Vituko vya watoto na ripoti za matokeo

Yes wazazi hawajui kwamba mtoto unatakiwa umuinspire kusoma ....

Kuna mdogo wetu ni product ya shule za kata yupo BOT sasa hivi
 
True story.

Kuna dogo alikuwa anafanya vibaya shuleni.

Akapeleka ripoti kwa baba yake. Ripoti mbaya.

Baba akamuuliza, imekuwaje umefanya vibaya hivi?

Mtoto akajibu, mimi sina akili, sina kumbukumbu. Nikisoma nasahau.

Baba akawa kama kakubali jibu. Hakuhoji zaidi.

Siku mbili zikapita, yule mtoto akaona mtu anasoma gazeti. Akaomba yule mtu akimaliza kusoma ampasie gazeti.

Dogo akawa anafunguka, anasema anataka kuangalia msimamo wa ligi, kwani Simba ina pointi hizi, Yanga ina pointi hizi, magoli ya kufunga mangapi, michezo iliyobakia mingapi, akawa anatiririka data nyingi za soccer pale.

Sasa yule baba yake pale pale akamuuliza. Wewe si umesema huna akili, shuleni ukisoma unasahau? Sasa haya mambo ya msimamo wa ligi mbona unayakumbuka vizuri sana?

Baba akasema, wewe tatizo lako si akili, akili unazo nzuri tu, tatizo lako huna interest na shule.
 
Kuna wanafunzi wanakariri nyimbo mitaani.Ila shuleni wanashindwa kukariri .
 

Hii ilinitokea pia
Tena nikambishia kabisa kwamba unafanya hivi yeye anasema anakumbuka siyo hivyo
Nikamkomalia akaandika jioni karudi page nzima imekatwa
Nikajifanya Nipo busy
 

Ila hii kitu ni ngumu kukubali

Binti yangu nae ni kama Hana interest na shule kabisa
Ameniomba nimnunulie mdoli ajifunze kusuka
Pamoja na vitu vya makeup

She spends a lot of time doing her hair, nimeongea nimechoka

Anataka heels na magauni ya designs
Anaweza badili nguo hata mara mbili

Hata sielewi namfanyaje akaze shuleni
 
Mpe anachopenda
 
Hahahahahahahahahahahahaha Kuna MTU karudi hapa nyumbani na matokeo yake......Ila kajitahidi Sana , sema muda wote anaongelea nahitaji ya shuleni ingawa shule ndio imefunga juzi.
 
Hii ilinitokea pia
Tena nikambishia kabisa kwamba unafanya hivi yeye anasema anakumbuka siyo hivyo
Nikamkomalia akaandika jioni karudi page nzima imekatwa
Nikajifanya Nipo busy

Yani unajisikia vibaya mno,bahati nzuri nilimdanganya kuwa siku hiyo nilikuwa nimekunywa β€œ chungu” (Red wine) huwa anaiita hivyo. So sikuwa vizuri,but next time sitokunywa kwanza chungu mpaka tumalize H/Work,akajibu β€œOk Mama next time be careful” lkn moyoni nilijisemea leo nimepuyanga mwanangu[emoji3][emoji3].
 
Hehe dogo langu kaleta report midterm 81, terminal 64.. average
Mdogo wangu bwana. [emoji23]
Na alivonipa io barua ya ada lazima payslip iwe imewekwa wakati wa kurudi. Nampangia siku nimpe somo.
 

Nenda nae taratibu but usimkatishe tamaa kwa hivyo anavyopenda,mwambie akiwa anasoma huku anafanya na hivyo apendavyo She will be Super Kid.
But namuona Naomi Campbell ajae ndani ya huyo mtoto wako.Yani hii ni talent yake na atafika mbali sana.

Wa kwangu mimi anabalance vyote,urembo na shule,anapenda kama ni kusukwa basi nywele ziwe ndefu hadi mgongoni,kwenye kuvaa sasa ndiyo usiseme, she is too selective hadi nilishasusa kununua nguo bila kumshirikisha.Sasa huwa nashangaa mbona mimi sina huo muda hata wa kukaa na kujipamba yeye anapata interest kutoka kwa nani na ni mtoto pekee tu.But nashukuru kwa darasani yuko vizuri zaidi.
 
Huyu wakwangu juzi aliniomba buku ya kitabu cha matokeo mwl wao aliwaagiza, nikampa. leo naulizia matokeo yako wapi anasema ile hela kapoteza baada ya kumbana sana anasema alinunua big boom za hela yote.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Zingatia comment ya walimu
 
Mtoto wa jirani kawa wa 60 kati ya wanafunzi 95 ,huku akiwa na wastani wa 85 na wa kwanza ana wastani wa 98

Hao ndiyo unakuta darasa zima wamepata Div one. Wanakuwa wanazidiana point tu. Kwa wastani huo hata angekuwa wa 80 ni poa tu kwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…