Vituko vya 'Maandazi Republic'?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,282
117,233
Wazungu kuna nchi wanaziita 'Banana Republics'
Sababu nchi hizo zinakuaga very unstable na corrupt sana...na kawaida huwa
zinaongozwa na dikteta asietaka ushauri.....na hali ya kiuchumi huwa mbaya sana...

Sifa nyingine ya Banana Republic huwa haziheshimu katiba wala utawala wa Sheria

lolote linaweza kutokea bila kujali sheria zinasemaje...

Nimejiuliza baada ya kuona yoote tuliyo yaona wiki hii na wiki iliyopita
hatupo kweli 'maandazi Republic'?

Hivi kuna nchi yoyote ile ambayo ina vituko kama vyetu?

Kuandaa mapambio na vibwagizo eti kwenye mkutano wa kupambana na madawa ya kulevya?
kweli?

Wale wale watuhumiwa nao kugeuka 'wasemaji ' na wapambanaji?
kweli?

kumbe hata bajeti tu ya mapambano ni sifuri..

Vituko vimekuwa viingi kwenye hiii Maandazi Republic...
full mizaha na kukomoana tu....hakuna kitu serious kabisa

Hela wanazotuhumiwa kupewa kina TID zilitolewa na nani na kutoka fungu gani?
 
Kuna viongozi ambao wamejifungia ndani hawataki kwenda nje wakajifunze angalau kidogo, wengine wana mawazo ya kizamani, they live in their own bubble ya kuamini mzungu mbaya, matajiri wabaya, hate hate hate, kila kitu kidogo ni hasira. Na hata wakiomba kura watapewa tena na tena kwa kua wananchi asilimia kubwa wapo kwenye the same bubble, kati ya wapiga kura wote unaweza kuta 20% tu ndio wanajielewa, wengine wote wanaamini propaganda. Its a really tough battle.
 
Tumeshadumbukiza miguu yote 2 bado kuzama tu tutaweza kuogelea na kujinasua ! Ndani ya maji haya ya ziwa ambayo hayana mwelekeo!!
 
Mkuu kwani Tz. unaionaje? Hakuna utawala wa sheria? hakuna demokrasia? Katiba haifuatwi? Kwani kuna uonevu? kama hayo hakuna basi hatuko ktk kundi lolote kati ya hayo mawili, ILA kama hayo hapo basi sisi ni....... nini vile eti?
 
Kuna viongozi ambao wamejifungia ndani hawataki kwenda nje wakajifunze angalau kidogo, wengine wana mawazo ya kizamani, they live in their own bubble ya kuamini mzungu mbaya, matajiri wabaya, hate hate hate, kila kitu kidogo ni hasira. Na hata wakiomba kura watapewa tena na tena kwa kua wananchi asilimia kubwa wapo kwenye the same bubble, kati ya wapiga kura wote unaweza kuta 20% tu ndio wanajielewa, wengine wote wanaamini propaganda. Its a really tough battle.

Hii bubble aisee inawadanganya mno
 
Back
Top Bottom