Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,433
- 38,402
WanaJF nawataka hali!
Katika harakati za kimasomo kuanzia primary (cc wengine hatujapitia zile shule zenu ambazo curricullum inasisitiza mtoto aimbe, anywe uji wa maziwa na baadae alale) hadi College au University kwa waliobahatika, huwa kuna vituko ama visanga wakati wa mitihani!
Kwa O-level na A - level sana sana ktk mitihani ya mwisho ya NECTA, na kwa upande wa vyuo visanga ama vituko unaweza kuviona kwenye semester exams ama hata final UE!
Mimi nimependa ku-share na wadau vile visanga ktk mitihani nilivoona ni vituko wakati wa harakati za kimasomo, vichache vyake ni hivi:
Tukumbushe visanga ama vituko wakati wa mitihani shuleni ama chuoni kwenu!
Katika harakati za kimasomo kuanzia primary (cc wengine hatujapitia zile shule zenu ambazo curricullum inasisitiza mtoto aimbe, anywe uji wa maziwa na baadae alale) hadi College au University kwa waliobahatika, huwa kuna vituko ama visanga wakati wa mitihani!
Kwa O-level na A - level sana sana ktk mitihani ya mwisho ya NECTA, na kwa upande wa vyuo visanga ama vituko unaweza kuviona kwenye semester exams ama hata final UE!
Mimi nimependa ku-share na wadau vile visanga ktk mitihani nilivoona ni vituko wakati wa harakati za kimasomo, vichache vyake ni hivi:
- kuna rafiki yangu mmoja, miaka yote ya kujuana pale shuleni, tumemzoea kuwa jamaa ni mpole na ni mwenye aibu sana, si kwa wasichana tu, mpaka kwa sisi boys wenzake! wakati tunafanya mtihani wa CSEE mwaka huo, ktk mtihani wa somo la Kiswahili, jamaa ktk chumba chetu cha mtihani alikuwa amekaa mbele kabisa (ktk alphabetical arrangement jina lake linaanza A)! Pepa ya Kiswahili inaendelea, utulivu uko juu, watu wako busy, kimya kimya! Ghafla jamaa anagonga meza kumuita Invigilator. Kuangalia mbele, ni mshikaji. Msimamizi akamsogelea na kumuuliza shida yake, jamaa akasema ana shida na Calculator! Msimamizi hakuyaamini masikio yake, akamuuliza tena unataka nini? Jamaa akasisitiza Calculator! Ktk somo la kiswahili haikutegemewa kuwa na mwanafunzi hata mmoja mwenye calculator, ikabidi msimamizi amuombe mwl mmoja wa pale pale shuleni kwetu akamletee jamaa calculator. Ikaletwa na akapewa! Darasa tulipigwa na taharuki na kuanza kuhaha tukitafuta ni wapi ktk mtihani ule wa Kiswahili, labda ile calculator imetajwa, hatukuona! Baada ya mtihani yule msimamizi na mwl walimwita awaeleze nini kazi ya ile calculator ktk mtihani wa Kiswahili, jamaa akawajibu alikuwa anatafuta TOTAL ya marks anazotarajia kuscore kwa pepa ile! Tulichoka.
- Hii ya pili nayo ilikuwa ktk pepa hizo hizo za NECTA za O-level. Sikumbuki ilikuwa ktk somo gani lakini katikati ya mtihani, ktk harakati za kusaidiana wanafunzi kwa wanafunzi ndani ya chumba cha mtihani. Jamaa jirani yangu kamgeukia mwenzake wa nyuma yake kumuomba msaada. Muomba msaada alisema kwa sauti na sote tukaskia (sijui kwa nini pamoja na ukubwa wa shule yetu na wingi wa wanafunzi, usimamizi ndani ya exam room huwa wa kawaida sana, sijui ni kwa vile govt sch ama vp, na kuna wakati tulisimamiwa na walimu wetu wa ndani). Jamaa kamuuliza mwenzie kama Zanzibar ipo Afrika! Wengi tuliskia lile swali, tulicheka sana, yaani mpaka msimamizi aka-mind! cha ajabu pepa nzima ya lile somo (sikumbuki somo gani) hakuna sehemu ama hata Multiple choices ilipotajwa zanzibar, achilia mbali hata ule upande wa maswali ya essay, Zanzibar haikutajwa pepa nzima!
- Hii nyingine boys ilitupa tabu sana! Ktk pepa ya Maths, tumepewa booklets vizuri! Tukapewa answer sheets. Tukaambiwa tujaze zile details za nje ya booklets, tukajaza vzr! Msimamizi akataja time, ile anaruhusu tuanze mtihani tu! Ghafla jamaa yetu mmoja anatetemeka! Mara anamaliza kutetemeka, akamwita msimamizi, anaomba ruhusa aende toilet! Yaani hata dk 5 bado tangu turuhusiwe kuanza pepa. Msimamizi akamkomalia aseme amepatwa na nini. Jamaa akawa anamgomea, wakabishana kama dk 10! Msimamizi akaenda kumwita mwl wa pale shule, mwl kuja akanong'ona na yule mwanafunzi! Baadae mwl nae akaongea na msimamizi! Wakawa wamefikia muafaka jamaa aruhusiwe kutoka, jamaa kasimama atoke (alikaa siti za nyuma) suruali chapa chapa eneo lote linalozunguka zip! Tulichoka!
- Chuoni nakumbuka kuna bidada aliweka kali "alijichora majibu" juu ya mapaja kisha akapiga min 1 matata! cha kupendeza zaidi yule bi dada alikuwa mrembo wa haja. Basi kila baada ya muda kuna invigilator anakuja kuangalia yale mapaja! kila baada ya muda anakuja, anaangalia as if na yeye anahamisha majibu kutoka ktk mapaja ya bidada! Mwisho wa pepa invigilator akamuita (tukaanza kutaharuki na kujua tayari mrembo wetu wa class kasha-disco), ukistaajabu ya Musa.......si akamuuliza kama yale majibu juu ya mapaja aliandika mwenyewe ama aliandikwa na mtu? Bidada akamjibu aliandikwa na mtu, invigilator akamwambia siku nyingine hiyo kazi apewe yeye!
Tukumbushe visanga ama vituko wakati wa mitihani shuleni ama chuoni kwenu!