6, au 4. Lakini vipimo hivi nadhani ni unene tu (width au thickness) wa tofali.

Je kwenye kimo (height) na urefu (length) vinatakiwa viweje kwa size hizo. Niliwahi kuona waraka wa TBS wenye standard ya TZS 283, lakini vipimo nilivyokuta humo havina uhusiano wowote na tofali nizionazo mtaani au kwa wajenzi mbali mbali.

Kwa mfano kuna kipimo cha 300 x 150 x 200 na 300 x 75 x 200 na pia 600 x 200 x 200 ambavyo vyote viko katika milimita (mm), ambapo kwa baadhi ya wauzaji nimeona vipimo vya 5" x 9" x 18" na 6" x 9" x 18" na pia 4" x 9" x 18" katika vipimo vya (inch)..

Ukiangalia vipimo hivyo kuna utofauti mkubwa tu hasa kwenye urefu.

Je TBS ina waraka wowote mpya tofauti na huo ambao unaonyesha vipimo vitakiwavyo?

Kuna adhabu yoyote anayoweza kupewa mtengenezaji matofali asiyefuata vipimo sahihi vilivyowekwa?

Ni muhimu kujua hili ili nisiingie gharama za kubadilisha kalibu (moulds) au mashine.

Msaada wenu ni muhimu. Asanteni.
 
Duh! Angalau na mie nimeambulia vipimo. Labda jaribu kwa hawa wakala wa vipimo (WMA) wanaweza kukupatia.
 
Mi nadhani watakua wanahusika na ubora wa bidhaa tu, kuhusu size sidhani
 
Back
Top Bottom