Victor wa happy
JF-Expert Member
- Apr 24, 2013
- 11,660
- 11,664
duuuh apo anaongea akili yake inawaza newyork..usishangae kesho unaambiwa yupo majuu
MATONYA!? Haiji tokea!!!
Wakati bajeti ya wizara ya afya imekwisha somwa na kupitishwa bungeni kwa mwaka 2015/16, eti JK atahakikisha vifaa na madawa kwa ajili ya watu wenye albinism yanatengewa fedha na kununuliwa na kwamba vyote vitakuwa bure! Ahadi hii ameitoa leo huko Arusha katika sherehe ya siku ya kimataifa albinism!
Hiki ni kituko kwani waziri wake wa afya hakuzungumzia cho chote kuhusu suala hilo wakati wa bajeti ya afya! Na kama JK atalazimisha kutekelezwa kwa ahadi basi ama bajeti ya wizara itavurugika au itakuwa ahadi mpya ambayo haitatekelezeka hadi anamaliza muda wake October mwaka huu!!
Cha kujiuliza hivi JK hakomi kuahidi ahadi hewa au haoni aibu kwa kutotekelezeka kwa ahadi lukuki alizowaahidi wananchi nchini kote mwaka 2010?!
Bado anaendelea tu kuahidi! Huyu ataahidi hadi siku mwenzake anaapishwa!
Mkuu Ileje,
Wala hata hii usiite kituko, pia sioni kwamba ni ajabu kwangu mimi. Mwaka jana watu walikaa kwenye bunge kama hilihili, wakapitisha mambo kibao tu. Umesikia mwaka huu walivyosema? kama hujasikia basi ni kua HAKUNA lolote lililopitishwa mwaka jana likaenda kama lilivyopangwa.
Kifupi ni kua kikao cha bajeti ni formality na kutafuna hela tu, hua hakuna linalopangwa pale likaenda hivyohivyo. Serikali ndio inayoshikilia pesa. Inagawa pesa pale inapojisikia, sio kuangalia bajeti inasema nini.
Wenyewe wanasema tunatekeleza dharura tu, hii miradi mingine huwa inasimamiwa na wafadhili moja kwa moja
Na madhara yake ni kua wafadhili wakigoma kama walivyogoma bajeti inayoisha sababu ya ESCROW SAGA tunakosa dollar zao kwenye mzunguko kiasi cha kufanya dollar ziadimike na kua ghali.
Hivi unaamini kabisa bajeti inayosomwa bungeni ndio inayotekelezwa? Kama ulikuwa hujuwi zaidi ya asilimia 60 ya fedha za miradi ya maendeleo zilizopitishwa na bunge 2014/2015 hazijapelekwa kwenye halmashauri.kwa hiyo jk ni haki yake kutoa ahadi hiyo.kusoma bajeti ni kukamilisha ratiba tu na kulipana posho.
President anauwezo na mamlaka kikatiba kutamka lolote na likatekelezwa...over!
Kwenye fiscal policy Rais HAWEZI kutamka kitu ambacho hakipo kwenye bajeti ya Wizara wala kwenye bajeti kuu!La sivyo apeleke pesa zilizotengwa kwa MAAFA kwenye albino
JK huwa ana ahaidi tu!Kyela alituhaidi meli mpya na barabara Kikusya-Matema Beach hadi leo hamna kitu
Mma ngafu. Hata upembuzi yakinifu haujafanyika?