Vituko vya binti wa kazi toka Tanga

Latoya

JF-Expert Member
Apr 18, 2013
660
457
Habari wanajamvi.Ni takribani siku nne sasa nimeletewa binti wa kazi toka Tanga.alipofika nilimwacha azoee mazingira kabla hajaanza kazi rasmi hivyo shughul zote nilikuwa nafanya mwenyewe huku nikimwelekeza.Kwa muda huo wa siku mbili za mwanzo nilimpa uhuru wa kupumzika na kujitazamia tv tu sebuleni.

kimbembe kimeanza jana tumeamka vizuri nikaandaa chai tukanywa then nikampa vyombo akaoshe.Baada ya kifungua kinywa nikatoka kuelekea sokoni kununua mahitaji ila nikamwachia maagizo kuwa asafishe chumba anacholala kwani alikuwa anakitumia mdogo wangu kabla ya kwenda home likizo.Nimerudi masaa mawili baadae nakuta yuko bize na tv chumba hajasafisha nikamwamuru kuzima tv na kwenda safisha chumba hiko.Alitii ingawa kwa shingo upande.Baadae nikapika msosi tukala,imefika jioni akaanza lia kuwa mwili unamuwasha na madai yake ni nyama niliyopika,kuwa anahisi nimemlisha kitimoto.Nikamwambia hapana nimepika nyama ya kawaida tu nikamwambia labda itakuwa mzio,nikamshauri akoge then apumzike,kama ataendelea washwa siku ya pili basi tutakwenda hospital tujue tatizo.

Tumeamka vyema leo baada ya usafi,nikaandaa kifungua kinywa ambacho alikula kidogo tu akaacha akidai ameshiba.Basi nikamtuma buchani akalete nyama tupike cha mchana kwa kuwa tulikuwa tunatarajia wageni.akaenda akaleta nyama nikaandaa pilau,punde wageni wetu wakawakawasili tukaandaa meza,ila akagoma kula akidai ameshiba.

Nikawakirimu wageni na kuendelea na story mbili tatu za maisha.ilipofika saa 8 nikamfata chumbani na kumsihi aje kula bado akasisitiza ameshiba,basi nikamwambia apate kinywaji akakubali.Nikiwa naendelea ongea na wageni akaniaga anaenda nje kupunga upepo,lol haikupita nusu saa napigiwa simu na babake kuwa kwann nataka muua mwanae na njaa kwani toka asubuhi hajala,nikamuuliza hayo maneno katoa wapi akasema jirani yangu kampigia simu kumweleza hilo.

Nikabaki nimepigwa butwaa nisijue la kusema.Sasa wandugu naombeni mawazo yenu nifanye nini,kwani binti nilimwita nikamwuliza akasema anaogopa kula chakula kwangu nisoje mpa najisi ilhali mie hata kitimoto situmii.Nilimwagizia chipsi mayai kwa mangi ndo akala.Sema nimebaki na maswali mengi kichwani.Je nimrudishe kwao? Nitaishije na mtu wa aina hii?Naombeni uzoefu.
 
Huyo binti hana nia ya kazi!.ulikosea kumwacha bila kazi kwa mda na kumpikia.anataka kurudi kwao.mrudishe tafuta mwingine,kitendo cha yeye mwenyewe kwenda kununua nyama kisha anadai najisi ni hila.pia kitendo cha kujenga ukaribu na majirani kupewa simu na kupeleka umbeya kwao haifai.pia hamuwezi kukaa wakati hamuaminiani.hakwamini nawewe humwamini.piga chini agiza mwingine usisubutu kumpikia mfanyakazi! labda kama hajui unamfundisha iwe mara moja moja.
 
Huyo ni wa kurudishwa kwao tu... Katafute mfanyakazi kafr mwenzako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom