Vituko vya Corona Afrika

Vituko vya Corona Afrika

Tuna rais wa ajabu sana kweli kuhamasisha watu wajifukize dawa za kienyeji watapona corona au ndo sababu kaamua kuongoza nchi kutokea mafichoni ili apate muda wa kujifukiza?
Ngoja muda ufike tuanze kuanguka kama kuku wa mdondo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio kila tiba inayotoka kwa Mzungu Ndio inafaa kwa afya ya binadamu. Usipende kuabudu sana vitu vyao nakuona ndivyo bora na kudharau ushauri unaotolewa na mu Afrika mwenzio
 
Ni wazi sasa baadhi ya nchi ya kiafrika zimeamua kwenda kinyume na kanuni za kimataifa za kitaalam za kupambana na virus vya Corona. Ni kama vile Afrika inataka kutoka kivyake na kuithibitishia dunia kuwa AFRIKA IKIAMUA INAWEZA...

Huko Madagascar rais wa nchi hiyo ametangaza kuwa majani ya aina fulani ya chai yanatibu virus vya Corona huku akithibitisha wagonjwa 20 kupona.. Shirika la afya duniani limesema dawa hiyo haijathibitishwa kitaalam na inaweza kuwa na madhara makubwa kiafya

Nchini Tanzania mkuu wa nchi amesisitiza maombi na matumizi ya kuvukiza maji ya mvuke kama tiba na kinga sahihi ya corona lakini wakati huo huo waziri wake wa afya akisema kuvukiza sio njia sahihi na salama kwakuwa njia ya hewa haikuumbwa kupitisha moto... Wananchi wamebaki na kizungumkuti kikubwa kushindwa kujua wamuamini nani

Nchini DRC wao wametoka kivyao... Wanasema virus vya Corona ni uzushi mtupu na wananchi wameanza kuhamasishana kwa njia ya muziki na kula bata.. Kwamba ukijichanganya kwenye kucheza na kurukaruka (dhana ya kutoka jasho) kama ile ya kuvukiza tuu... Virus vinakimbia

Nchini Uganda hali ni tofauti kidogo.. Spika wa Bunge la nchi hiyo ameidhinisha USD million 3 kinyume na maagizo ya mahakama ili zikasaidie mapambano dhidi ya corona huku kila mbunge akiingiziwa USD 3000 toka kwenye hilo fungu.. Ukostaajabu ya Musa utaona ya firauni.. Eti Museveni hana habari na hilo jambo na amewatahadharisha wabunge wasitumie hizo pesa kwakuwa ni kinyume na maamuzi ya mahakama

Huku mitaani mafundi nguo wamepata biashara ya kushona barakoa.. Usalama wake ni kiasi gani? Hilo sio muhimu kwa sasa.. Kikubwa kuziba pua... Utadhani corona ina harufu...
Vyovyote iwavyo Afrika inajaribu kutoa ujumbe fulani kwa mabeberu na hii inaweza kuwa mwanzo wa kuwindana hasa kama njia za Afrika zitafanya kazi.. Lakini mpaka hii corona ipite tutashuhudia mengi mno
Je umesikia na hiki kilio cha nchi za Afrika kutaka kusamehewa madeni yake makubwa na mabeberu ili pesa hizo zitumike kupambana na korona?

Nje ya mada: corona imeua biashara ya lipstick

Jr
Duuuh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila tiba inayotoka kwa Mzungu Ndio inafaa kwa afya ya binadamu. Usipende kuabudu sana vitu vyao nakuona ndivyo bora na kudharau ushauri unaotolewa na mu Afrika mwenzio

Hiyo ndio tabia yetu mzee, usishangae hilo. Tumefikia hatua mbaya sana kiasi kwamba hata kujiamini kwetu kumetoweka kabisa. Kila wasemalo wazungu tunaliona kama limetoka mbinguni na hata kupima ukweli wake hatujisumbui. Hii ni mbaya sana.
Jiulize kama lockdown kweli ilikuwa hatua sahihi, kwanini nchi hizo ndio zimeathirika sana? Wee ugonjwa unaoenea kwa njia ya hewa unajifungia ndani kweli?? Labda kama wangesema tujitumbukize kwenye mapipa yasiyoingiza hewa kabisa.
Tuache hii dharau dhidi yetu wenyewe, sio kila mzungu ni padre.
 
Ndo nini hiki

Jr
Kunakuwa na mchanganyiko wa miti mbali mbali ambayo hutumika kama tiba, huchemshwa pamoja kwenye chungu then mgonjwa au muhusika hutakiwa kujivukiza mvuke unaotoka kwenye hicho chungu. Naamini unaelewa isipokuwa unahitaji maelezo tu!

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
.
tapatalk_1587674127987.jpg


Jr
 
Korona toka ushindwe kwa jina la Yesu


Jr
 
Back
Top Bottom