Vituo vya mwendokasi viwekwe ulinzi imara hasa Kimara

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
Tangu daladala zizuiwe kwenda maeneo ambayo gari za mwendokasi zinaenda vituo hivyo vimekuwa vikajaa watu wengi sana kipita kiasi.

Kibaya zaidi, mrundikano huo wa watu hauna ulinzi wa kutosha. Watu wanaingia bila hata kukaguliwa, ikitokea lolote, tunaweza kupoteza watu wengi kwa uzembe kabisa.

Kama baadhi ya bar/ club (disco) wanaweza kuweka ulinzi mzuri kwa wateja wao pindi uingiapo na kutoka basi naamini hata vituo vya mwendokasi vitawekwa ulinzi imara na hasahasa kituo cha kimara kwakuwa huwa kinakuwa na idadi kubwa sana ya watu.
 
Tutaufanyia kazi ushauri wako tatizo litakapotokea sasa hivi tuko buzy na vwonder
 
Wazo zuri.
Waanze kuweka na cctv camera kila kituo na kila basi.
 
Back
Top Bottom