Vitunguu vs viazi ulaya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitunguu vs viazi ulaya.

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Slave, Jul 25, 2012.

 1. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Nina mpango wa kulima kimojawapo lengo ni kulima heka 3 cha msingi nahitaji kujua zao lenye faida zaidi ya lingine,changamoto zake,soko pia muda nitakao utumia tangu kupanda mpaka kuvuna.
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unampango wa kulima sehemu gani mzee hiyo kitunguu? maana na mimi nafikiria kulima vitunguu
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nipo geita eneo lina udongo wa mfinyanzi,
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Kitunguu kinastawi sana kwenye eneo kavu kiasi hasa wakati wa kiangazi na kama kuna maji ya kutosha ya kumwagilia ila gharama za pembejeo ni kubwa sana. Kwa mfano kwa maeneo ya Singida ambako ni eneo la pili kwa Tanzania kwa kulima vitunguu mavno wakati wa kiangazi ni kama gunia 60 mpaka 80 na gharama ya kilimo ni shilingi laki 9 mpaka 1100000.

  Wakati wa masika gharama ya kulima ni kama shilingi 700000 mpaka 800000 lakini mavuno ni chini ya gunia 60.
  Gharama hupungua kutokna na kwamba huitaji kumwagilia lakini pia mavuno hushuka kutokana na kwamba kitunguu hakihitaji maji mengi.

  Eneo la Mang'ola Karatu ambako linaongoza kwa uzlishaji gharama za kilimo cha kitunguu ni kubwa kutokana na pembejeo kuwa aghali hasa madawa na mbolea (1,700,000 mmpaka 2,000,000 kwa eka) lakini uzalishaji ni mkubwa hadi gunia 160.

  Vitunguu vina bei nzuri sana hasa miezi ya September hadi march kutokana na maeneo ya uzalishaji mkubwa hasa Karatu uzalishaji kupungua.

  Lima lakini vitunguu vinahitaji uangalizi mkubwa................Process

  Kuotesha kitaluni mpaka wakati wa kung'oa ni siku 45
  Kupandikiza mpaka kuvuna ni miezi 3

  Note: mimi si mkulima lakini kuna study nilishawahi kuwa involved na maeno hayo nilifika. Maundumla na Slave mpo hapo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  salute you mkuu!!
   
 6. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Platozoom
  VP una data za kilimo cha vitunguu swaumu?
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hapana mkuu.....ni vitunguu maji tu.
   
 8. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Platozoom
  Soko la vitunguu maji liko vp ukifanya kwa large scale?
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Soko ni zuri sana ila inahitaji timing: Kwa mfano Vitunguu kutoka Tanzania huuzwa Kenya, Uganda, rwanda, Burundi, South Sudan!!

  Lakini bahati mbaya wakenya ndio huchangamkia kuuza vitunguu huko kwa wingi kuliko Watanzania. Ukifika soko la Kilombero Arusha kuna wastani wa Tani 50 mpaka 70 zinazopelekwa Kenya kuanzia miezi ya March mpaka October. Waakati mwingine wakenya huenda mashambani huko Karatu kuchukua wenyewe na hata waganda na wanyarwanda pia.

  Kwa hiyo unaweza kuona mtu kutoka Rwanda kwa umbali woote huo anaenda kuchukua vitunguu Karatu ama Singida. Lakiini inahitaji ucheze na hesabu za season.............Kwa mfano msimu wa mavuno na mauzo kwa Mkoa Wa Singida ni miezi ya February mpaka June baada ya hapo mavuno yanayoletwa kwenye soko la Ukombozi Singida (soko kuu la vitunguu ukanda wa kati) unakuwa chini sana mapaka kufikia magunia 50 kwa siku.

  Kwa Karatu mavuno yanakuwa makubwa miezi ya May mpaka October.........Ikifika October wanahifadhi vitunguu kwenye maghala............. ingawa miezi mingine uzalishaji unaendelea kwa kiasi kwa sababu wanatumia sana kilimo cha umwagiliaji.

  Ukiangalia hesabu hizo hapo utaona miezi ya October mpaka February kunakuwa na ombwe la upungufu kwa hiyo soko linakuwa zuri,..........kwa hiyo kama utalima kuanzia mwezi huu utavuna December na bei inakuwa nzuri tu.

  Tena kwa large scale ndiyo nzuri kwa sababu utaweza kuuza mwenyewe sokoni badala ya kusubiri walanguzi shambani kwako. Kifupi bei ya vitnguu kwa gunia 1 likiwa shambani kwa muda huu ni Tsh. 60000 mpaka 70,000 (singida)....soko la Arusha ni sh 70000 mpaka 80000.

