Viumbe 10 vinavyobadili rangi zao kulingana na mazingira

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,065
Reaction score
61,398
Picha: viumbe 10 vinavyobadili rangi zao kulingana na mazingira

Uwezo wa kubadili rangi ya mwili kufanana na mazingira (camouflage) kwa baadhi ya viumbe duniani huwasaidia kujilinda dhidi ya maadui na pia katika kuwinda chakula chake. Kwa kuweza kubadilika huku, viumbe hivi huweza kuwa karibu kabisa na maadui zake au na windo lake bila kuonekana hivyo kumhakikishia usalama wake au kumrahishia kupata chakula.

Kuna viumbe wengi sana duniani wenye uwezo wa kubadilika rangi kufanana na mazingira anayokuwapo. Kwa sisi Watanzania, tumezoea kumuona kinyonga kwakuwa ndiye aliyepo kwenye mazingira yetu.

Zifuatazo ni picha 10 za viumbe wenye uwezo wa kufanya hivi:

Bundi

1-5.png

2. Mjusi aina ya Gecko

2.png

3. Gecko mwenye mkia unaofanana na majani (Leaf-Tailed Gecko)

3.png

4. Chavichavi aina ya Baron (Baron Caterpillar)

4-2.png

5. Farasi wa Baharini (Seahorse)

5-1.png

6. Buibui (Spider)

6.png

7. Mdudu Fimbo (Stick Insect)

7-1.png

8. Chura

8.png

9. Samaki Bapa (Stone Flounder)

9.png

10. Chui wa kwenye barafu (Snow Leopard)

10-2.png

Ashukuriwe mwenyezi MUNGU Kwa kutuwekea vitu vizuri namna hii hapa duniani. Je Mbinguni itakuwaje. Tumche MUNGU kama kweli mna Nia tukakutane tena Mbinguni.
 
Huo ni uwezo wa viumbe hai kufanya adaptability kwenye mazingira ili kuishi.

Camouflage ni moja kati ya ushahidi wa evolution maana inahusisha mabadiliko ya viumbe hai.

Huwezi kusema camouflage ni maajabu ya Mungu maana kama ungekuwa ni mpango wa Mungu mwenye upendo wote kwa viumbe vyake, asingiumba viumbe vyenye uadui vyenyewe kwa vyenyewe.
 
Kila mtu na mitizamo Yake mimi naamini kila kitu ambacho sio artificial made ni Mpango wa MUNGU.. Anzia kwenye galaxy tazama anga lilivyo. Jiulize kuhusu jua. Wingi wa nyota. UKIJA duniani cheki water cycle venye inakuwa. Ni mipango na akili za MUNGU hivyo sipati Shaka humu duniani maajabu ya viumbe wote MPANGILIO na Sifa zao ni mipango ya MUNGU
 
Huo ni uwezo wa viumbe hai kufanya adaptability kwenye mazingira ili kuishi.

Camouflage ni moja kati ya ushahidi wa evolution maana inahusisha mabadiliko ya viumbe hai.

Huwezi kusema camouflage ni maajabu ya Mungu maana kama ungekuwa ni mpango wa Mungu mwenye upendo wote kwa viumbe vyake, asingiumba viumbe vyenye uadui vyenyewe kwa vyenyewe.
Ushaanza hivyo.

Hapa tunaisubir ile timu yako ikiongozwa na Kiranga......
 
Huo ni uwezo wa viumbe hai kufanya adaptability kwenye mazingira ili kuishi.

Camouflage ni moja kati ya ushahidi wa evolution maana inahusisha mabadiliko ya viumbe hai.

Huwezi kusema camouflage ni maajabu ya Mungu maana kama ungekuwa ni mpango wa Mungu mwenye upendo wote kwa viumbe vyake, asingiumba viumbe vyenye uadui vyenyewe kwa vyenyewe.
Anachofanya Mungu si lazima afanye unavyotaka wewe,kwa akili utaona ni uadui lakini Yeye aliyeumba ameumba hali hiyo iwepo ili kuwe na manufaa fulani, ambayo wewe,kwa ufahamu wako mdogo waono sivyo.
 
Huo ni uwezo wa viumbe hai kufanya adaptability kwenye mazingira ili kuishi.

Camouflage ni moja kati ya ushahidi wa evolution maana inahusisha mabadiliko ya viumbe hai.

Huwezi kusema camouflage ni maajabu ya Mungu maana kama ungekuwa ni mpango wa Mungu mwenye upendo wote kwa viumbe vyake, asingiumba viumbe vyenye uadui vyenyewe kwa vyenyewe.
Mabadiliko hayo yasikufumbe macho MUNGU ndio anayaendesha kaka. Evolution imekuwapo na bado tutashuhudia changes nyingine nyingi. Subiri nikupe maajabu mengine ya MUNGU kwenye picha
 
Daah!..Nimemuona kinyonga tu hapo
Huyo farasi wa baharini sijaona chochote hapo
mkuu mbona anaonekana pale tu, kajifunga ule mkia wake kwenye mimea. Kama unaangaliaga channels za wanyama utamuona vzr na kumjua aisee
 
Hata mimi siajmuona mkuu, nikadha ni labda atakua ametoka nazidi kumsubiri akirudi nimtazame...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom