Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Daaah bora ungeliuaga chief hahaha ila ungekua keko saiv bure sana lile jamaa
Ata hio issue ilinisumbua kidogo jamii yake ilikuja juu sana ni vile mzee wangu alikuwa anakubalika sana issue ikaenda kindugu ndugu mpaka ikapoa kabisa wakati huo nipo zenji na nimeanza na school kabisa maana nilimpa nakozi za fasata km tatu hivi kidevu na kati moja akaangukia kisogo mtu mwenyewe alikuwa dhaifu shoga tu so akamwaga sana damu pale kila mtu akatoka mbio e neo lile watu walijua amekufa
 
Shoga albino alikuwepo mwanyamala very smart pale kamanyola bar...ibrahm kipofu anatembea mwendo mrefu pembezoni mwa road bila ya kuguswa na gari wala baiskel kufata madada poa kwa wahaya..kuna kinunga nae albino huyu alikuwa anacheza mpira balaa
Dah! Nimemkumbuka bhana huyo albino
 
Dah sina uhakika mkuu huyu alibino me nilikuwa simjui km shoga mkuu kuna siku alinikuta nimesimama maeneo yangu nimetoka gym si unajua kipindi kile lazima uwe mbavu ili uendane na mazingira akanishika dushee akaniambia tall mambo" nilichomfanya aisee awez kunisahau maisha yake yote alikwenda kuzindukia kwa dr mvungi pale maana ilikuwa maeneo ya vijana ndio kuna gym ya kishua..wazee wake walikuwa wanalala kwa mzee wangu week nzima mpaka kijana wao alipopata nafuu me nilivuka maji kabisa
Samahani mkuu hivi bi mkubwa wako aliwahi kuwa mjumbe?
 
Mpaka sasa hivi sijaona sehemu zimetajwa bei za simu.

Sijawahi kununua simu dukani.

Simu yangu ya kwanza ya gharama kabisa kununua ni G Tide nilinunua 40,000 kwa Inno.

Ya pili 50,000 ilikua ndiyo enzi za simu za kichina kubwa kama kiganja.

Ya tatu 40,000 nokia 6300.

Siku hizi simu za range kama Samsung Galaxy s4, A3, J7, Note 2,3, LG G1,G2, G3, HTC one M8, one m9, Huawei p7, 8, 9, Y5, Y6 ni 150 au chini na haizidi 200, ukinunua zaidi ya hapo tunakucheka. S5, Note 4, 5, ni 200 mwisho 250.

Simu ambazo hazina soko ni Nokia Lumia na Blackberry, BlackBerry Torch mwaka 2013 ilikua bila 300 hujainyanyua siku hizi 40,000 sijaona ikizidi 60,000.

Iphone 5 iwe C au S haizidi 200, 6 iwe plus au nini unakula kuanzia 200 haitazidi 300. Iphone 7 kupanda sizioni kabisa.

Itel sisemi.

Nilikuta humu mtu anauza Tecno C5 200k nikamwambia yesu atarudi atakukuta nayo, huku hiyo ni 40,000 mpaka 100,000 kutegemea na muonekano wake. C8, J8, C9 ni range ya 130 mpaka 150.

Tecno H6, J7, zinaanzia 40,000 haizidi 80,000. Y3, y4, 30,000.

Huawei 530 na 500 ni 40,000

aisee hadi nachoka.

Kipindi kile ilikua ukipost tu humu inakuja ile 'Sent by simu hiyo hiyo using jamiiforums mobile app' mi nilikua naangalia baadhi ya majibu ya kifedhuli ya watu halafu naangalia na thamani ya simu yake.

Hawafanani
Mkuu niunganishe na raia anayepush phone 6+
 
kumbukumbu yangu ya nyamala ni ule uwanja wa B...yani lolote linaweza kutokea kabla,katikati na baada ya mechi
wahuni wanavuta bangi mbele ya askari
enzi hizo gemu za ndondo watu wanakuwa na majeshi mastaa,akina lunyamila,mohamed hussein mmachinga,said msasu(huyu alitokea timu ya kitaa chetu hadi akaenda simba)
tulikuwa tunatembea kwa mguu tokea mwembechai,tunadondokea tandale kwa tumbo flani,tunavuka kimto cha kizushi(daraja mti mmoja mwembamba,usipokuwa good balancer unadondokea majini ukitoka kambale wamekudandia nguoni)
kwa ufupi mwananyamala ni nyoko..my favorite spot ni masai these days....nyapu nje nje
mwembechai timu yako ilikuwa ipi KAGERA RANGERA au MESSINA ya mtaa kondoa
kombe la kinesi hiyo
fainali kagera na messina penart ya mwisho tunaangalia nje ya uzio wa mabati maana lazima ngumi zilike
MAMAANGU mdogo alikuwa anakaa NYUMA ya gholofa kongwe so nilikuwa nakuja sana magomeni weekend kwa brozangu
hicho kidaraja ukishavuka unatokea uwanja wa rasco ukipandisha juu unatokea ngilangwa au kwa jolijo mnavuka mto ng'ombe noma sana hiyo
 
Back
Top Bottom