Vivuli vitatu

Aisee Mshana ule uchawi wa kunyofoa kivuli cha mtu wanatumiaga hii knowledge ya vivuli??

Wanayofoa kivuli gani kati ya hivyo vitatu.

Kuna jamaa yangu mmoja nilisikia aliwahi kunyofolewa kivuli alikuwa anatembea kama "li kopo" tu, kuna ukweli juu ya hili??
 
Chochote kinachofanyika kwenye ishu za kiroho kuhusiana na vivuli ni kivuli kidogo kivuli cha ndani ndio hutumika
 
Mmh hii sijawahi kusikia nijuavyo ni kwamba vivuli huwa virefu ama vifupi kutokana na mzunguko wa jua lakini kukosa kabisa sijawahi kuona
Bro Mshana, hii nimehadithiwa na mtu kuwa yeye binafsi(alienihadithia) ilishawahi kumtokea. Hata katika jua kali hakuwa akikiona kivuli chake.
Mwenyewe nilishangaa sana.

Tafiti kuhusu hilo mkuu na ukipata chochote ukikileta hapa unitag plz
 
Inasemekana kuna watu hawana vivuli kwa sababu kuna stori moja kipindi gani kile cha Fredrick bundala Kuna stori ya jamaa alipewa dawa ili apenye ukutani kutokana na janga lililokuwa linamsibu ndani ya nyumba fulani.
Cha ajabu ilishindikana kwa sababu baada ya manuizi kuna nguvu ilikuwa inamsukuma, kama inapata ukinzani fulani halafu anarudishwa ndani.
Mtaalam ingawa alikuwa mtoto kiumri akamwambia hataweza kumsaidia zaidi kwa sababu kwa utaalam wake amegundua jamaa hana kivuli ambacho hutumika kwenye kupita sehemu ambazo hazipitiki kwa kawaida na huwa kinatangulia kimoja kwanza kati ya kivuli au mwili. Yaani kivuli ni kama mdhamini sijui tuseme.
 
Kivuli kidogo kivuli roho ndio kila kitu
 
Wewe ndio umeniogopesha jaman duuh! Mtu kafa wakati namuona!
Utani huo.

Hujawahi sikia mtu anasimama kwenye mwanga na hatokei kivuli, teh teh teh
Ni mambo ya kamati za ufundi tyuu.....
 
I like U,upo vizuri sana maana umenishawishi kiasi fulai kufuatilia Nyuzi zako kama mshana jr huwa nampenda sana mara nyingi ananiambia vitu navyotaka kusikia,naona na wewe umeingia pale napopataka
 
Hili nahitaji kulitafiti zaidi nisije nikapotosha
Kaka Mshana asante kwa somo la vivuli, ni kweli kabisa tangu nikiwa kijijini miaka ya 1993 nilikuwa nikijiuliza sana maana nilikuwa naona vivuli vyangu vitatu baadae nikapata majibu...ila pia nikaja kusikia uvumi, naita uvumi kwani bado sijajiridhisha iwapo ni kweli au la...eti Mamba anaweza kuua mnyama au mwanadamu kwa kukamata kivuli chake na hivyo mtu huyo kushindwa kukimbia na kujikuta akidakwa kiurahisi, je hili swala lina ukweli wowote ule???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…