Viwanda vya magari, Haiwezekani Tanzania??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viwanda vya magari, Haiwezekani Tanzania???

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lekanjobe Kubinika, Sep 29, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani, nawaza kila wakati sipati jibu.
  Mwalimu JKN alithubutu kuanzisha utengenezaji wa magari ya NYATI hapa nchini akiwatumia wanajeshi kwa kuamini kwamba ni waaminifu zaidi na wanajituma kazi, tena kwamba labda wataweza kuwa wabunifu wakatengeneza na magari mbalimbali ya kivita na kupunguza ununuaji wa magari kutoka nje ya nchi. Nyati miaka yote hii ukibahatika utaambiwa imepita lakini ni ya jeshi. Technologia haijasambazwa na wala sidhani kama kuna mpango huo.

  Afrika kusini wanatengeneza magari aina zote ya kijapani, kijeremani na kadhalika na kujipatia ajira na vipuri kinafuu sana kiasi kwamba kuwa na gari kuu kuu sio tija kule. Botswana nao wanatengeneza magari. India ni third word pia na hata China lakini hata ndege zinatengenezwa kule.

  Kwa nini Tanzania haichukui hatua za makusudi kulobby makampuni makubwa yanayotengeneza magari Japan, China, India, German nk kuja kuwekeza nchini ambapo tunalo ardhi kubwa kabisa isiyofaa kwa kilimo lakini ingetumika kwa kazi za viwanda hivyo, nasi tukawa kama Japan siku moja kiviwanda kwa kununua au hata kuiba technologia zao na kuzikarabati ili kutengeneza made in TZ hapa hapa, badala yake tumeshupaza shingo kuleta magari ambayo ni mikweche tu kuja kujaza kama vyuma chakavu nchini, kama dumping area?

  Hivi hatuna wataalam wa kulobby uwekezaji mkubwa wa aina hiyo, ila wa kubangaiza wachimba madini ambao wanatuachia mashimo tu? Nadhani uzalendo ni tatizo kubwa TZ. Imekaa vipi hapo?
   
 2. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hata mimi Nimeliona hilo, Lakini wewe kwa unavyoona huu utawala wa CCM na JK Unadhani swala kama hilo
  litawezekana kweli?!. Kwa sasa nadhani Tungeshughulikia hili la Kubadili Uongozi. Hata hao wawekezaji hawatakubali
  ku input mtaji wao wakati soko la ndani (Raia) ni masikini wa kutupwa, Ufisadi na ukiritimba uliokuwepo kwenye
  Bandari zetu. Wafanyakazi watoke wapi? wakati kiwango na hali ya Elimu yetu Unaijua. MiundoMbinu Je ya kusafirish hizo mali ghafi?.
  -Namaliza kwa kusema "Usitie kitumbua cha mwenzio mchanga".
  Unataka Akina KINANA, MANJI, ROSTAM wasipate 10% za kuagizia Siri-Kali gari Mbovu.:mad2:
   
 3. s

  smilingpanda Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inavyoonekana watu wanaochangia hii mada wote watupuuu!
  hebu angalia statistica hala patapiacha kama wewe ingekua ndo billionare, ungejenga kiwanda katika nchi kama hii kweli?uchumi wa nchi haufai kama ukiniomba ushauri hata kuwanda cha penseli usifungue
   
 4. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Amehaidi kujenga Reli Mpya ya Kati na kwa Muda wa 5 yrs itakuwa imekamilika.

  Hivi huyu Kikwete anatuona sisi Watanzania ni MAZUZU saaaaaana................Daaaaaaaaaaaaaaaamn
   
 5. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  .

  Usemayo ni kweli mkuu Imma. Lakini hiyo hali itaendelea hata lini? Serikali badala ya kuwa na budget tegemezi kila mwaka ingekuwa na chanzo kizuri sana cha viwanda vua magari au mortor works. Ni vyanzo vya uhakika na ingesaidia kupandisha thamani ya shilingi yetu maana isingekuwa lazima kununua nje magari kwa pesa ya kigeni, mbali na kunyenyua viwango vya maisha ya wananchi wetu. Sasa Serikali mpya sijasikia hata ilani moja ya chama chochote inayolenga huko kwa kweli. Labda Chadema kwamba wanafikiria kujenga reli itakayowezesha kusafiri MWZ to DSM kwa masaa matatu. Bila shaka wanaweza kuanzisha viwanda vya chuma cha pua hapahapa kunusuru gharama kubwa ya kujenga miundombinu hiyo.

  Kweli CCM wamechoka kubuni vitu vipya, wapo kuendekeza ubabe uleule conservatively,lakini nao kama wanasikia (najua wakitaka wataachana na porojo na kufanya kweli) wanaweza kutumia nguvu yaporojo zao kulobby mambo makubwa yenye manufaa kwa wananchi wote, baala ya kujitetea kila kukicha kwamba wamefanikiwa wakati wanajua kabisa sio sana waongeayo. wangeiga mseto kama Zanzibar nadhani wangeanza kukomaa kiutaifa mioyoni mwao. Hivi sasa majigambo yamekaa kisiasa zaidi.
   
 6. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu, kila anachoahidi anasema atakifanya ndani ya miaka mitano akichaguliwa. Shinyanga ameahidi kujenga hospitali ya Rufaa wakati Bugando na KCMC ni rahisi kufika wagonjwa, na Mikoa ya kusini wamelilia hospitali ya Rufaa tangu enzi za Ng'walimu mpaka machozi yamewakauka. Shinyanga pia kaahidi kuwajengea Chuo Kikuu! Mambo kibao yanaahidiwa this time na anashangiiwa kwelikweli. Anasema wasiwachague wapinzani sababu ni vyama vya msimu, amesahau kwamba aliyoahidi 2005 mambo kibao hajayafanya lakini anasema yeye na wapabe wake ati tayari amefanya. Anajua maneno wanayotaka kusikia wasikilizaji wake na anamaximize that opportunity.

  Hata Moi na Gobachev walijiamini hivyo lakini ilibidi kusalimu amri na kukaa wakilalama pembeni. Makamba kwa kuficha aibu ya chama ameamua kupiga marufuku mwanaccm asihudhurie midahalo wasije wakafichua siri katika hasira zao wakizibuliwa na wananchi live. Kumbe kuna kuruka matope na ukakanyaga nanihii, samadi ya mtu?

  Mpaka 31 October sipatipicha ni ahadi alfu ngapi atakuwa amezitoa na sijui kama atakumbuka katoa wapi na wapi ahadi gani. Tushangilie tu kama mavuvuzela, sie watanzania halisi.
   
 7. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kulikuwa na nyumbu kule kibaha, iliota mbawa. nafikir labda tatizo ni uchumi kama wengine wanavyosema...kwasababu hata wenzetu wakenya walishaanzishaga cha kwao, kiliota mbaya. nionavo mimi, hii kitu inawezekana sana kama tutaweka incetives kwaajili ya vitu kama hivyo...makampuni ya magari mengi tu ya ulaya, america, china na japan yanaweza kuleta hapa na soko lipo kubwa sana. kama kiwanda cha magari kitajengwa hapa, soko lake ni kubwa kwani watafeed congo (64mill population),Rwanda, burundi, Kenya, Uganda, Zambia, mozambique na Tz. hili soko sio dogo....ni kubwa na linajitosheleza kabisa.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa mkuu ni mawazo finyu kufikiri kuwa ardhi peke yake ni kitega uchumi, NI nchi chache sana duniani ambazo hazina Ardhi ya kutosha, lakini still zimepiga hatua. Hong Kong, Singapore, San Marino. Ukisema unataka kumvutia mwekezaji kwa ajili ya ardhi utachekesha sana. Brazil na China wanavutia investements kwa cheap skilled labour, honest and diligent workers, good policies, safety of investements, cheap social emenities, maji, umeme, simu vyote ni very cheap na available 24/7/365. Hivi ni vichache tu, iangalie Tanzania kwa vigezo hivyo uone kama mwenye akili anaweza kuvutiwa kuja kuweka Tanzania ambako wezi wanaiba mpaka central bank. Ambako maji ni muhimu kuwepo ikulu na sio kiwandani au muhimbili.

  Juhudi zote zinazofanywa na Tanzania kuvutia uwekezaji ni kama kutaka kujaza ndoo kwa matone. Hakuna efforts zinazofanywa kwenye core issues, tunadeal na madogo madogo tu ya sera labda na ukazi na usajili wa makampuni.

  Mpaka sasa Tanzania haijafikia uwezo wa hata kuvutia kiwanda cha Adidas ambacho hakihitaji teknolojia kubwa au ardhi kubwa. Kaulize Shprote matatizo wanayokumana nayo mpaka wanakaribia kukimbia nchi, karibu kila siku wanalalamika kuwa wafanyakazi ni wadokozi kupita kiasi, serikali hiyo ni wazi kabisa ni kama tumehalalisha.

  Swali la kwanza ambalo wawekezaji huwa wanauliza ni umeme na maji. Tanzania tumeshindwa kuprovide maji na umeme hata kwa miezi 6 mfululizo, kwa sisi wenyewe je tutaweza kuprovide kwa wageni wakija? Kukatika kwa umeme na maji ni sehemu ya miasha yetu, how can you attract investments where you can not even manage drinking water?

  Sisi tumezoea uswahili swahili, yanayotufaa ni kama biashara za umachinga ambazo hazihitaji maji,umeme, ofisi mguu wako haa ukiwa peku unaenda tu.

