Vituko vishaanza bunge maalum la katiba

Okinawa

Senior Member
Nov 16, 2009
174
29
Kutokana na wajumbe wengine waliochaguliwa kwa kujuana leo kuna mjumbe mmoja aliruhusiwa kumuuliza mgombe nafasi ya Mwenyekiti wa Muda ndugu Kificho na kumuuliza:
"Ndugu mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Muda umetuomba wote tukupe kura za ndiyo, je mimi nikikupa kura yangu utafurahi? ".

Ndugu wananchi hilo ndilo lilikuwa swali la mjumbe huyo. Huyo ndiye watanzania wanamtegemea kutengeneza Katiba kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa. Nilimshangaa yule Mwenyekiti Mwanamama naye kulikubali swali la kijinga namna hiyo.

Watanzania tutegemee vituko vingi kwenye bunge hili. Tatizo kubwa likiwa ni kuteuliwa wajumbe kwa kujuana na kulipa fadhila badala ya kuchagua mtu anayeweza kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya Taifa.

Ni bora tungekuwa na wajumbe 250 wenye moyo wa uzalendo wa kutengeneza katiba kwa maslahi mapana ya taifa hili kwa ajili ya kulinda raslimali zetu zinazoibiwa kila siku kwa mikataba mibovu kuliko hawa zaidi ya 600 ambao wengi wao ni wale wa kushangilia 'ndiyooooo' au kuuliza maswali ya kitoto na kijinga kama alilouliza hule 'mjinga'. Naomba wanamkumbuka jina lake wamtaje hapa hadharani.
 
Halafu tunajifanya kushangaa Kenya, Rwanda na Uganda wakitupotezea!! Hayo ni MAJANGA!!
 
Back
Top Bottom