Viwanda vya Scania na Valmet Kibaha!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanda vya Scania na Valmet Kibaha!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Jul 14, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,779
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..najua kuna madogo wengi sana hapa wa miaka ya 90.

  ..hawa watashangaa kusikia kwamba Tanzania kulikuwa na viwanda vya ku-assemble malori ya Scania na matrekta ya Valmet.

  ..viwanda hivyo vilikuwepo Kibaha mkoa wa Pwani.

  ..sijui viwanda hivyo vina hali gani sasa hivi ukizingatia zoezi la UBINAFSISHAJI.

  ..kiwanda kama VALMET kingekuwa na umuhimu sana ktk mpango wetu wa KILIMO KWANZA.

  ..moderator naomba uiache hoja hii hapa ili kuipa nafasi ipate michango mingi zaidi.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM wanajua vyema na serikali yao .Watu waligawana nadhani na kufunga miradi ile
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hata madogo wa 90s wanayaona magofu ya hivyo viwanda.
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni serikali yetu, kuna viwanda vingi wakati wa ubinafishaji walikuwa wanagawa vipuli kwa wawekezaji badala ya kuviboresha, cha ajabu wawekezaji ni viongozi hao hao, which is a crazy business for our country.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,567
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Umesahau LAND ROVER na LEY LAND Mbagala sikuhizi nasikia ni kiwanda cha CEMENT.
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ccm huijui wewe,wao wanaua nguvu ya wananchi na kuwaleta wahindi na waarabu wamiliki uchumi.wameua viwanda vyote.tipa ipo wapi?mengine na0‹2a uvivu kutaj
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu naona wewe unakufa na hawa madogo duh .Wape nafasi wapumue .CCM imesha wamaliza hata cha kuwaeleza hatuna .
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimepata document moja yenye kuonesha vitu vyote tulivyokuwa navyo ambavyo matajiri wetu mambo leo wameviuza... tulikuwa na vitu vingi.
   
 9. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji tafadhali tuwekee hiyo nyaraka yenye orodha ya vyote tulivyokuwa navyo kwa ufahamu wa ambao bahati mbaya hatujui kinaga ubaga kisha tuchanganue/kuchambua na kuona mwelekeo wa nchi yetu though umekuwa mbaya day after day.
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Waligawana, wewe unasewma hilo mbona yapo mengi tu, tulikuwa na Wajapan na Matsushita wakitengeneza radio (Dudu proof) pamoja na betri ngoja MMJ alete list hapa .... .... .
   
 11. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hebu shusha nondo hapa, wakati bado wana maluelue ya kuondoka kwa RA.
   
 12. M

  Maengo JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasikia hvyo viwanda hao wawekezaji wao wamevifanya ma-godown cku hiz! Mim nadhan hii serikali yetu hawa viongozi wake nao wanagonga "kitu cha arusha"! Maana inahitaj moyo kuwakandamiza wenzio namna hii bila huruma!
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,779
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Wacha1,

  ..Matsushita nadhani ndio wamekuwa Panasonic sasa hivi.

  ..kama tungeendeleza kiwanda kile leo hii kungekuwa hakuna haja ya kuagiza electronic products kutoka Dubai.

  ..tatizo ni kwamba unaweza kukuta hicho kiwanda cha Matsushita kimeuzwa kwa "Mr.Kanjibai" ambaye amekigeuza kuwa godown la vyuma chakavu.

  ..pia kulikuwa na kiwanda cha majembe na zana za kilimo kikiitwa UFI. more than 60% ya wa-Tanzania ni wakulima wa jembe la mkono. sasa inakuwaje kiwanda cha majembe kinakufa, au hata hatuoni sababu ya kukifufua?
   
 14. M

  Moses msisia Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Viongozi hata wasome vipi lakini kama hawana vision ni takataka.nyerere alikuwa na vision ndiomaana alijenga hivi viwanda vyote.mungu amuweke mahari pema peponi
   
 15. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna gari la kijeshi likitwa Nyumbu lilikuwa linaundwa pale Kibaha.

  Land Rover Leyland Mbagala mhusika wa mwisho Leodigar Tenga Presidaa wa TFF.

  National Milling muulizeni Azam na Bahresa.

  Kiltex nchi nzima waulizeni kina Gulamali

  Mashamba ya mkonge akina Karimjee.

  TRC akina CCM na TRL (Mahindra) uchaguzi wa 2005

  Moproco, Canvas, magunia moshi, machine tools, etc etc, acha mabenki

  Orodha ni ndefu

  WAPENDE WASIPENDA WANA MASWALI YA KUJIBU HATA WAKIJITETEA KUWA WALIKUWA NA NIA NJEMA
   
 16. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mkuu, Nina swali:........sasa mkishapewa hayo majibu na maelezo ya kufa kwa mlolongo wa hivi viwanda then what?
  Kama watu hawatochukua hatua za kuingia mitaani si itabaki kuwa manung'uniko tuu hapa jamvini na mitaani wakati wenzenu wanaendelea kuitafuna nchi halafu wakijiuzulu wengine WANAZIRAI.......ha ha ha
   
 17. soine

  soine JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  General tyre arusha 2muulize nani?Yaan sijui hii nchi imelaaniwa, kila kizuri walichoasha mkoloni na Nyerere havipo tena.Natamani mjerumani arudi na bakora atembeze kwa viongozi wazembe.
   
Loading...