  So forget about it. Alijaribu Nyerere lakini tulivuruga wenyewe, lazima tujifunze kujimanage kwanza then ndio tunaweza kuanza kufikiri hayo
   
 9. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kiwanada cha Magari si kipo South Africa, Kina supply Nchi ngapi Africa?
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Kama tungekuwa na nia ile ya nyerere ya Taifa huru na linalojitegemea, kuwa na gari la brand yetu ingeliwezekana kabisa.Lakini bado tunafikiria kijima kwamba lolote zuri lazima tufunge safari kulifuata ulaya.
  Kutengeneza gari letu ni ndoto isiyowezekana maana muda wa kuwekezakatika tafiti utakuwa haupo with this quick fix approaches we have developed now.
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Ni NYUMBU sio Nyati japo mnyama Nyati na Nyumbu karibu wa wafanane.
  Kiwanda kinafufuliwa ila sasa kitatengeneza zana za kisasa za kilimo pamoja na matrecta kwa ubia na kampuni fulani ya India.
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu smilingpanda, unachekesha sana. Lengo la kuanzisha mada kwa kawaida ni kutaka mawazo ya watu ili kuelimika pale mtu anapopwaya. Sasa inapotokea kipofu anamcheka kipofu mwenzake ni ukweli kwamba ni burudani hiyo na sio tena mafunzo tuyatafutayo, ingawa hapo napo tunaifunza kwamba nyan haoni nanihii yake.

  Nilifurahia kusoma sentensi ya kwanza inayoonyesha kwamba wote wanaochangia mada hii ni watupu, nikakaa mkao wa kula kupata mawazo mbadalaya mtu aliyesheheni ujuzi wa mambo. Nimekatishwa tamaa kuona unagoma kabisa kuleta mawazo yako na badala yake unasema hushauri mtu afuvgue hata kiwanda cha penseli. Huo sio utupu wa akili uliokubuhu kweli? Ni uwanja wa uchumi huu, nilitarajia utaeleza sababu za kutowezekana kufungua kiwanda chochote hata cha penseli lakini nikakumbana na nukta!

  Tanzania inaweza kuwa nchi ya viwanda kabisa, magari yakiwa mojawapo. Jana tu matrekta yameletwa toka India, tunashabikia ati. Kama tunafanya juhudi za kilimo kwanza, tunashindwa nini kuwekeza katika kufungua viwanda vya kutengeneza vitendeakazi vya kilimo kwanza ambavyo kila mwananchi ataweza kuvifikia kwa unafuu na kuvisustain? Hapo unahitaji kuelezwa? Kule SUma hawakaguliwi mahesabu sawa na wanavyokaguliwa wengine raia. Ni rahisi kuelekeza macho SUMA JKT kupitishia fedha za misaada na hata mikopo ambayo wananchi watakuja lipa baadayelakini kiasi kikubwa kinachopitia kule kikawa kinawanufaisha vigogo ambao wewe na mimi hatuwezi kuwauliza maswali ila watavimbiana matumbo hadi wapasuke. Umejionea mwenyewe meremeta, haiulizwi maswali sana kwa sababu ati mkuu alipiishia huko, sio kwa bahati mbaya bali kwa calculation. Kagoda kako wapi? Jamani, tanzania watu wake sio mbumbumbu sana, ndo maana tunasema Bongo hakua amani ila kuna utulivu, watu hawaulizi maswali kwa sababu ya hofu zao. Wamechagua bora maisha kwa sababu maisha bora ni kwa kundi fulani tu in practice.
   
 14. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pasco asante sana kwa kurekebisha jina hilo. Lakini wakati nasikia jana waziri mkuu alipokuwa anafungua matrekta pale Mwenge kwa Suma JKT, story ilikuwa kwamba Nyumbu wanafanya assembly na sio wanatengeneza. Tunachotaka sana sasa ni ndoto ya kutengeneza na sio kuunganisha parts ambazo zimetengenezwa nje ya nchi. Hao Nyumbu wangetufaa sana wangetumia upenyo huo wa kupata parts za kwanza wakajenga machinery za kutengeneza kila part na hatimaye uwezo wa kutengeneza na kuassemble kila trekta na magari hapohapo. Ndivyo wajapan walivyoanza nasasa hata waliowafundisha wanageuka wanafunzi wao.
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  hiyo Nyumbu imeuliwa na CIA, kwa kuogopa Tanzania wangekuja kuwa wako fit na wala wasingehitaji vifaa vingi vya kijeshi, kwani hiyo Nyumbu ingework out vizuri, ingekuwa raisi kuwa modified na kutengeneza mashine za aina mbalimbali mpaka vifaru
   
Loading...