Vituko vya mochwari

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,865
730,452
Jamani jamani jamani pale mahali paoneni hivi hivi, pana vibweka pale mwanzo mwisho, na Kama kuna viumbe wana visa vibaya marehemu wanaongoza
Kama mtu alikuwa malaya kwenye uhai wake hata akifa maiti yake huwa na pozi zile zile.

Mtu katili hufa na ukatili wake na hata pale mochwari maiti yake huwa na dalili zote.... Wabishi matapeli wachawi nk hubaki na hizi tabia hata pale ndani
Huwezi amini maiti uliyokuwa umeiweka vizuri tu ukaikuta imechanua miguu.

,ama maiti nyingine kuikuta tu imegeuka yenyewe ...! Unakaa na kujiuliza na mshangao mkubwa hii imegeuka saa ngapi? Ama imegeuzwa ? na nani?

Mbaya zaidi ni zile zenye tabia ya kukonyeza.... Yani live kabisa ukiangalia unaona marehemu anakukonyeza.... Walevi mateja mabosi nk wote wapo kwenye kile chumba.

Na kuna wakati mochwari attendant hujua kabisa kwamba Leo mochwari patafurika ama mzigo utakuwa mdogo.... Ni uzoefu tu wa kazi.

Nikimkumbuka yale niliyokutana nayo wakati ule naona kabisa kuna mengi bado hatuyajui.
d8a579ed333254ea09d729cf18d44a46.jpg
 
Back
Top Bottom