Vituko vya Mwananyamala: Mtaa kwa mtaa (special thread)

Kinyozi maarufu DILUNGA
alikuwa ananyoa pale chini ya mwembe karibu na geti la mochwari ya mwananyamala...
Kabla teknolojia haijachukua kasi yake..
Weekend mnapangwa foleni...
Aliweka kioo chake ktk mwembe ilikuwa lazima nijiangalie ktk kile kioo nikiwa natokea juu DSSD nashuka chini
 
Vibaka mashuhuri kama akina ng'ombe bado wapo?
Kuna vibaka wengine mashuhuri hao ni kinondoni walikua mapacha duuh hao walikua hawachezi mbali na kwa manyanya.. walipewa jina la "vipacha" kwa ajili ukibaka.
Kuna siku usiku wa manane nakatiza viuchochoro vya vijana pale niko na demu umeme umekatika giza totoro mara mbele naona kuna njemba mbili kugeuka nyuma njemba 2 zingine nikajisemea leo nimekwisha kuja kucheck vizuri kumbe ni vipacha viko na vibaka wengine wawili.Uzuri vipacha vinanifahamu basi ikabidi vikaushe vikasema braza mauza uza tuachie basi hata ya mjani nikavipa buku 2 ikabidi nisindikizwe hadi home na vibaka ili nisjepatwa na wengine.
 
Kulikuwa na Muuza magazeti maarufu alikuwa anaitwa Salehe..
Alikuwa anauza magazeti nyumba kwa nyumba...
Daah ni siku nyingi sana...
Sijui naye alikuja kupotelea wapi..
Saiz amebaki yule Kibonge wa geti la Hospitali...
Namkumbuka muuza magazeti na yule mwingine mpiga picha anayetembea nyumba kwa nyumba...huyu dula mbabe bondia unamkumbuka kipindi anauza mkaa tunamuita kiroba?
 
Na kuna jamaa wa mingo za bia za kuvizia MK, Mango au Masai wote karibu wanatokea Mwananyamala nawakumbuka Idd kibonge na rafiki yake Yero; na kuna jamaa mkongo huyo yuko hapo keshakua mbongo akiitwa Jozee duuh.
 
Namkumbuka muuza magazeti na yule mwingine mpiga picha anayetembea nyumba kwa nyumba...huyu dula mbabe bondia unamkumbuka kipindi anauza mkaa tunamuita kiroba?
Ndiyo
Wauza mkaa wote walikuwa wanakaa upande Makaburi..
Ukikutana jioni washafunga hesabu unawasahau...
Wameulamba hatari...
 
Ofisi na kampuni za mifukoni: Eneo lote la Kinondoni Mkwajuni mpaka Biafra ni hatari kwa shughuli hizo.. Utataka nini ukose.. Mihuri ya siri? Nyaraka za serikali? Mikataba mbalimbali, nyaraka za kusafisha mizigo.. Pesa bandia, madini bandia.. Kila kitu hukosi hapo. Mitaa hiyo ni maarufu kwa madaktari feki, Wanausalama, polisi, wanajeshi mahakimu, wanasheria, wabunge hata mawaziri nk
Nimeelewa kwa nini The bold alitumia Scene ya kufungua ofisi fake mahali pale kwenye ile 'movie' ya Vipepeo Weusi: Mkakati namba...!
 
Kuna mwaka alikuja siti binti kasiri yule mkenya aliyekuwa anaigiza ktk igizo la TAUSI unakumbuka wanafunzi wa B tulikwenda ktk ile nyumba mpaka ukuta wa ile nyumba ukadondoka..maeneo mwanymala kule kuna sehem inaitwa magodoro
nakumbuka halaf unamkumbuka yule mchina aliyekuwa anakuja kufundisha dini na kiswahili chake
 
nakumbuka halaf unamkumbuka yule mchina aliyekuwa anakuja kufundisha dini na kiswahili chake
namkumbuka sana then kuna Tajir mmoja sijui alitokea mkoa gani kipindi kile alikuja kuanzisha secondary mwananyamla B..inaitwa sijui Avot centre uniform sketi nyekundu shule yake ilikuwa hapa uwanjani B karibu na geti la uwanjani kuna kichochoro unatokea sokoni mapinduzi madirisha ya madarasa yana tizamana na gesti dah ile shule ata miezi 3 aikufika naisi ilikufa
 
Back
Top Bottom