Viwango hafifu vya timu za taifa za Tanzania kwenye michuano ya CECAFA

Maroon4

Member
Oct 4, 2007
15
13
Wana Jamii,

Mimi Kama mdau wa michezo hususani mpira wa miguu nimekua nikifuatilia kwa ukaribu michuano ya CECAFA inayoendelea hapa jijini Dar es Salaam. Ila nimesikitishwa sana na viwango duni vya team za Tanzania Bara na Zanzibar Heroes. Swali linakuja, nani alaumiwe? Je TFF na ZFA zimeonyesha nia ya dhati ya kuendeleza soka la nchi hii? Je kuna haja ya kuendelea na wakongwe ambao wameshindwa kuiletea mafanikio yoyote nchi hii katika michezo huku tukiwa tunahubiriwa ndoto hizi za Abunuwasi za Kwenda kucheza kumbe la dunia Brazil 2014? Je si wakati muafaka wa kuachana na kundi hili na kujikita zaidi kwenye soka la vijana na pengine tuwe na ndoto za kushiriki michuano ya kimataifa baada ya miaka kumi hivi pale ambapo vijana hawa watakua wameshapevuka na pengine tuwe katika viwango vya timu Kama Ghana? Great Thinkers, what's your opinion on what needs to be done to bring this 50 year old nation sports status to its DESERVED levels?
 
Chanzo cha matokeo mabaya ya timu za taifa ni maandalizi hafifu. Kwa kiwango cha soka cha tz timu inatakiwa ikae kambini si chini ya siku 14. Pia inatakiwa mechi za majaribio na timu kubwa kabla ya mashindano. kwa ufupi TFF wamechoka hawana jipya wala hawana upeo wa kuona mbali na ubunifu. Fedha wanazopata hawazitumii kwa vipaumbele. wasilaumiwe makocha wala wachezaji tatizo ni TFF.
 
Tatizo ni kubwa zaidi ya uwezo wa TFF,serikali ndio ya kulaumiwa kwani si katika soka tu ni katika michezo yote.Serikali haina dira ya michezo ya muda mrefu wala mfupi.Tutakuwa wasindikizaji wa wenzetu kwenye michezo yote labda tubadilike.
 
Back
Top Bottom