  Kuna kingine nimeacha?
   
 10. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Platozoom
  Thanks boss you have touched everything I needed
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Asante. Labda pengine unataka kulima maeneo gani? na utatumia mvua au kumwagilia? na kama kumwagilia ni kwa kutumia pampu au matone?
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hivi maeneo ya pwani vitunguu vinastawi?
   
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Eneo la ruvu ni zuri sana vinastawi tena ukilima kiangazi ni safi sana
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nashukuru sana kwa info.

  Una contact yeyote mitaa ya huko Ruvu?
   
 15. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hapana but let me try nitakupa mrejesho
   
 16. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ardhi yako ni ya aina gani? Je upatikanaji wa maji upoje hapo? Ni sehemu gani upo au unaishi?
   
 17. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Nataka kulima dodoma mkuu nitakuwa nafanya irrigation bado nipo kwenye process za kuchimba kisima so ntakuwa kwa kuanzia ntakuwa namwagilia kwa mipira tu ila project ikisimama ntatumia sprinklers matone nadhani ni very expensive ni project ya 200 acres kuset drip irrigation kwenye 200 acres I can't afford it's too expensive na zao kubwa ninalofikiria kulima ni vitunguu na pilipili hoho that's why nikaulizia market ya vitunguu in a large scale.Any advice boss?
   
 18. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Haina shida kutumia mpira kwa kuanzia, market change yes lakini huwezi kukosa chochote. Kwa mfano kwenye study ambayo tumefanya ni kwamba wakati mwingine uzalishaji unakuwa mkubwa sana baadhi ya miezi kwa hiyo bei inashuka, nafikiri miezi niliyokuwekea hapo juu itakupa picha. Ni vyema utakapozalisha unaulizia masoko ya Kahama Dar na hata Mwanza ili ikiwezekana upeleke mwenyewe...........usihofu kuna wakulima wakubwa hasa wilaya ya Iramba hawahitaji hata kusafirisha wenyewe .pesa ije yenyewe walipo!

  Kuna mwingine naye nimemkuta amechimba kisima kikubwa sana kwa ajili ya pampu na ameanza na eka 60.

  Kama huna uzoefu kabisa ni vyema ukaanza na eka 100 nafikiri itakuwa vizuri zaidi. Hakikisha unapata mbegu nzuri (red bombay au planet onions) na mbegu zinapatikana madukani ama kwa wakulima (Iramba kuna wakulima wakubwa wanalima mbegu hasa vijiji vya Mwanga, Msingi n.k) wala usipate shida.

  Kwa Dodoma ni pazuri kwa sababu moja kubwa...ukame......vitunguu havitaki maji mengi ingawa ardhi ni vizuri ikawa na rutuba ili kuepuka gharama kubwa za mbolea.
   
 19. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Thanks kwa ushauri mkuu sitaanza kulima yote kwa pamoja nikishamaliza kuchimba kisima nitaanza kama na ekari 20 tu hivi au 30 ili kupata uzoefu kwanza na nitakuwa naongeza ukubwa wa eneo kadri ya muda unavyokwenda na matokeo ya awali yalivyo,Vitunguu vinahifadhika kwa muda gani? what is the maximum time unayoweza kuvitunza another alternative naona ni kuvitunza hadi soko liwe zuri kama haviharibiki mapema.Huyo jamaa na yeye yupo Dodoma? kama yes ningependa kumtembelea kujizolea uzoefu wa vitendo kidogo 60 acres kama anazimanage vizuri ni nyingi sana
   
 20. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Vinahifadhika mpaka miezi mitano. Kwa mfano Karatu ikifika mwezi wa Kumi wanaweka ghalani mpaka mwezi wa pili mwaka unaofuata ndipo wanaviuza...............Ila ujaribu kutengeneza ghala linalopitisha hewa vizuri na liwe kavu lili visioze ingawa hupungua uzito kiasi (lakini kwa soko la Kenya ndiyo huzingatia uzito).......Nazitafuta picha zinazoonyesha ghala lilivyo zikipatikana nitakutumia kwa PM (na ghala lenyewe linatengenezwa kwa mabanzi, miti na kuezekwa kwa nyasi) na hii ni Karatu ndiyo wanafanya kwa sababu wana uzalishaji mkubwa.

  Kuhusu huyo mkulima huyo yupo wilaya ya Iramba kiijiji cha Mwanga.............unapitia njia ya kinampanda na kupita barabara inayoenda Hydom..........Naiangalia namba yake nitakutumia PM
   
Loading...